Nakupinga vibaya sana ! Lipo atakalolifanya , ni hili la kudidimiza maendeleo kwa kusigina katiba ya nchi .
Hata mimi hilo ndilo jambo ninaloliona la hatari mno ambalo hata kwa yale mazuri aliyoyafanya yataelekea kuangamia.
Tutambue kuwa hakuna nchi yoyote duniani iliyofanikiwa kupata maendeleo makubwa bila kuwa na utawala bora.
Tunaposema utawala bora maana yake ni utawala unaozingatia sheria.
Kwa bahati mbaya sana ambayo watanzania walio wengi wanaogopa kumwambia ukweli huu kuwa kitendo cha Mkuu wa nchi kuisigina waziwazi Katiba yetu ya nchi ambayo aliapa kuilinda na kuitii ndiko kutakakoliangamiza Taifa letu.
Inashangaza kwa mtu kama Tundu Lissu, Mwanasheria mahiri akieleza ukweli namna Rais wetu anavyoongoza nchi na kutoa matamko yanayovunja Katiba ya nchi waziwazi, badala ya kufanyia kazi ushauri huo badala yake Rais huyu anatumia vyombo vyake vya dola kuhakikisha kuwa watu wa design ya Tundu Lissu hawapati nafasi ya kuendelea kuuleza ukweli na badala yake anaendelea kurundikiwa kesi kibao zisizo na kichwa wala miguu.
Njia pekee ya Taifa hili kupata maendeleo endelevu ni lazima Rais wetu aongoze nchi kwa misingi ya sheria.
Kwa trend tunayoenda nayo ambayo watu wanakuwa na hofu tupu kutoweza kujua leo Rais ataibuka na tamko lipi, ni mwendo wa hatari sana.
Tumeshuhudia matamko kadhaa ya Rais wetu ambayo yameleta kizaazaa.
Nitataja baadhi yake.
1. Alipiga marufuku uagizaji sukari nje ya nchi ambapo ilisababisha bei ya sukari kupanda nchi nzima, ambapo hadi hivi leo bei bado haijastabilize.
2. Ametoa matamko yenye utata mkubwa tena yenye kuvunja Katiba ya nchi kuhusu zuio la kutofanyika shughuli zozote za kisiasa kwa vyama vya upinzani hadi mwaka 2020 na baadaye akalegeza msimamo kidogo kwa kudai wanaruhusiwa wanasiasa walioshinda nafasi kama za ubunge na udiwani ndiyo wanaoruhusiwa kufanya siasa tena kwenye maeneo yale yale tu waliposhinda, ambapo kauli zote hizo 2 ni za uvunjaji wa wazi wa Katiba ya nchi.
Nakumbuka Mwalimu Nyerere wakati wa uhai wake aliwahi kutuusia kupitia kwenye hotuba zake kuwa Tunapaswa kuchagua Rais ambaye ataiheshimu na kuitii Katiba ambayo ameapa kuitii na Mwalimu Nyerere akaendelea kueleza kuwa iwapo atatokea Rais ambaye hataki kuitii na kuiheshimu Katiba yetu Mwalimu Alisema Rais wa aina hiyo HATUFAI.......