Endeleeni kumpamba na kumsifia, ila time will tell.Kwa aliyofanya mpaka sasa hivi yanatosha, sema kwasababu nawe ni muhanga wa vyeti feki ulizoea kula kijanja janja unaleta fyoko fyoko zako hapo, hapa haina kudevera devera Magufuli mbele kwa mbele.
Kabla hata ya kumshukuru ninaye Muamini, naomba Mods Msiupoteze uzi huu ili iwe kumbukumbu katika jukwaa hili.
Wana Jukwaa, niseme na nikiri tu kwamba katika makosa yote ambayo aliyo fanya Kikwete katika mihula yake kama kashfa za ufisadi, kukithiri kwa rushwa, kushuka kwa thamani ya Shilingi, na hata mengine uyajuayo ninaweza kumsamehe na kuyasahau makosa hayo kabisaa.
Kosa kubwa ambalo hata nishikiwe bunduki ambalo sitaweza kumsamehe JK ni la kutuletea Magufuli. Nasema hivi kwa sababu Kkwete anamjua Magufuli fika.
Natambua kwamba majeraha ambayo aliyaacha Kikwete alipaswa kutuletea mtu wa kuyatibu kwa utaalamu na busara ya hali ya juu. Lakini Ninacho shuhudia mimi Majeraha yale yameanza kuongezeka taratibu na kuwa makubwa zaidi ingawa kwa njia nyingine tofauti na JK.
Magufuli huyu ambaye tunamuona Shujaa wa kupambana na Ufisadi na kutaka maendeleo ya gafla hatofanikiwa chochote zaidi ya kulalamika kwenye majukwaa na kipiga mikwara.
Naamini asilimia kubwa ya wanajukwaaa hili wengi ni wasomi. Na kama ni ndivyo naamini mnatambua kwamba nchi huongozwa na Mipango thubuti (Strategies) yenye kutoa dira na njia ya kufikia yale tunayo yataka.
Tuliambiwa serikali hii ni ya viwanda, serikali ya kutoa ajira kupitia viwanda, watu wafanye kazi (hapakazi tu). Lakini mpaka sasa hatuoni mikakati ya viwanda hivyo vitakujaje eidha wavijenge serikali au wawekezaji wa ndani na nje ya nchi. Mara nyingi tumemshuhudia waziri wa viwanda akisimulia kapokea simu nyingi kutoka kwa wawekezaji wa nje na tena wengine wamemfata kwenye ofisi yake wakitaka ardhi kwa ajili ya kuwekeza.
Ukweli ni kwamba wawekezaji wengi wameingia uoga na wengine kutokomeaa kutokana na uchumi wa nchi hautabiriki na hasa pia serikali kupanga bei za bidhaa za soko, kubana matumizi na kutoa vitisho vingi kwa wawekezaji waliopo.
Bado hali haijakaa sawa, tunaambiwa Serikali kuamia dodoma ndani ya mwezi mmoja tena kwa amri pasipo mipango yenye kukamilisha hilo. Bado najiuliza ajenda za awamu hii ni zipi hasa, yaani tuna target kufika wapi hasa?
Rais amekuwa akitoa matamko kila siku mpaka wakati mwingine anapoongea unajikaza mwili mzima ukihofu ataongea nini, yaani unaogopa asitoe kauli zenye ukakasi ambazo mataifa mengine kutushangaaa. Yaani haipiti siku bila kusikia Magufuli kasema nini.
Hakuna mipango na mikakati thabiti ya kutufikisha kule tunapo pataka au anapopataka yeye, inaonekana kwamba dereva tuliye naye anayo nia ya kufika ila hajui njia ya kupita kufika tunapotaka, anabahatisha njia, lakini mbaya zaidi abiria tuliopo ndani ya gari ni wachache tunaona tunapotea ila tunahofu ya kumweleza dereva huyu njia sahihi kwa maana mbili, kwanza tunajua hawezi kutusikiliza zaidi ya kichapo, pili abiria wengine ambao ni wengi watatubwatukia kwa matusi mengi na kutukejeli kwamba nasi tunautaa udereva.
Nimalizie kwa kusema kwamba, nchi hujengwa kwa misingi na mipango thabiti. Marekani ya leo anaweza kuongoza hata Jay Z au Kanye West na Marekani isitetereke, kwa sababu moja tu, Nchi ina mising, Kila Rais ajaye pamoja na ajenda zake hukua ajenda kuu za nchi kwenye meza yake ambayo lazima aitekelezee. kuna mengiya kueleza lakini naomba niishiee hapa, ila wote ambao tutausoma uzi huu tusipoteze kumbukumbu, hakuna kitakacho badilika iwe ni maisha bora, uchumi, huduma za jamii, demokrasia, haki za binadamu na vitu vingine vinavyo maanisha maendeleo, zaidi ya kudidimia.
Tutakwenda kwa mikwara na kuanzisha ajenda ambazo zitakufa kibudu kwa muda mfupi, na kwakua CCM ina take advantages ya uoga na umbumbumbu wa watanzania waliowengi, 2020 watabadili maneno tu, kwamba ni HAPA NI KAZI ZAIDI.
Ibilisi
Hizo ni legacy za Jk sio magu! Kumbuka mikataba ya standard gauge ilishasainiwa na Jk, na Jk ndo amewatafuta hao wachina sio magu! Magu hajawahi kukanyaga chinamkuu barabara,reli havina IMPACT kwa mwananchi wa kawaida?
Acha kuongopa wewe hao wachina walimfuata Magufuli Ofisini kwake na kusaini MoU we unasemaje,kwani kila alichokiendea JK huko ng'ambo lazima kifanikiwe, si ingejengwa wakati huo;huo mkataba wa Ujenzi wenyewe umesainiwa juzijuzi tu hapo Magogoni mbele ya Magufuli na tena ni baada ya Magufuli kuwashawishi hao wachina watie mkono we unatuongopea hapa, be current ndugu follow the news.....SOMA HAPA Tanzania na China zatiliana saini hati ya makubaliano ya ushirikiano (MoU) ujenzi wa reli ya kati | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania TodayHizo ni legacy za Jk sio magu! Kumbuka mikataba ya standard gauge ilishasainiwa na Jk, na Jk ndo amewatafuta hao wachina sio magu! Magu hajawahi kukanyaga china
Kafanya mengi yapi? Kufukuza watumishi Wa umma bila kujali kanuni za utumishi. Maisha yamekuwa magumu usipime.Natamani wazungu watutawale kuliko kutawaliwa na kiongozi ambaye hajui anakoelekeaKamma nini we unamaanisha.
Maana watu washaona mengi keshafanya hadi sasa. Sasa wewe unasemea kitu gani hasa.
Mi mpaka sasa nasubiri laptop lakini naona kimya.
Kwa kweli JK ni zaidi ya kiongozi.
Yule jamaa alifanya makubwa sana. Watu wamedanganywa sana kuwa kila kitu awamu ya nne kilikua kibaya.
Mikataba yote ya leo ni ya J K , ndio maana bado wachina ndio wanaofanya kila kitu kwenye miradi ya maendeleo.
Watu wanabwabwaja tu kuwa pato la nchi limeongezeka ila hawajui kuwa pato hili linatoka katika vyanzo alivyoacha JK. Na vyanzo vingi vinapungua kwa kasi kwa maana kuwa miaka miwili ijayo pato la nchi linaweza likashuka huku wananchi wakiwa hawana fedha za kuendesha maisha yao wenyewe.
Enzi za JK fedha zilikuwa ni nyingi sana na alikua ni mjanja wa kutafuta fedha na Serikali yake ilikua kubwa na matumizi makubwa. Leo serikali ndogo na matumizi madogo lakini hakuna mikakati ya kupata fedha.Mzunguko wa fedha unapungua sana miongoni mwa wananchi.
JK alipoingia aliboresha sana maisha ya wafanyakazi na wengi wakajenga na kumiliki magari. Mkapa na JK waliwakuta wanyakazi wakiwa na maisha duni sana huku bei za vitu zikiwa juu.
Mfano TV ya kichogo nchi 21 ilikua inauzwa 350,000/- wakati mshahara take home wa mfanyakazi wa chini ulikua sh 41,000/- elfu arobaini na moja. Mkapa akajitahidi kupandisha kidogo mpaka 119,000/ JK akaongeza kwa kasi zaidi na kuongeza mabenki huku akiruhusu mikopo kwa wafanyakazi.
Akaruhusu bidhaa nyingi ziingiezwa kwa mitaji ya wafanyabiashara kwa kodi kidogo na misamaha ya kodi. Watu wakaweza kuununua TV kwa bei ndogo,radio zikashuka bei. Wafanyakazi wakamiliki nyumba na magari kutokana bidhaa kuuzwa kwa bei ndogo. Leo hii mpaka sukari haikamatiki. Mishahara ni ile ile ya JK huku bei za vitu zikipaa juu.
Watu wanazidi kuwachukia matajiri kwa wimbo wa wakwepa kodi.
Ni lazima kwanza serikali iwawezeshe wananchi wake kwa kuwapa misamaha ya kodi ili wapate faida kubwa wakuze mitaji badae wawe na mitaji mikubwa ya kuanzisha viwanda na kutoa ajira kwa wengine.Miaka ijayo nchi yetu ajira zitakua ni ngumu sana, bila sekta binafsi nchi itakua na watu wengi wasio na ajira na waoga wa kufanya biashara.
Kodi zilipaswa zipunguzwa zaidi. Kama JK analaumiwa hakukusanya kodi pesa za matumizi alikua anatoa wapi?
Nadhani ingekua ni vyema serikali ingepunguza kodi na kupunguza matumizi kama alivyofanya Magufuli. Wakaflsanye kodi kwa kasi lakini wasiiongeze iliwezekana waipunguze.
Ninachokioni ni Kwamba JPM ni kama greda la kusawazisha barabara. Yupo ajaye baada yake 2020 kuweka mipango ya kitaifa ya kuinua uchumi wa nchi na maisha ya watanzania yawe ya raha , furaha na amani.
Kila mtu atafurahia kazi ya mikono yake.
Tanzania mpya inakuja.
Hilo nalo usifie kwanza subiri kidogo..........Kubwa ambalo amelifanya na halija leta madhara ni kuhakikisha huduma za umeme kwa watumiani wadogo hasa majumbani zina shuka, hilo ndilo nililo liona mimi na halija leta madhara yeyote.
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] u can't be serious,eti elimu bureNadhani si kweli kwamba hatafanya lolote kwa sababu mpaka sasa ameshafanya tunayaona kama vile kuongeza makusanyo ya mapato,kudhibiti kwa kiasi ufisadi na matumizi mabaya ya fedha na madaraka,kuasisi miradi mikubwa kv Tanga Ug pipeline,Ujenzi wa Central line ambao unaanza soon,Elimu bure,Madawati,kuwasepesha Wazembe kazini,kupunguza majizi bandarini etc binafsi naona ameshafanya mengi...Labda ungesema hatakamilisha yote miongoni mwa aloahidi kuyafanya.Over.
Kamtumbua KitwangaHivi mpaka sasa amefanya nini cha kumkomboa mwananchi wa hali ya nchi, ni ongezeko la kodi au?
Kafanya mengi yapi? Kufukuza watumishi Wa umma bila kujali kanuni za utumishi. Maisha yamekuwa magumu usipime.Natamani wazungu watutawale kuliko kutawaliwa na kiongozi ambaye hajui anakoelekea