Rais Magufuli hatofanya lolote ndani ya miaka 5

Rais Magufuli hatofanya lolote ndani ya miaka 5

General Mangi

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2013
Posts
15,317
Reaction score
23,192
Kabla hata ya kumshukuru ninaye Muamini, naomba Mods Msiupoteze uzi huu ili iwe kumbukumbu katika jukwaa hili.

Wana Jukwaa, niseme na nikiri tu kwamba katika makosa yote ambayo aliyo fanya Kikwete katika mihula yake kama kashfa za ufisadi, kukithiri kwa rushwa, kushuka kwa thamani ya Shilingi, na hata mengine uyajuayo ninaweza kumsamehe na kuyasahau makosa hayo kabisaa.

Kosa kubwa ambalo hata nishikiwe bunduki ambalo sitaweza kumsamehe JK ni la kutuletea Magufuli. Nasema hivi kwa sababu Kkwete anamjua Magufuli fika.

Natambua kwamba majeraha ambayo aliyaacha Kikwete alipaswa kutuletea mtu wa kuyatibu kwa utaalamu na busara ya hali ya juu. Lakini Ninacho shuhudia mimi Majeraha yale yameanza kuongezeka taratibu na kuwa makubwa zaidi ingawa kwa njia nyingine tofauti na JK.

Magufuli huyu ambaye tunamuona Shujaa wa kupambana na Ufisadi na kutaka maendeleo ya gafla hatofanikiwa chochote zaidi ya kulalamika kwenye majukwaa na kipiga mikwara.

Naamini asilimia kubwa ya wanajukwaaa hili wengi ni wasomi. Na kama ni ndivyo naamini mnatambua kwamba nchi huongozwa na Mipango thubuti (Strategies) yenye kutoa dira na njia ya kufikia yale tunayo yataka.

Tuliambiwa serikali hii ni ya viwanda, serikali ya kutoa ajira kupitia viwanda, watu wafanye kazi (hapakazi tu). Lakini mpaka sasa hatuoni mikakati ya viwanda hivyo vitakujaje eidha wavijenge serikali au wawekezaji wa ndani na nje ya nchi. Mara nyingi tumemshuhudia waziri wa viwanda akisimulia kapokea simu nyingi kutoka kwa wawekezaji wa nje na tena wengine wamemfata kwenye ofisi yake wakitaka ardhi kwa ajili ya kuwekeza.
Ukweli ni kwamba wawekezaji wengi wameingia uoga na wengine kutokomeaa kutokana na uchumi wa nchi hautabiriki na hasa pia serikali kupanga bei za bidhaa za soko, kubana matumizi na kutoa vitisho vingi kwa wawekezaji waliopo.

Bado hali haijakaa sawa, tunaambiwa Serikali kuamia dodoma ndani ya mwezi mmoja tena kwa amri pasipo mipango yenye kukamilisha hilo. Bado najiuliza ajenda za awamu hii ni zipi hasa, yaani tuna target kufika wapi hasa?

Rais amekuwa akitoa matamko kila siku mpaka wakati mwingine anapoongea unajikaza mwili mzima ukihofu ataongea nini, yaani unaogopa asitoe kauli zenye ukakasi ambazo mataifa mengine kutushangaaa. Yaani haipiti siku bila kusikia Magufuli kasema nini.

Hakuna mipango na mikakati thabiti ya kutufikisha kule tunapo pataka au anapopataka yeye, inaonekana kwamba dereva tuliye naye anayo nia ya kufika ila hajui njia ya kupita kufika tunapotaka, anabahatisha njia, lakini mbaya zaidi abiria tuliopo ndani ya gari ni wachache tunaona tunapotea ila tunahofu ya kumweleza dereva huyu njia sahihi kwa maana mbili, kwanza tunajua hawezi kutusikiliza zaidi ya kichapo, pili abiria wengine ambao ni wengi watatubwatukia kwa matusi mengi na kutukejeli kwamba nasi tunautaa udereva.

Nimalizie kwa kusema kwamba, nchi hujengwa kwa misingi na mipango thabiti. Marekani ya leo anaweza kuongoza hata Jay Z au Kanye West na Marekani isitetereke, kwa sababu moja tu, Nchi ina mising, Kila Rais ajaye pamoja na ajenda zake hukuta ajenda kuu za nchi kwenye meza yake ambayo lazima aitekelezee. kuna mengi ya kueleza lakini naomba niishiee hapa, ila wote ambao tutausoma uzi huu tusipoteze kumbukumbu, hakuna kitakacho badilika iwe ni maisha bora, uchumi, huduma za jamii, demokrasia, haki za binadamu na vitu vingine vinavyo maanisha maendeleo, zaidi ya kudidimia.

Tutakwenda kwa mikwara na kuanzisha ajenda ambazo zitakufa kibudu kwa muda mfupi, na kwakua CCM ina take advantages ya uoga na umbumbumbu wa watanzania waliowengi, 2020 watabadili maneno tu, kwamba ni HAPA NI KAZI ZAIDI.

Ibilisi
 
Kwa aliyofanya mpaka sasa hivi yanatosha, sema kwasababu nawe ni muhanga wa vyeti feki ulizoea kula kijanja janja unaleta fyoko fyoko zako hapo, hapa haina kudevera devera Magufuli mbele kwa mbele.
 
Kwa aliyofanya mpaka sasa hivi yanatosha, sema kwasababu nawe ni muhanga wa vyeti feki ulizoea kula kijanja janja unaleta fyoko fyoko zako hapo, hapa haina kudevera devera Magufuli mbele kwa mbele.
Mkuu Ndio kwanza nimemaliza chuo mwaka huu, Sina mpango hata wa kuandaa CV ya kuomba kazi, nilicho somea ni ajira tosha, nilijua haya ,mapema.

Mark my words, hata watendaji aliowatumbua ambao wengi hakuna sababu za msingi hakuna mabadiliko yoyote tutakayo shuhudia kwa miaka hii mi 5
 
Jibu hoja mkuu....
karibu,
Nadhani si kweli kwamba hatafanya lolote kwa sababu mpaka sasa ameshafanya tunayaona kama vile kuongeza makusanyo ya mapato,kudhibiti kwa kiasi ufisadi na matumizi mabaya ya fedha na madaraka,kuasisi miradi mikubwa kv Tanga Ug pipeline,Ujenzi wa Central line ambao unaanza soon,Elimu bure,Madawati,kuwasepesha Wazembe kazini,kupunguza majizi bandarini etc binafsi naona ameshafanya mengi...Labda ungesema hatakamilisha yote miongoni mwa aloahidi kuyafanya.Over.
 
Jmaaa hasomeki formula yake vizuri lakini kajitahidi baadhi ya mambo tusimkatishe tamaa na kukasirisha watu, mfano Wafanyakazi hewa, fyeti feki, madawati shuleni, naia yatafuata madarasa, ubadhirifu kupunguzwa, rushwa kadhaa mfano ya yule masamaki na ule wa risiti feki za milioni saba kwa dakika na kuua vyama vya upinzani (Hii ni ajenda kuu pia japokuwa haijadiliwi wala haisemwi popote)....mengine yanakuja
 
Back
Top Bottom