Rais Magufuli hatofanya lolote ndani ya miaka 5

Rais Magufuli hatofanya lolote ndani ya miaka 5

mkuu aliyofanya ni kidogo sana kuliko aliyo yasema, mbaya zaidi yanamezwa na ambayo yanaendeleaa.
Tatizo tunapoteza kumbukumbuu
We mtu wa ajabu sana mpaka ugeuzwe jinsia ndio utambue kwamba amefanya kubwa. Magufuli kafanya mengi sana kwa mfupi. Ameweka elimu bure, amerejesha nidhamu ya kazi kwa watumishi wa umma, amewezesha upatikanaji wa madawati, ameokoa mabilioni ya fedha za umma zilizokuwa zitumike kwa mambo yasiyo ya msingi mfano sherehe za uhuru na muungano, safari za nje nk. Magufuli hata kabla ya kuwa rais alikuwa akifanya mambo mengi sana yaliyo na faida kwa watanzania.
 
Reli ya kisasa,ndege mpya 2,elimu bure,Barabara ya mwenge posta,barabara ya mwanza airport,mapato kuongezeka, kuongeza fedha za maendeleo nk .
 
Mtoa mada nimekuunga mkono 100%, kwa sababu zifuatazo:- kwanza binafsi natokea kilimanjaro, nilitegemea mawazo ya rais kuwa nchi ya viwanda ingekwenda sambamba na kuboresha kilimo. Mpk sasa kule kilimanjaro zao la kahawa kama limesahaulika kbs, rais angeelekez nguvu kwenye kilimo atilie mkazo wananchi tufufue yale mazao ya kibiashara kama kawaha, mkonge, pamba yalimwe kwa wingi tuuze soko la dunia tupate pesa za kigeni na pia tupate raw materials ya kutosha kwa viwanda vinavyoanzishwa.

Na uhakika mpk aondoke zao la kahawa halitafufuka am sure
 
Watu wengine hata mfanyiwe nini, mtakosoa tu hivi naomba kuuliza ni nani amenunua ndege za atc, nani kaleta mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda, ni nani amesaini pesa ya kujenga reli ya kati, nani ameziba mianya ya rushwa na wakwepa kodi, nani amepambana na tatizo la wafanyakazi hewa.
Watz tuwe wakweli huyu mtu amefanya yote hayo ndani ya miezi nane tu ni nani unaefikiria angeweza kufanya yote hayo hata Lowassa kamsifia juzi.
 
Huwa najiuliza sana na sipati jibu, huwa natamani ni m face JK nimuulize why? Kwamba alitaka kutukomoa? Tulikuwa tunaelekea kuzuri but siyo huku tunakoenda sasa! Ushawahi kuwa na kitu ambacho hukutegemea? Ndo what kinachofanyika! Anauliza mi si ndo mkubwa wa kitengo flani! Na hao jamaa wako mbinguni ina maana walikuwa wanaishi kama malaika sasa nawaamuru waje wafungue kituo!
Why JK? Jamaa hakutegemea! Mi naamini ntapata kile nachoamini na nikipata sintoduwaa bali ntafanya kazi ila jamaa hakutegemea! Why JK?
 
upo sahihi ngoja tuendelee cheki hii movie
 
magu ni mr walk and talk na sio mr walk the talk.
 
Hadi sasa ameshafanya mambo ma3 makubwa sana;
1. Effective tax collection
2. Discipline in public funds expenditure
3. Discipline in public service

Hata asipofanya lingine la maana haya tu yanatosha
 
mi kusema ukweli sijataka kuvaa kikoi kutabiri mabaya. Cause sijakata tamaa bado. My

Sina utabiri mbaya kuhusu JPM.

Bado natafiti, Nataka kujua ukweli ni upi haswa...?
Je Udikteta ni njia bora ama sio.?hope Huyu magu atatusaidia kufikiri tofauti siku zijazo.
Though najua ana miaka kumi tangu sasa.

Kimsingi nataka kuamini kua kama alitaka kuongoza hahitaji sisi tumshauri cha kufanya cause alishajipanga na anajua nini akifanye kwa wakati. Na kutopokea kwake ushauri ni dalili ya komfidensi aliyonayo. Ili kama mambo yakija kuharibika pengine itakua easy kusema yeye kaharibu na kama yatafanikiwa tutasema yeye ndiye kafanya haya yote.

Wengi wetu tunataka kumchakachua kama jk kwa mawazo mbadala ambayo yatachelewesha utendaji wake. Kitu ambacho kwa mipasuko iliyopo nchini tutarudi kwenye matatizo ya jk tena.
Sijaona hata western counttries zikimlaumu kwa maamuzi yake. Which means hata wanapo upiga vita ushoga, hizi nchi haziachi kutoa misaada yao tena.

Tumpe pumzi, bado nahisi kuna taasisi bila style yake wananchi tutaumia sana kwenye kupata huduma kwa heshima zote.
Mfano tanesco, hospitali, maji, Ardhi, na mahakamani na mavyuoni.

Pia mlundikano wa iliterates maofisini umedhorotesha sana ufanisi nchini. Jamaa acha aikarabati nchi.
Cdm sio kwamba ni mahiri bali utawala uliopita ulikua wa hovyo sana kiasi magepu mengi yalijionesha waziwazi.

Msingi wa kusema hili ni kwasababu kuna wakati bajeti yao pendekezi mbadala ilionekana ina mapungufu fulani wakati wa dk.slaa kama ile ya ccm.
 
Nakupinga vibaya sana ! Lipo atakalolifanya , ni hili la kudidimiza maendeleo kwa kusigina katiba ya nchi .
 
Nasema mwenda wazimu ndio ataunga mkono hoja hii. Mpaka miaka mitano iishe JPM atakuwa amefanya mengi kuliko tawala za awamu ya pili, tatu nne na awamu ya sita pia.
Unamaanisha atakuwa ametoa matamko mengi kuliko watawala wa awamu zote sio!
 
Back
Top Bottom