johnsonmgaya
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 2,818
- 3,731
Dedication "usinipangie" by Baghdad, zimuendee mkulu popote alipo
Akiongea leo wakati anaapisha wateule wapya Ikulu. Amesema mitandao yetu ni ya ovyoovyo na inaandika mambo ya ajabu ajabu.
"Jana nimesoma kwenye mitandao ya kijamii kuwa eti Mwakyembe hawezi kuja kuapishwa, na mimi nilikuwa nasubiri asifike nione. ''Sasa si huyu hapa amefika"
Ameongeza kuwa..... "Jana kuna mwingine kapost Kinana kuongea na waandishi wa habari kesho, wakati ukweli Kinana nimemtuma India Kwa siku kumi na mbili"
Amewaonya wamiliki wa vyombo vya habari kwa kuzipa nafasi habari mbaya mbaya tu, "mfano kuna tv habari za migogoro ya wafugaji ndio wanaipa nafasi kubwa zaidi, amesema hayupo tayari kuvumilia hayo mambo.
Ameshangaa magazeti ya leo kujaza mbele picha ya mtu mmoja, na hata kurasa za ndani kujaza habari hiyo hiyo.
Amemwambia Mwakyembe akasimamie kwa umakini hasa tasnia ya habari, amesema hayupo tayari kuona nchi ikichezewa..l
Ameshangaa kutangaza kutoandika habari za mtu, wakati huo huo wanaandika mbaya tu.... "Kama hamtaki kumwandika si masiandike yote mazuri na mabaya"
Halotel wapo vyema bado Tsh10000 unapata 10GB mwezi mzima unakula news ni bampa to bampa to the extent [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]Ndio maana bando wamezipunguza ili tusitumie mitandao. Washindwe walegee
Nyie ndio mnaotakiwa kuonyooshwa haswa haswa, shida zako yeye ndio atakutatulia.
Mjifunze maisha mapya, kwasababu atazidi kubana hadi mjue kwamba..
Hapa kazi tu
Na muwe na heshima mkiwaongelea viongozi wetu
Hasira ikikuzidi jipige vibao vya uso na zitaisha.
Magufuli oyeee
Jombaa C.I.A ndugu zako mbona unajiamini sanaa, maneno yako hayo!!!!!!Atulie aacha udaku anataka nini huku wakati yeye ni mchapa kazi....aseme na kiki yake iliyobuma ile...
Tafuta kuna video/picha alikua na kikwete wanatoa shukrani kabla ya kuapishwa, alikua na kitochi. Insta kaijua 2016 huyo.....naamini kabisa wapo WASOMI WA HADHI YA PROFESOR wanaopingana na kasi ya ukuaji wa TECHNOLOGY..!!
Kuwa msomi haimaanishi kuwa wewe lazima uwe mpenda maendeleo.
Tujaribu kuwauliza MARAFIKI zake na MUKULU...kipindi kile akiwa waziri...
ISIJEKUWA ALIKUWA NA SIMU YA TOCHI...namaanisha simu isiyokuwa na uwezo wa INTERNET....
Yawezekana MUKULU ni mgeni wa hizi simu za SMARTPHONE..
Tukajikuta tunampasha habari mtu aliyesaidiwa kufunguliwa akaunti ya FACEBOOK...INSTAGRAM...TWITTER ..N.K.
TUFANYENI UTAFITI....maana sidhani ata kama anayo LAPTOP...!?
Ni MASHAKA YANGU...
Wewe nawe ni kati ya wagonjwa subiri utumwe india kutibiwa.Unamlazimisha Pascal aandike unachokijua wewe?Una hakika anakijua ujuacho wewe?Kama wewe unajua huo ufisadi mbona hujaandika?Unataka Pascal aende kutoa ushahidi wa kusikia?PASCAL MAYALLA ACHA UZUSHI, WE KILA SIKU NI KUMSEMA RAIS TU, JIKITE KATIKA ISSUES BANA, UFISADI NI MWINGI SANA, MFANO YULE NDUGU YENU WA DAWASCO. YULE LUHEMEJA. MBONA HAMUENDI HUKO MUANDIKE YAKE? AU KWA SABB ANAWAPOOZA
Huo ujinga wenu wa kukosa adabu hauwaogezei..kijana yeyote mwenye adabu aliyeelimika hawezi andika upuuzi wa namna hii..kuheshimu watu achilia mbali umri na hadhi zao zngn haihitaji kufundishwa darasani, nchi hii ina tatizo kubwa la attitude za vijana..na revolution hii ya habari ndio imeongeza ujinga mwingi kichwani, badala ya kuitumia kwa tija imekuwa jukwaa la kukejeli na kutukana watu..na tusingempata Rais tuliye naye sasa nchi hii ingefukiwa, family zetu ziko so loose wazazi wako busy na maisha malezi kwa watoto na kuwafundisha ipasavyo ni ndoto kwao..iko shida kubwa ukisoma michango ya vijana, elimu yetu haifuti ujinga tena hata ile ya chuo kikuu ni zero..angalia maneno km aliyoandika huyu..sasa huyu anaweza kuaminiwa kwa jambo lipi ukadhani atafanya vema, kwa kumtathimini kupitia maneno anayotamka tena kwa kiongozi wake wa nchi..wengine atawaheshimu huyu..Asitupangie cha kuogea kwa maana tulivyonunua bando hakuna aliyetusindikiza tulinunua wenyewe, na ata yeye maneno yake ni ya ovyoovyo haijawai kutokea.