Rais Magufuli, awashushua TAKUKURU na Watendaji wote wanajipendekeza kwake na kupeleka miradi ya Maendeleo Chato

Ni kinyago chake hawezi kumhofia hata kidogo.
 
Masikini ni mtu mbaya sana na asie na msimamo ni mchonganishi na mtu wa kujikombakomba masikini ni mtu wa kuogopa mana hawezi kusimamia anachokiamini ni very dynamic na hafai katika jamii, Hemu check watendaji wa Trump ndio utajua kuwa mtu mwenye uhakika na Ugali wa kesho anavyokuwa na msimamo Nitatoa mifano Trump alishindwana na Secretary of State Jim Mattis na Mattis bila purukushani aka resign vilevile ameshindwana na Top security advisor John Bolton na Bolton akakaa pembeni bila kulamba miguu ila pia walishindwa kuelewana na CIA chief James comey akawa fired na Maisha yanaendelea, Rais wetu anafanya mazuri ila kumtukuza kwa kiwango kikubwa ivo ni Ulimbukeni usio na tija yoyote tutekeleza majukumu yetu kwenye nafasi zetu kwa kufata miongozo ya kitaifa sehemu ukiona unapishana sera na kiongozi wako fata order au resign ila utashi pia hauziuwi ndio mana hawa top officials pia ni advisors alichofanya huyo Brigadier General ni aibu kwa kwakweli
 
Bw Mkubwa ni smart sana...kwani hao takukuru wanataka nini huko Chato?.

Wakishaweka makazi huko kinachofuata ni kuichokonoa ile miradi iliyowekezwa kule.
 
Ameshakamata idara zote hana Cha kuhofia...Sasa hivi Taasisi ya Jeshi inapewa makavu live..maana ndio taasisi iliyobaki ambayo alikuwa na woga nayo.
Aendelee tu kuwaaibisha wanajeshi tena mbele ya raia. Nyerere angekuwa hai angemwambia, chezea taasisi zote ila sio JWTZ
 
GENTAMYCINE nami sasa naongezea ( nakazia ) hapo hapo kwa kusema..." Enyi Wakubwa wote ninaowateua katika Nafasi zenu mbalimbali Msijependekeze tu Kwetu Uzanakini Mkoani Mara ( Musoma ) bali naomba sasa mtawanye Maendeleo Tanzania nzima na kwa Kuanzia mnaweza mkaenda Chato Geita pale mkajenga hata Uwanja wa Ndege kwani hawana, na pia kuwepo na Benki kama ya CRDB na kuwa si mbali na Ziwani na kuna Wanyama wengi mnaweza mkaweka na Mbuga ya Wanyama, "

Pelekeni pia Maendeleo huko Kagera kwa Wahaya, Singida kwa Wanyiramba na Warangi, Kigoma kwa Waha, Dodoma kwa Warangi na Mwanza kule Kisiwani Ukerewe kwa Wakara kwani na Wao wanahitaji na wapenda Maendeleo kama haya ' Mnayojipendekeza ' kila Siku kuyaleta hapa mkoani kwangu Mara ( Musoma ) Mimi Rais GENTAMYCINE. Sitaki kila Maendeleo muwe mnayaleta tu hapa Mkoani Mara na mkiendelea na hii tabia ya ' Kujikomba ' Kwangu kuna Siku nitampiga Mtu Ngumi hadharani labda ndiyo mtanielewa.
 
Tatizo lako huekeweki tusipojipendekeza unatutosa tukijipendekeza unatusema hizi tabia za kenge
 
Lack of confidence. Kwanini watu wasisimamie kazi zao kama inavyotakiwa. Mpaka kujipendeleza ndio mambo yaende?
 

Angeanza na waliojenga airport,Bandari,majengo makubwa ya mahakama,tra,nk
 
Nampa kura kwa haya maneno tu....

Ingalikuwa kiongozi siyo mwanajeshi wa cheo cha juu, walaahii angalitumbuliwa siku ileile na saa ileile!! Ila hao watendaji walipo chini ya Chief Executive wote ni wa kutumbua!! Kudos Rais Magufuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…