Nilikuwa nasafiri kutoka Musoma kwenda Dar kwa bus la Osaka, tulivyofika Tinde tulisimamishwa kupisha msafara wa mkubwa uliokuwa ukielekea chato. Basi kuna jamaa akaanza kubwata mara ooh msafara wake una magari mia, mara ooh kwanini asipande helkopta, mara madereva wake wanaendesha kama wehu. Mwoshowe abiria tukachoshwa na kelele za yule bwana tukaamua kushuka kwenye gari na kwenda njiapanda kushuhudia msafara wa mkuu.
Muda si mrefu JPM aliwasili magari yake yalikuwa katika mwendo wa taratibu huku sheria za barabarani zikizingatiwa, msafara wake ulikuwa na magari sita tu tena matatu yakiwa ya polisi watu walishangaa sana. Na kila mtu aliyekuwa pale alimsifu, mamalishe mmoja akawa anasema wamezoea kuona magari ya serikali yakiendeshwa kwa mwendo wa kasi sana lakini msafara huu ndio wakwanza kupita eneo la Tinde ukiwa katika mwendo wa kawaida.
Tulivyorudi kwenye bus abiria walianza kumshambulia yule bwana huku wakimkejeli kwa kumuuliza kahesabu magari mangapi kwenye msafara? yule bwana akaanza kujifaragua ati JPM kaamua kupanda gari la polisi kuokoa pesa watu wakamzomea na kuangua vicheko.