Vijana wa bodaboda tuache mchezo na usalama wa Rais

MMASSY

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
290
193
Leo jioni nikitokea kazini kurejea nyumbani nimeona kituko cha bodaboda mmoja ambaye kimsingi sikuweza kushika kwa haraka plate number za pikipiki yake lakini ilikuwa inaishia na CEA.Wakati magari yote yamesimamishwa kupisha msafara wa Rais kutoka Gran Melia Hotel eneo la Philips,baadhi ya madereva bodaboda wao walikuwa wanawaponyoka polisi waliohangaika kuwazuia bila mafanikio.

Ndio akatokea mmoja wa madereva toyo akautangulia msafara wa Rais huku gari moja Vx, Pt nadhani ya RTO ikajitahidi sana kumkimbizia pembeni ya barabara huku huyo toyo akiendesha kwa madaha bila wasiwasi.Kwa kuwa Pt hiyo ndio ilikuwa ikiongoza msafara(Safisha njia)hawakuweza kumkamata dereva bodaboda huyu ambaye alipaki kwa muda pembeni eneo la Pan African Postoal Union (PAPU) karibia na Mount Meru Hotel.

Nataka kueleza nini kwa kutumia kisa hiki?

1.Usalama wa kiongozi wa nchi uwe ni kipaumbele cha kila mwananchi.Haiwezekani madereva wote wakatii kusimama kuupisha msafara wa kiongozi wa nchi halafu hawa bodaboda wakawa wanaachwa tu kujifanyia wanavyotaka.Polisi wamekuwa pengine kutokana na ugumu wa kuwakamata hawa bodaboda wanaishia kuwaangalia tu bila kuwa na mbinu za kuwadhibiti.Nalisihi jeshi la polisi lisifumbie macho ujinga kama huu.

2.Kuna haja ya Polisi kuja na njia sahihi za kuwakabili bodaboda.Isiishie tu sababu wanaweza kupita kokote bila kukamatwa ikawa ndio wajifanyie kama wanavyoweza.Wakati fulani nilikuwa naendesha pikipiki yangu toka Mbuguni kuelekea moshi kupitia Kia,Trafiki walinisimamisha kunikagua,wakiwa wananiuliza maswali yao zilipita bodaboda kama kumi na kitu madereva hawana helmet wala baadhi ya pikipiki hazina number plates na wamebebana mishikaki haswa.Lakini kwa kuwa walikuwa speed sana hakuna trafiki aliyehangaika nao,walikomaa na mimi niliyekuwa na kila kitu isipokuwa stika ya nenda kwa usalama.Sababu ya kunihukumu mimi ilikuwa mwendo wangu wa taratibu na kutii pale waliponisimamisha.Nilisikitika sana lakini waliishia kunikamua kama kawaida.

3.Baadhi ya maeneo ni muhimu sana kufungwa Camera barabarani ili kudhibiti huu uhuni.Kwa nilichokiona leo pengine polisi hawapaswi kulaumiwa.Lakini msafara wa Rais kuchezewa na bodaboda ni hatari sana.Aliyekuwa anaendesha PT ya mbele kabisa kwenye msafara wa Rais leo atanielewa.Haiwezekani bodaboda anapigiwa honi,anawashiwa taa na kukimbizwa na gari nadhani ya RTO bado akawa anaendesha kwa madaha tena katikati ya barabara halafu tukakaa kimya.Something else must be done kudhibiti hawa wahuni.Baadhi ya nchi jambo kama la leo ni Camera tu unakamatwa kama fuko yule anayekula mazao kule kibosho.

4.Kuna haja ya kuimarisha mafunzo wanayopewa madereva.Naishukuru serikali ilifanikiwa kwa kiasi fulani kidhibiti utoaji holela wa leseni.Lakini hilo halitoshi.Wakati nafundishwa udereva miaka 10 iliyopita sikufundishwa kabisa kuhusu kupisha misafara ya viongozi na athari zake kama sitafanya hivyo.Nilifundishwa kupisha ambulance!!Pengine ndio hali ilivyo kwa hawa bodaboda ambao wengi wao hawaendi hata kusoma udereva.Kuna haja ya kuandaa mafunzo ya kina kwa madereva haswa bodaboda na hawa wa hiace sababu tukiwa kwenye hivi vyombo wakati mwingine unashangaa dereva kaunga na gari za msafara wa kiongozi ili tu awawahi wengine kupakia abiria.Hii si sawa kabisa.

5.Wakati wa kampeni tumekuwa na tabia ya kuwazoesha hawa bodaboda kucheza na misafara ya viongozi wetu.Hii inawafanya waone viongozi ni wa kawaida sana na hawawezi kuadhibiwa pale wanapofanya makosa kama la leo.Fikiria kijana a aendesha pikipiki kwa tairi moja huku amenyanyua tairi moja angani halafu sisi tunashangilia.....Ajabu sana.Wanasiasa lazima wawe mfano bora kutii sheria na kjonekana wakitii sheria.Hapa itasaidia maagizo ya polisi na vyombo vya usalama pia kuheshimika.Kuwaruhusu hawa vijana kujiendeshea tu watakavyo madhara yake yanaweza kuwa makubwa kwetu na viongozi wetu.

6.Kuna umuhimu wa kuwa na ukaguzi wa akili za madereva mara kwa mara.Ukipanda hiace nyingi nyakati za asubuhi utasikia makondakta na madereva wakimlaumu Rais kuondoa wa machinga barabarani.Sababu wanazotoa ni kuwa walikuwa wanapata "gauge" karibu.Yaani madawa ya kulevya na pombe cheap karibu.Wengi wa madereva hawa wanatumia madawa ya kulevya,pombe n.k.Tukio la leo linanifikirisha sana.Jeshi la polisi liweke utaratibu wa kuwapima kiwango cha ulezi madereva wote mara kwa mara na kwa kushtukiza watawakamata wengi sana.

7.Kuna mmomonyoko mkubwa sana wa maadili miongoni mwa jamii.Kuna haja ya taifa kujitafakari upya juu ya aina ya maadili yaliyo katika jamii yetu.Kuanzia kwenye familia,shuleni,makanisani/misikitini na kwenye makundi mengine lazima tuangazie suala hili kwa kina.Tuna rika flani ambalo linaweza kufanya lolote mbele ya yeyote.Ukishaona kijana anauwezo wa kutukana matusi mbele ya wazazi wake,kwenye vyombo vya usafiri,ukiona kijana anavuta bangi barabarani bila hofu,jua hataona shida kabisa kutotii amri ya askari polisi na kuchomoka kuutangulia msafara wa Rais.Upuuzi mtupu.

Natoa rai kwa viongozi wa jeshi la polisi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuongeza umakini hasa kwa hawa wanaoitwa bodaboda.Mimi sio mtaalamu wa masuala ya ulinzi wala sotaki kuwaingilia katika kazi yenu lakini ninachokiona huko barabarani haswa leo ni hatari kwa usalama wa misafara ya viongozi wetu.Hawa jamaa wakiachwa kuna siku watatuletea hasara kubwa.

Kama kijana mmoja anaweza kuwachomoka polisi ambao wako busy kulinda usalama na akatamba katikati ya barabara huku akiona kabisa gari za msafara wa kiongozi mkuu wa nchi zinakuja eneo ambako ameshaona kuna viongozi wa vyombo vya ulinzi pia kama IGP,CDF,RTO,RPC na amiri jeshi mkuu ni dharau na lazima tujitafakari kama wazalendo wa nchi hii.

Jerome Mmassy

Arusha
 
Wanakatazwa kuingia city center kwa upuuzi kama huo hawajali cha mataa wala zebra closing sijui huwa wanawahi wapi hao jamaa na akiri zao hazina utulivu kabisa yaani boda ukipanda na kufika salama unakoenda kwa kweli unashukuru mungu kwa rafu zao yaani jamaa ni hovyo sana.
 
RSO wa dar anapaswa kuwajibika, wasiojulikana aka raia wema walipaswa wadeal nae mapema tu
 
Boda boda wa Arusha walishashindikana siku nyingi,ugoro wenyewe wauita geji, gongo wana jina lao jipya, mirungi, na mabange. Utawaambia nini? Huko central wameshapazoea wanaita ndo Nyumbani
 
Watakuwa na nidhamu nakuwaheshimu mkiacha kuwatumia nyakati za kampeni.
Hivyo kiburi mmewapa wenyewe.
 
Ni kweli kiongozi ye yote na hasa Rais lazima apewe ulinzi wa kutosha kabisa usio na mjadala; na pia aheshimiwe. Lakini hapo matatizo ni mawili. La kwanza, hapo ulipokuwa umesimama au karibu yako kulitakiwa kuwe na mtu wa usalama ambaye ndiye angechukua hatua ya kudhibiti au kuchukua namba za watovu wa nidhamu kama hao na kuwachukulia hatua stahiki.

La pili, shuruti ya boda boda kutii sheria za traffic barabarani pamoja na kuhakikisha waendesha boda boda wana leseni ni muhimu mno si kwa ajili ya usalama wa viongozi tu ila kwa ajili ya usalama wa wananchi wote na hao watalii tunaotaka waje Tanzania.

Kwa hakika polisi wangeweka siku maalum za kushughulikia wavunja sheria na kujiandaa kuwashika wanaokimbia ili boda boda waache hii tabia na wasizoee.

Hii ndiyo ingekuwa sababu ambayo ingeungwa mkono na kila mwenye akili ya wastani kuwa kama boda boda hawataki kufuata sheria hawataruhusiwa kuingia katikati ya miji.

Vinginevyo boda boda wanapita kwenye taa nyekundu, hawasimami kwenye vivuko vya waendao kwa miguu, wanaendesha boda boda kwenye njia za waendao kwa miguu bila wasi.

Hii ndiyo picha ya utawala bora nchini tunayotoa kwa nchi nyingine kama vile viongozi hawaoni wakisafuri nje ya nchi.

Lakini utakuta hata viongozi wanasifu kazi nzuri ya polisi! Usalama wa maisha na viungo vya binadamu ni muhimu kwa taifa letu na ndilo jukumu la kwanza la serikali inayojitambua.
 
Kufunga kamera zann mie Kama chuma kiliondoka pamoja na ule ulinzi mengine yote kwangu ni mbwembwe tu
 
Watawala kupitia CCM Mpya ndiyo wa kulaumiwa maana waendesha Bodaboda na machinga ndiyo mtaji waliowekeza 2015 na 2020
 
5.Wakati wa kampeni tumekuwa na tabia ya kuwazoesha hawa bodaboda kucheza na misafara ya viongozi wetu.Hii inawafanya waone viongozi ni wa kawaida sana na hawawezi kuadhibiwa pale wanapofanya makosa kama la leo.
Hapa ndio kiini cha tatizo haswaaa!
 
Back
Top Bottom