Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi Burundi kufuatia kifo cha Rais Nkurunziza. Asema alikuwa mpigania amani na kuruhusu demokrasia

Status
Not open for further replies.

Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
5,592
11,831
Hivyo ndivyo alivyoandika Mh Rais JPM akituma salamu za pole kwa serikali ya Burundi juu ya kifo cha Rais Nkurunzinza.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter mh Rais amesema Nimeshtushwa na taarifa za kifo cha Rais wa Burundi, Mhe. Pierre Nkurunziza. Nitamkumbuka kwa uongozi wake imara na juhudi zake za kupigania amani, maendeleo na kuruhusu demokrasia. Kwa niaba ya Serikali na Watanzania nawapa pole familia na Warundi wote. Mungu amweke mahali pema.

Magufuli.JPG

Mh Rais ametoa pole hizo kwa niaba ya watanzania wote.

Apumzike kwa amani, poleni warundi wote Mungu awatie nguvu kwenye kipindi hiki kigumu.

Ahsante mh Rais kwa uugwana wako marehemu hasemwi kwa mabaya.

Pia soma > Breaking News: - Serikali ya Burundi yatangaza kifo cha Rais Pierre Nkurunziza
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom