Shoctopus
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 3,434
- 1,985
Naamini Rais Kikwete angetumia mamlaka yake kukamilisha mchakato wa Katiba mpya kwa misingi ya rasimu ya tume ya Warioba angebaki madarakani hadi leo hii kwasababu zifuatazo:
1. Kwanza angejijengea heshima na upendo mkubwa sana kwa Watanzania kwa kuwaletea Katiba mpya iliyo bora kuliko hii tuliyonayo.
2. Pili kwa kufanya hivyo angestahili kugombea urais chini ya Katiba mpya na angeshinda kutokana na kuwaletea Watanzania Katiba mpya.
Kwahiyo Rais JPM anaweza kufanya kile alichokataa Kikwete katka kipindi hiki kwa kutumia mamlaka aliyonayo kuepusha sintofahamu iliyopo kuelekea November 2020. Afanyeje?
1. Akamilishe mchakato wa Katiba mpya kwa misingi ya rasimu ya tume ya Warioba kwa mamlaka aliyonayo hata ikibidi aahirishe Uchaguzi Mkuu.
2. Apunguze idadi ya wizara na mikoa na wilaya, pamoja ukubwa wa Serikali kubana matumizi na kuongeza ufanisi.
3. Apunguze idadi ya wabunge/majimbo ya uchaguzi kwa madhumuni ya hapo juu.
4. Uchaguzi Mkuu chini ya Katiba mpya na tume HURU ya uchaguzi, ufanyike miaka 2 baada ya November 2020 ili kuimarisha mfumo mpya wa demokrasia nchini na kukabiliana na majanga yaliyoko mbele yetu bila kuingiliana na masuala ya kampeni na vurugu za uchaguzi.
Kwakufanya hivyo JPM atajijengea upendo mkubwa sana na heshima ya Watanzania kwa kuwaletea Katiba mpya.
Miradi mbalimbali ya maendeleo aliyoianzisha atakuwa na muda mzuri wa kuikamilisha kwakuwa ataendelea kubaki madarakani chini ya Katiba mpya na Serikali mpya itakayokidhi viwango vya hapo juu.
Vilevile kwa ufanisi utakaotokana na Katiba mpya, demokrasia na misingi ya haki za binadamu na Utawala Bora uchumi wa nchi na wananchi utaboreshwa, mapato ya Serikali yataongezeka na uwezo wa kuhudumia wananchi utaongezeka.
Hiyo ndiyo njia pekee ninayoiona ya kurudisha umoja, amani, upendo na mshikamano katika nchi yetu ili tukabiliane na majanga yaliyoko mbele yetu. JPM peke yake, hawezi. CCM peke yake haiwezi. Chadema au ACT, CUF, NCCR; Mbowe peke yake au Zitto, Lissu, Maalim Seif na wengine peke yao hawawezi.
Lakini Watanzania kwa ujumla wetu chini ya Katiba mpya na tume HURU ya uchaguzi chini ya Rais John Pombe Joseph Magufuli, akiamua kutumia mamlaka aliyonayo kuepusha sintofahamu inayotukabili kisiasa, kiuchumi, na majanga yaliyoko mbele yetu tunaweza.
Sent using Jamii Forums mobile app