Rais Magufuli asirudie makosa ya Mzee Kikwete; atumie mamlaka yake vizuri abaki madarakani beyond 2025

Shoctopus

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
3,434
1,985
Naamini Rais Kikwete angetumia mamlaka yake kukamilisha mchakato wa Katiba mpya kwa misingi ya rasimu ya tume ya Warioba angebaki madarakani hadi leo hii kwasababu zifuatazo:

1. Kwanza angejijengea heshima na upendo mkubwa sana kwa Watanzania kwa kuwaletea Katiba mpya iliyo bora kuliko hii tuliyonayo.

2. Pili kwa kufanya hivyo angestahili kugombea urais chini ya Katiba mpya na angeshinda kutokana na kuwaletea Watanzania Katiba mpya.

Kwahiyo Rais JPM anaweza kufanya kile alichokataa Kikwete katka kipindi hiki kwa kutumia mamlaka aliyonayo kuepusha sintofahamu iliyopo kuelekea November 2020. Afanyeje?

1. Akamilishe mchakato wa Katiba mpya kwa misingi ya rasimu ya tume ya Warioba kwa mamlaka aliyonayo hata ikibidi aahirishe Uchaguzi Mkuu.

2. Apunguze idadi ya wizara na mikoa na wilaya, pamoja ukubwa wa Serikali kubana matumizi na kuongeza ufanisi.

3. Apunguze idadi ya wabunge/majimbo ya uchaguzi kwa madhumuni ya hapo juu.

4. Uchaguzi Mkuu chini ya Katiba mpya na tume HURU ya uchaguzi, ufanyike miaka 2 baada ya November 2020 ili kuimarisha mfumo mpya wa demokrasia nchini na kukabiliana na majanga yaliyoko mbele yetu bila kuingiliana na masuala ya kampeni na vurugu za uchaguzi.

Kwakufanya hivyo JPM atajijengea upendo mkubwa sana na heshima ya Watanzania kwa kuwaletea Katiba mpya.

Miradi mbalimbali ya maendeleo aliyoianzisha atakuwa na muda mzuri wa kuikamilisha kwakuwa ataendelea kubaki madarakani chini ya Katiba mpya na Serikali mpya itakayokidhi viwango vya hapo juu.

Vilevile kwa ufanisi utakaotokana na Katiba mpya, demokrasia na misingi ya haki za binadamu na Utawala Bora uchumi wa nchi na wananchi utaboreshwa, mapato ya Serikali yataongezeka na uwezo wa kuhudumia wananchi utaongezeka.

Hiyo ndiyo njia pekee ninayoiona ya kurudisha umoja, amani, upendo na mshikamano katika nchi yetu ili tukabiliane na majanga yaliyoko mbele yetu. JPM peke yake, hawezi. CCM peke yake haiwezi. Chadema au ACT, CUF, NCCR; Mbowe peke yake au Zitto, Lissu, Maalim Seif na wengine peke yao hawawezi.

Lakini Watanzania kwa ujumla wetu chini ya Katiba mpya na tume HURU ya uchaguzi chini ya Rais John Pombe Joseph Magufuli, akiamua kutumia mamlaka aliyonayo kuepusha sintofahamu inayotukabili kisiasa, kiuchumi, na majanga yaliyoko mbele yetu tunaweza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli hataki kuwa rais baada ya 2025, kwa mujibu wa maneno yake mwenyewe.

Pia godfather wake Mkapa kasema hataki kuona rais Magufuli anaendelea zaidi ya 2025.

Mnataka kuambiwa nini ili mfute ndoto za Magufuli kuwndelea kuwa rais baada ya 2025?
 
Hivi kwenye kiapo chake hakukuwa na maneno ya " ntailinda na kuiheshimu Katiba ya Jamhuri wa Muungano " ?
 
We jamaa uraisi una kikomo miaka 10 kama haijamtosha basi awaachie wengine. ..gurudumu la maendeleo Ni is watz wote sio flani tu
 
Naunga mkono hoja,maana hiki ni kilio cha wapinzani kwa muda mrefu sana. Inaweza kua kama kwa Paul.

macson
 
Duuh hii kweli dunia ukistaajabu ya musa utaona ya filauni, wakati walio wengi wanatamani aishie miaka mitano tu asiongeze hata sekunde wewe unataka aongeze muda. Watu walishachoka wako hoi biashara haziendi, maisha yamesimama, ugomvi kwenye familia kila siku kwa sababu ya njaa, watu wanajinyonga ovyo wengine wanapotea katika mazingira yasiyoeleweka, bado unahitaji aendelee!
 
Wewe uliyeandika ni mwanaume? Ina maana kati ya raia wote Magufuli ndio kidume pekee wa kuwa Rais?

Unajidharau mdau

_____________________________
" With or without religion, good people can behave well and bad people can do evil; but for good people to do evil - that takes religion.
 
Jamaa anazungumzia katiba mpya na endapo jpm anataka kuingia kwenye kumbukumbu nchini.

issue ya urais itakuwepo kwenye katiba mpya.
We jamaa uraisi una kikomo miaka 10 kama haijamtosha basi awaachie wengine. ..gurudumu la maendeleo Ni is watz wote sio flani tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jpm ameshafanya makosa yake na ni makosa makubwa zaidi kuliko ya kiongozi mwingine aliyetangulia nchi hii.
 
Salaaaleeee athubutu ili ajionee hasira za wananchi wanyonge, yanapowafika shingoni. Maana hapa tu raia hatuna hamu. Acha kumponza Kiongozi wa Malaika.
 
Hujui kuwa wanaongea kinyume na matendo yao?mark my words utaona nink kitatokea
Magufuli hataki kuwa rais baada ya 2025, kwa mujibu wa maneno yake mwenyewe.

Pia godfather wake Mkapa kasema hataki kuona rais Magufuli anaendelea zaidi ya 2025.

Mnataka kuambiwa nini ili mfute ndoto za Magufuli kuwndelea kuwa rais baada ya 2025?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naamini Rais Kikwete angetumia mamlaka yake kukamilisha mchakato wa Katiba mpya kwa misingi ya rasimu ya tume ya Warioba angebaki madarakani hadi leo hii kwasababu zifuatazo:

1. Kwanza angejijengea heshima na upendo mkubwa sana kwa Watanzania kwa kuwaletea Katiba mpya iliyo bora kuliko hii tuliyonayo.

2. Pili kwa kufanya hivyo angestahili kugombea urais chini ya Katiba mpya na angeshinda kutokana na kuwaletea Watanzania Katiba mpya.

Kwahiyo Rais JPM anaweza kufanya kile alichokataa Kikwete katka kipindi hiki kwa kutumia mamlaka aliyonayo kuepusha sintofahamu iliyopo kuelekea November 2020. Afanyeje?

1. Akamilishe mchakato wa Katiba mpya kwa misingi ya rasimu ya tume ya Warioba kwa mamlaka aliyonayo hata ikibidi aahirishe Uchaguzi Mkuu.

2. Apunguze idadi ya wizara na mikoa na wilaya, pamoja ukubwa wa Serikali kubana matumizi na kuongeza ufanisi.

3. Apunguze idadi ya wabunge/majimbo ya uchaguzi kwa madhumuni ya hapo juu.

4. Uchaguzi Mkuu chini ya Katiba mpya na tume HURU ya uchaguzi, ufanyike miaka 2 baada ya November 2020 ili kuimarisha mfumo mpya wa demokrasia nchini na kukabiliana na majanga yaliyoko mbele yetu bila kuingiliana na masuala ya kampeni na vurugu za uchaguzi.

Kwakufanya hivyo JPM atajijengea upendo mkubwa sana na heshima ya Watanzania kwa kuwaletea Katiba mpya.

Miradi mbalimbali ya maendeleo aliyoianzisha atakuwa na muda mzuri wa kuikamilisha kwakuwa ataendelea kubaki madarakani chini ya Katiba mpya na Serikali mpya itakayokidhi viwango vya hapo juu.

Vilevile kwa ufanisi utakaotokana na Katiba mpya, demokrasia na misingi ya haki za binadamu na Utawala Bora uchumi wa nchi na wananchi utaboreshwa, mapato ya Serikali yataongezeka na uwezo wa kuhudumia wananchi utaongezeka.

Hiyo ndiyo njia pekee ninayoiona ya kurudisha umoja, amani, upendo na mshikamano katika nchi yetu ili tukabiliane na majanga yaliyoko mbele yetu. JPM peke yake, hawezi. CCM peke yake haiwezi. Chadema au ACT, CUF, NCCR; Mbowe peke yake au Zitto, Lissu, Maalim Seif na wengine peke yao hawawezi.

Lakini Watanzania kwa ujumla wetu chini ya Katiba mpya na tume HURU ya uchaguzi chini ya Rais John Pombe Joseph Magufuli, akiamua kutumia mamlaka aliyonayo kuepusha sintofahamu inayotukabili kisiasa, kiuchumi, na majanga yaliyoko mbele yetu tunaweza.

Sent using Jamii Forums mobile app
..... na hiyo ndiyo njia pekee ya yeye kujinusuru ku-Gaddafiwa na "beberus" October 2020!
 
Duuh hii kweli dunia ukistaajabu ya musa utaona ya filauni, wakati walio wengi wanatamani aishie miaka mitano tu asiongeze hata sekunde wewe unataka aongeze muda. Watu walishachoka wako hoi biashara haziendi, maisha yamesimama, ugomvi kwenye familia kila siku kwa sababu ya njaa, watu wanajinyonga ovyo wengine wanapotea katika mazingira yasiyoeleweka, bado unahitaji aendelee!
Sasa JPM hayupo kama mlivyotaka. Lakini kuna aheri gani? Mrithi wake ameshasema JPM na yeye ni kitu kimoja!

Si bora JPM angeleta Katiba mpya? Tatizo lenu hamufikirii ya kesho.
 
Back
Top Bottom