Rais Magufuli aongeza muda kwa usajili wa laini kwa alama za vidole


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Subirini vituko siku yakuzimwa..zitazimwa hata zilizosajiliwa....subirini

hilo liko wazi ndugu ukitaka kujua ukweli, tafuta card ya voda iliyokwishasajiliwa mpigie mwenye namba ya voda inaanza sauti kuwa 'laini yako haijasajiliwa kwa alama ya vidole kama inavyotakiwa kisheria.....'

niliudhika nikawapigia eti najibiwa samahani hiyo sauti imewekwa kimakosa lkn baadae wataitoa. nikamuuliza dada pamoja na wasomi wa it mlionao wameshindwa kuweka mfumo thabiti wa kutifautisha cards zenye usaili na zisizosajiliwa iki kutuondolea kero ya kusubiri dk nzima kupisha tangazo lenu? alibaki kuuma midomo.

nahisi site tutapigea pini watuambie tena tukaunge foleni maduka yao awamu hii tukiwa na kitambulisho na barua ya kiapo cha mahakama. huwa najisemea tu, teknolojia inatukimbiza tofauti ma mwendo wa gari letu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 27 Desemba, 2019 amefanya usajili wa laini yake ya simu kwa kutumia alama za vidole na kuwasisitiza Watanzania wote wahakikishe laini zao za simu zinasajili kwa alamu za vidole kama ilivyoelekezwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Mhe. Rais Magufuli amefanya usajili huo Chato Mjini katika Mkoa wa Geita.

Hata hivyo, Mhe. Rais Magufuli ameongeza siku 20 kuanzia tarehe 01 Januari, 2020 hadi tarehe 20 Januari, 2020 kwa wote ambao watashindwa kusajili laini zao katika kipindi cha kuishia tarehe 31 Desemba, 2019 kama ilivyotangazwa na TCRA kutokana sababu mbalimbali zikiwemo kuugua na kukamilisha upataji wa namba ama Vitambulisho vya Taifa. Mhe. Rais Magufuli amesisitiza kuwa baada ya muda huo hakuna kisingizio chochote kitakachokubalika na ameagiza TCRA kuhakikisha laini ambazo hazijasajiliwa zinazimwa.

Amefafanua kuwa usajili wa laini za simu kwa alama za vidole ni muhimu kwa usalama wa nchi ikiwemo kuepusha vitendo vya utapeli na ujambazi vinavyofanywa na wahalifu, ambao licha ya wengi wao kukamatwa na vyombo vya dola wameendelea kusababisha usumbufu na upotevu mali za wananchi hususani fedha.

Pamoja na kuwasalimu wananchi wa Chato Mjini waliojitokeza kushuhudia wakati akisajili laini yake kwa alama za vidole, Mhe. Rais Magufuli amewasalimu na kusikiliza maoni yao kuhusu zoezi hili na pia mwananchi Steven Joseph Wandwi anayefanya biashara ya kuuza chipsi na mishikaki akawaongoza wenzake kumuombea Mhe. Rais Magufuli na kumshukuru kwa utumishi wake mzuri ulioongeza kasi ya maendeleo kwa Taifa hasa vijana ambao sasa wanachapa kazi bila bughudha.

Kabla ya kwenda kusajili laini yake ya simu, Mhe. Rais Magufuli ametembelea Mtaa wa Chato Kati na ametoa pole kwa familia ya Marehemu Atanasi Masansa Mnaku aliyefariki dunia juzi tarehe 25 Desemba, 2019 na mazishi yake yamepangwa kufanyika kesho.

View attachment 1304650

View attachment 1304651

View attachment 1304652

View attachment 1304653
Tuko kwenye lait traki kuelekea uchumi wa katikati

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuongeza siku bila kulikabili na kutatua tatizo la msingi ni kujidanganya. Hapa tatizo kubwa ni vitambulisho vya taifa. Inashangaza kuwa suluhu ilikuwa 'NIDA wapeni namba za vitambulisho wanaoomba vitambulisho vya taifa'! Hii ilikuwa ni suluhu ya ajabu...ikiwa mtu umemsajili na kumpa namba kwa nini husimpe kitambulisho chake? Hata suluhu hiyo ya nama nayo imeshindwa kutatua tatizo kikamilifu! Hakuna anayetuambia ni kwa nini NIDA wanashindwa kutoa vitambulisho? Hii inaathiri hata wanaotaka huduma zingine kama vile maombi ya passport. Bado tuna kumbukumbu za huko nyuma tulipoaminishwa kuwa watendaji wakuu waliokuwepo hawakuwa mafisadi tu bali ndio walisababishwa watanzania wote kukosa vitambulisho- na mfano mzuri ulikuwa tume ya taifa na vitambulisho vya mpiga kura! Je kumetokea nini sasa tofauti na huko nyuma?

Tunaambiwa hata RITA nao wanatoa vyeti vya kuzaliwa kwa kuandika kwa mkono. Waxiri mhusika anatuaminisha hii ni sawa na kuwataka wanahitaji hati hizo kwa shughuli zingine wazikubali kuwa ni sahihi!
Nchi ya viwonders hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom