Rais Magufuli anahoji; Je, ninyi hamuamini kuwa yupo Mungu?

mtoto wa mchungaji

JF-Expert Member
Oct 24, 2020
279
480
Mhe. Rais naona ameumaliza mzizi wa fitina leo katika mazishi ya Balozi Kijazi na kusema kuwa magonjwa yalikuwepo, yapo na yataendelea kuwepo, na sisi si pekee ndiyo tunaotaabika na matatizo haya ya magonjwa ya milipuko hata nchi zingine wamekufa wengi sana. Na tatizo linapokuwa kubwa kuzidi uwezo wa binadamu tulisogeze kwa Mungu.

Rais anasema mwaka jana tulimuona Mungu akitusaidia lakini sasa naona wengine hawana imani tena wanatengeneza taharuki na kutishana mimi sifanyi lokudauni tuchape kazi Mungu yupo. Kwanini au amwamini kuwa Mungu anaweza kuishinda Korona?

Mimi mtoto wa mchungaji nahoji hivi hawa baadhi ya viongozi wa dini ambao nao pia wanaogopa Corona kiasi cha kwamba wanatushauri tuwasikilize watu wa afya na wamitandaoni hivyi hawa watumishi wa Mungu si wangeacha hiyo kazi na kuja huku mchangani ijulikane moja.

Nawauliza na ninyi wana janvi Mungu yupo au, maana babuzetu waliomba mvua zilinyesha, waliomba nzige waondoke asubui waliwakuta chali kificha mende, magonjwa ya mlipuko hayakuwagusa, hivi na yule Mungu wa babu zetu yupo wapi siku hizi na huyu wa kanisani na msikitini yupo wapi.
 
Nafurahi sana napomuona Rais wangu akiijua sana dini kuliko watu wote duniani (ukimtoa Askofu Rasheed) Jinsi anavyomjua sana Mungu kuliko hata Watumishi wa Mungu! Jinsi anavyomjua sana Mungu kuliko wale waliotuletea habari za Mungu! Yaani Rais wangu mpendwa anamjua sana Mungu kuliko hata Bible inayosema "Imeandikwa pia, usimjaribu Mungu wako"!

Hivi anamuona Bwana Yesu ni zuzu aliyemgomea shetani kujitupa chini kutoka juu ya mnara, au Rais wangu anafikiria nini hasa? Mbona Yesu hakujitupa pamoja na bible kusema Mungu atawaamuru malaika wake watamchukua mikononi mwao ili asijikwae?
 
AMWAMINI MUNGU....
Kamwe huyu Mungu tunayemwabudu Wakristo Mungu wa Abraham, Izaka na Yakobo siye Mungu anayemwabudu Magufuli.

Kwa matendo aliyowatendea wenye vyeti feki, aliowatumbua kazini, aliowapeleka Segerea, aliowaua kwa kikundi cha WASIOJULIKANA, anaowanyima nyongeza za mishahara, anaowabomolea nyumba Kimara kamwe hawezi kuomba Mungu akamsikiliza. Kwa namna anavyoacha watu wasichukue tahadhari kwenye Corona, huyu hawezi kuwa anamuamini Mungu.

Labda mungu (m- ndogo) wa Gwajiboy, Mch Mashimo na Sheikh Alhad wa Dar ambao anaomba nao kila mara
 
Wenye akili km zako hawapaswi kuwa JF kwa hakika. Inasikitisha kuona wapo watu humu wenye akili finyu za kusubiri rais aseme ndio ajue tatizo lipo au la na achukue hatua. Idiot!

Corona si tatizo la kumwita Mungu, ni tatizo la kupambana nalo kwa maarifa aliyotupa Mungu. Kimsingi Magu anashindwa kumeza maneno yake ya kujigamba, hawezi. Lakini cha ajabu hata sisi hatutaki kujikinga tunasubiri et rais aseme "chukueni tahadhari". Ujinga.

Ebola haikutoka kwa maombi, polio, surua, ndui n.k havikuisha kwa maombi. Jiue kwa ujinga wako km hao wapuuzi wanaoendelea kukusanyika misibani bila kuvaa hata barakoa.
 
Kamwe huyu Mungu tunayemwabudu Wakristo Mungu wa Abraham, Izaka na Yakobo siye Mungu anayemwabudu Magufuli.

Kwa matendo aliyowatendea wenye vyeti feki, aliowatumbua kazini, aliowapeleka Segerea, aliowaua kwa kikundi cha WASIOJULIKANA, anaowanyima nyongeza za mishahara, anaowabomolea nyumba Kimara kamwe hawezi kuomba Mungu akamsikiliza. Kwa namna anavyoacha watu wasichukue tahadhari kwenye Corona, huyu hawezi kuwa anamuamini Mungu.

Labda mungu (m- ndogo) wa Gwajiboy, Mch Mashimo na Sheikh Alhad wa Dar ambao anaomba nao kila mara
Eti kamwe, Mungu mwenyewe ndiye anayemjua, wewe ni worthless individual unayebweka tu. Unadhani kuwa kiongozi wa nchi Mungu hahusiki. Nyumbu bhana
 
Maneno mazuri ya kutia moyo, tuendelee kumtumainia Mungu kwa hili hakika tutashinda.
 
Back
Top Bottom