Rais Magufuli amtishia mtoto wa dada’ke

Rais Magufuli amtishia mtoto wa dada’ke

Nasikia na yule bosi wa Muhimbili ni binamu yake,Emmanuel Buhohela pia nduguye
Buhohela atakuwaje ndugu yake wakati mi muha wa kigoma? Wapo ndugu zake tuliamini watapenya kwenye uteuzi. Mtu ana Masters, na ni ndugu hasa lkn amebaki kuwa katibu walimu wilaya moja hivi. Tulitarajia ataupata ukurugenzi, hakupata. Tukasubiri kwenye u dc hakupata, u ras n.k ye yupo na ukatibu wilaya
 
Magufuli anashangaza mno

mamlaka ya kupeleka umeme hapo kiwandani hayapo kwa huyo meneja wa Pwani Tanesco

kiwanda cha Bakhresa kinahitahi megawat 10
sawa na mahitaji ya mkoa mzima wa Dodoma....

sio investment ndogo

maamuzi yako Tanesco headoffice na wizarani

alipaswa kumtishia waziri wake na sio huyo
Anaye tolea taarifa ni nani?
 
Huyo Jamaa ni kimeo tu utadhani kwereakwereae wa kwadelo na Mrijo.

Wewe mtu unaskia alikuwa Tanga na Musoma bado unaona kapendelewa. Magufuli anamiaka mingapi ya urais?

Piga kazi acha majungu
Na vindege vya KELEMA mkuu.
 
Mbona huyo alikuwa Kagera na Tanga kama Meneja kabla ya JPM hajachukua nchi.Tusibwabwaje sana na tuache kufikiria hasi.
 
Rais John Magufuli amempa miezi miwili mtoto wa dada yake, ambaye ni Meneja wa Shirika la Umeme (Tanesco) mkoa wa Pwani, Mhandisi Martin Madulu, kuhakikisha umeme unafika kwenye kiwanda cha kusindika matunda cha kampuni ya Bakhresa kilichomo ndani ya mkoa wake, vinginevyo atamtumbua.

Rais alitoa agizo hilo wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho kilichopo Vikindu wilayani Mkuranga mkoani humo, agizo ambalo limekumbusha jinsi alivyomtumbua aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga aliyekuwa anadaiwa kuwa rafiki yake wa karibu.

Uteuzi wa Kitwanga kwenye Baraza la Mawaziri ulitenguliwa na Magufuli Mei 20, mwaka huu baada ya Mbunge huyo wa Misungwi (CCM) kuingia bungeni akiwa amelewa na kujibu swali lililoelekezwa kwenye wizara yake.

Na katika uzinduzi wa kiwanda hicho jana, Rais ambaye alikuwa mgeni rasmi, alilazimika kutoa agizo hilo kwa mpwa wake mara tu baada ya kuelezwa na mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo, Aboubakar Bakhresa, kuwa wanalazimika kutumia jenereta kukiendesha kutokana na kutokuwapo kwa nishati ya umeme wa Tanesco.

Aboubakar alimweleza Rais kuwa upatikanaji wa umeme bado ni changamoto katika kiwanda hicho na kwamba wanahitaji umeme wa megawati 10 ili kukiendesha.

“Meneja wa Tanesco mkoa wa Pwani, wewe Madulu, tena ni mtoto wa dada yangu, nitakutumbua wewe!" Alisema Rais Magufuli na kufanya umati uliohudhuria halfa hiyo uangue kicheko.

"Ulifanya kazi nzuri ulipokuwa Kagera na Tanga, sasa fanya kazi na hapa. "Nataka ndani ya miezi miwili umeme uwe umefika hapa, mimi huwa sibembelezi mtu, mkono wangu ni mwepesi sana kutumbua.”

Rais Magufuli alimtaka meneja huyo kushirikiana na meneja wa Tanesco wilaya ya Mkuranga, Dar es Salaam na Pwani kuhakikisha umeme unafika kwa haraka katika kiwanda hicho.

Alisema ni jambo la kushangaza kwa Tanesco kutopeleka umeme katika kiwanda hicho wakati nia ya serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya viwanda.

Rais alisema ni jambo ambalo haliingii akilini tangu upimaji wa kiwanja ulipoanza hadi kiwanda kinajengwa na kukamilika, umeme haujafika katika kiwanda hicho wakati makao makuu ya Tanesco yako kilomita chache kutoka kilipo.

Alisema kutokana na kiwanda kutumia jenereta kujiendesha, gharama za uzalishaji zinakua juu, hali itakayosababisha hata wafanyakazi kulipwa mishahara midogo.

“Leo (jana) ni Oktoba 6, kabla ya mwezi wa 12 (Desemba), nataka umeme uwe umefika hapa," alisema Rais Magufuli. "Tena ninatamka kwa dhati kutoka moyoni mwangu; kama mnataka kazi, basi umeme uwe umeshafika hapa. Nyie Tanesco ni watu wa ajabu sana, sijawahi kuona... ila Madulu fanya kazi usiogope sikutumbui leo,” alisema Magufuli na kufanya umati uangue kicheko kwa mara nyingine.

Alisema Tanesco inapaswa kujipanga kwa kuangalia maeneo ya kipaumbele ya kupata umeme na "ikiwezekana wasipeleke umeme katika magereza ya wafungwa, lakini uzalishaji viwandani ni lazima umeme upewe kipaumbele".
Source:Nipashe.

MDOGO.JPG
​
Issue ya kitwanga ni planned, mwenye akili yoyote anajua
 
Mimi siwaelewi baadhi ya Watz, hivi mtu akiwa kiongozi wa ngazi za juu Serikalini, ndugu zake hawatakiwi kuajiriwa au kishika nyadhifa Serikalini hata kama wana sifa zinazohitajika?
Naomba mnisaidie, sura/ibara gani ya Katiba au Sheria inayozuia ndugu wa kiongozi fulani kushika nyadhifa Serikalini.
Hicho kifungu hakuna mkuu.
Aliyesema tribalism alikua mbali na mazingira halisi..mazingira halisi yangeweza kuwa nepotism...lakini ikiwa imethibitika hivyo....
 
Mkuu mrangi wewe ni mtu wa heshima hapa jamvini. Ngoja nikuambia yangu. Kama baba yangu angelichaguliwa kuwa rais wa Tanzania basi watu wasiofikiria nje ya box wangekufa kwa kiroho cha kusema anapendelea ndugu zake. Kwanini? Uzao wetu tuko watoto 16 (wake na vimada) na wote tumesoma na watano wako kwenye position za juu serikalini. This means kwamba watu wasingeweza kuona kama kila mtu kafika pale kwa juhudi zake bali wangesema wamebebwa na baba yao ambaye ni rais!
Kweli kabisa
 
Mkuu, nadhani utapoteza muda wako kujaribu kujenga hoja na baadhi ya watu ambao kwao ujinga umekuwa he.kima na busara.

Kuna wengine hawafahamu kama ni wajinga na kwa mantiki hiyo hawawezi kujifunza.
Ubarikiwe sana
 
Tulitangulia kusema mapema... mabadiliko yanayotakiwa katika nchi hii ni ya mfumo. Mtaendele kuyaona wenyewe. JPM anachapa kazi sana. Lakini yeye na uchapa kazi wake anabaki kuwa yeye tu. Tanesco ni ile ile, Utendaji wa Wizara na taasisi zake ni ule ule. Ugoigoi, urasimu na "akili matope" ya watendaji wengi wa serikali ni ile ile....
 
Tena ndugu ndo wanaongoza kwa kukwamisha kazi huna budi kuwa kauzu tu!
 
Magufuli anashangaza mno

mamlaka ya kupeleka umeme hapo kiwandani hayapo kwa huyo meneja wa Pwani Tanesco

kiwanda cha Bakhresa kinahitahi megawat 10
sawa na mahitaji ya mkoa mzima wa Dodoma....

sio investment ndogo

maamuzi yako Tanesco headoffice na wizarani

alipaswa kumtishia waziri wake na sio huyo

Uko sahihi. huu ni umeme mwingi ambao TANESCO hawawezi kuuongeza kwenye grid ndani ya miezi 2. Pamoja na tatizo la kifedha bado huo umeme hauwezi kuzalishwa ndani ya kipindi kifupi hivo hata kama pesa zote zipo.
 
Back
Top Bottom