Rais Magufuli amtishia mtoto wa dada’ke

Rais Magufuli amtishia mtoto wa dada’ke

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,185
Reaction score
24,055
Rais John Magufuli amempa miezi miwili mtoto wa dada yake, ambaye ni Meneja wa Shirika la Umeme (TANESCO) mkoa wa Pwani, Mhandisi Martin Madulu, kuhakikisha umeme unafika kwenye kiwanda cha kusindika matunda cha kampuni ya Bakhresa kilichomo ndani ya mkoa wake, vinginevyo atamtumbua.

Rais alitoa agizo hilo wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho kilichopo Vikindu wilayani Mkuranga mkoani humo, agizo ambalo limekumbusha jinsi alivyomtumbua aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga aliyekuwa anadaiwa kuwa rafiki yake wa karibu.

Uteuzi wa Kitwanga kwenye Baraza la Mawaziri ulitenguliwa na Magufuli Mei 20, mwaka huu baada ya Mbunge huyo wa Misungwi (CCM) kuingia bungeni akiwa amelewa na kujibu swali lililoelekezwa kwenye wizara yake.

Na katika uzinduzi wa kiwanda hicho jana, Rais ambaye alikuwa mgeni rasmi, alilazimika kutoa agizo hilo kwa mpwa wake mara tu baada ya kuelezwa na mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo, Aboubakar Bakhresa, kuwa wanalazimika kutumia jenereta kukiendesha kutokana na kutokuwapo kwa nishati ya umeme wa TANESCO.

Aboubakar alimweleza Rais kuwa upatikanaji wa umeme bado ni changamoto katika kiwanda hicho na kwamba wanahitaji umeme wa megawati 10 ili kukiendesha.

“Meneja wa TANESCO mkoa wa Pwani, wewe Madulu, tena ni mtoto wa dada yangu, nitakutumbua wewe!" Alisema Rais Magufuli na kufanya umati uliohudhuria halfa hiyo uangue kicheko.

"Ulifanya kazi nzuri ulipokuwa Kagera na Tanga, sasa fanya kazi na hapa. "Nataka ndani ya miezi miwili umeme uwe umefika hapa, mimi huwa sibembelezi mtu, mkono wangu ni mwepesi sana kutumbua.”

Rais Magufuli alimtaka meneja huyo kushirikiana na meneja wa TANESCO wilaya ya Mkuranga, Dar es Salaam na Pwani kuhakikisha umeme unafika kwa haraka katika kiwanda hicho.

Alisema ni jambo la kushangaza kwa TANESCO kutopeleka umeme katika kiwanda hicho wakati nia ya serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya viwanda.

Rais alisema ni jambo ambalo haliingii akilini tangu upimaji wa kiwanja ulipoanza hadi kiwanda kinajengwa na kukamilika, umeme haujafika katika kiwanda hicho wakati makao makuu ya TANESCO yako kilomita chache kutoka kilipo.

Alisema kutokana na kiwanda kutumia jenereta kujiendesha, gharama za uzalishaji zinakua juu, hali itakayosababisha hata wafanyakazi kulipwa mishahara midogo.

“Leo (jana) ni Oktoba 6, kabla ya mwezi wa 12 (Desemba), nataka umeme uwe umefika hapa," alisema Rais Magufuli. "Tena ninatamka kwa dhati kutoka moyoni mwangu; kama mnataka kazi, basi umeme uwe umeshafika hapa. Nyie TANESCO ni watu wa ajabu sana, sijawahi kuona... ila Madulu fanya kazi usiogope sikutumbui leo,” alisema Magufuli na kufanya umati uangue kicheko kwa mara nyingine.

Alisema TANESCO inapaswa kujipanga kwa kuangalia maeneo ya kipaumbele ya kupata umeme na "ikiwezekana wasipeleke umeme katika magereza ya wafungwa, lakini uzalishaji viwandani ni lazima umeme upewe kipaumbele".
Source:Nipashe.

MDOGO.JPG

Martin Madulu akisubiri kutumbuliwa na Rais Magufuli
​
 
Magufuli anashangaza mno

mamlaka ya kupeleka umeme hapo kiwandani hayapo kwa huyo meneja wa Pwani Tanesco

kiwanda cha Bakhresa kinahitahi megawat 10
sawa na mahitaji ya mkoa mzima wa Dodoma....

sio investment ndogo

maamuzi yako Tanesco headoffice na wizarani

alipaswa kumtishia waziri wake na sio huyo
 
Mambo mengine utani akimtumbua anampangia kazi nyingine. Anko ataenda kwa bibi then bibi atamwita mjukuu kwa utani Mme wangu madullu umekuja na hela yangu ya ugoro. Akijiliza tyuuu lazima anko aitwe chato aambiwe neno. Mjomba anauma nyie acheni utani nyie.
Utani wa Sagai kwa leo huo
 
Magufuli anashangaza mno

mamlaka ya kupeleka umeme hapo kiwandani hayapo kwa huyo meneja wa Pwani Tanesco

kiwanda cha Bakhresa kinahitahi megawat 10
sawa na mahitaji ya mkoa mzima wa Dodoma....

sio investment ndogo

maamuzi yako Tanesco headoffice na wizarani

alipaswa kumtishia waziri wake na sio huyo
Ni namna ya kutafuta kumtumbua waziri husika
 
KUMBE WAKO KILA KONA MAGU CLAN...

OVA
Mkuu mrangi wewe ni mtu wa heshima hapa jamvini. Ngoja nikuambia yangu. Kama baba yangu angelichaguliwa kuwa rais wa Tanzania basi watu wasiofikiria nje ya box wangekufa kwa kiroho cha kusema anapendelea ndugu zake. Kwanini? Uzao wetu tuko watoto 16 (wake na vimada) na wote tumesoma na watano wako kwenye position za juu serikalini. This means kwamba watu wasingeweza kuona kama kila mtu kafika pale kwa juhudi zake bali wangesema wamebebwa na baba yao ambaye ni rais!
 
Namkumbuka dingi alikuwa anaupenda sana wimbo wa Ndala Kasheba.

Mawazo yamenijia leo aliokuwa mzee wangu akisema dunia msongamano wa watu wenye akili tofauti. Ukitaka kuish vyema fikiri kabla ya kujib (kaul za kukurupuka). Jifunze kwa walimwengu walimwengu wajifunze kwako dunia nikuona mambo halafu kuyasahau.

Mateso nimeshayapata matatizo mengi yamenikuta furaha nyingi nimeshaona maisha nusu nimeshafanya naelezea usemi sasa lazima niwe na utuliv sababu kuishi kwingi nikuona mengi kuelimisha wanaobaki waish kwa heshima.

Huyo chunusi huyoo

Dunia msongamano asema baba nimeona leo nakubali mie. Wengine upendelea kufurahia wanaposikia fulani kaafaaa hoo (rejea Lowasa alivyotukanwa). Kufa kwa binadam upangwa na Mungu namuomba mwenyezi anipe maisha hoo
 
Back
Top Bottom