Rais Magufuli alaani kitendo cha watu wanaosadikiwa kuwa ni majangili kumuua Rubani Roger Gower

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,720
55,844
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelaani kitendo cha watu wanaosadikiwa kuwa ni majangili kumuua kwa kumpiga risasi Rubani wa helkopta Kepteni Roger Gower, raia wa Uingereza na kisha kuidondosha helkopta aliyokuwa akiiendesha wakati alipoungana na Askari wanyamapori waliokuwa wakikabiliana na majangili katika pori la akiba lililopo katika wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu.

Rais Magufuli ameelezea kusikitishwa sana na tukio hilo na ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha waliomuua Kepteni Gower na kuidondosha helkopta aliyokuwa akiiendesha wanakamatwa na wanafikishwa mikononi mwa vyombo vya sheria.

Amemtumia salamu za pole, Balozi wa Uingereza hapa nchini kwa kumpoteza raia wake ambaye alikuwa akitoa mchango mkubwa katika kuhifadhi wanyamapori wa hapa nchini Tanzania.

Aidha, Rais Magufuli amesema serikali yake itahakikisha inaendeleza mapambano dhidi ya ujangili kwa nguvu zake zote na kuwataka wananchi na wadau mbalimbali wa hifadhi ya wanyamapori, kutokatishwa tamaa na tukio hili na watoe ushirikiano wa kutosha kuwafichua watu wote wanaojihusisha na ujangili ama biashara ya bidhaa zitokanazo na ujangili.

Katika tukio hilo, pamoja na kumuua Kepteni Roger Gower watu hao wanaosadikiwa kuwa majangili wamemjeruhi Askari wanyama pori mmoja na wamewaua tembo watatu.

Gerson Msigwa.

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.

Dar es salaam

31 Januari, 2016
 
Tutaona rangi halisi ya Ngosha. The dentist kapotea,simsikii tena. R.I.P kamanda uliyeuawa kazini
 
Ndiyo, baadhi ya majangili yameshakamatwa kutokana na habari ya hapo chini ya BBC chipolopolo 2


Tanzanian police have arrested three suspects over the death of a UK pilot working for a conservation fund whose helicopter was shot down by poachers.
Natural Resources and Tourism Minister Jumanne Maghembe told AFP news agency that those detained were co-operating.
"Soon more people making up the poaching gang will be netted and brought to justice," he said.
Roger Gower, 37, had been flying near an elephant killed by poachers when his helicopter came under fire.
The incident happened in Maswa Game Reserve, which borders the Serengeti National Park in northern Tanzania.
Mr Gower managed to land his helicopter, but died before he could be rescued, a Tanzanian MP and former minister for natural resources and tourism, Lazaro Nyalandu, said in a tweet.
A spokesman for Tanzania's national parks, Pascal Shelutete, said three elephant carcasses had been found in the area, indicating "that whoever shot the chopper down was on a serious illegal hunting spree".
He said such poachers can be "heavily armed with sophisticated military weaponry".
Mr Gower was originally from Birmingham and worked in London before moving to East Africa to work as a helicopter pilot.
His brother Max told the BBC: "He would not have gone anywhere near those poachers if he'd known that they were armed.
"As I understand it, he knew they were around but came across them by accident. He didn't really have enough time to evaluate the situation before they opened fire on him."
Fun-loving man
Max Gower also said his brother would be remembered as "very much his own man".
"He had a very strong moral compass. He just loved having fun, he couldn't be with his friends without making sure that everybody had fun."
The Gower family have invited donations to a fund established in Roger's memory that will contribute towards anti-poaching efforts in Tanzania.
The Friedkin Conservation Fund, for which Mr Gower had been working, said the organisation had lost "a dear friend".
The charity's founder, Dan Friedkin, said: "We believe that Roger can best be honoured by redoubling our commitment to protect elephants and our priceless wildlife heritage.
"This tragic event again highlights the appalling risk and cost of protecting Tanzania's wildlife."
The Friedkin Fund says elephant poaching is "especially prevalent" in Maswa, with rangers encountering ivory poachers "on a fairly regular basis".
 
Muingereza ataingilia kati kuwatumbua hawa majangili. Kuua raia wake si mchezo; Sisi, tumeshindwa hii vita.
 
16c20590395c30d41facaf418922e374.jpg
 
Mmmh ahsante rais kwa agizo lako, wananchi wote tunaozunguka eneo la hifadhi tutoe ushirikiano ili tusaidie ktk kupambana na majangili hao!
 
Nasubiri kuona ujangili utapungua kwa kiasi gani kipindi hiki cha Magu....ili nijue kama JK ndo alikua anazingua ama kweli yalimshinda
 
Mbona hakutoa kauli kifo cha kinyama cha Alphince Mawazo,
Mbina hakukemea polisi kuingia bungeni na mbwa. Nampenda rais wangu ila asikubali kudanganywa na qasaidizi wake.
Mimi binafsi nimechukia kwa majangili kuuwa huyo rubani, ila pia ni vyema kukawa na mambo maalum ya Mh rais kuyazungumzia.
Jambo kama la Zanzibar, amekaa kimya au ni hadi kutokee machafuko ndipo akemee??
Acha kuchanganya mambo bwana
Mbona kilajambo mnaleta siasa za kitoto
Badilikeni
 
Rais kulaani jambo fulani si jambo la kawaida wala la kubeza. Baada ya kutolewa taarifa kuwa kuna mauwaji yamefanyika,ya Bwana Roger,yakiwahusisha majangili Rais ameguswa na kukasirishwa. Rais Magufuli na Serikali yake wapo katika vita vya ujangili,hasa wa tembo,nchini.

Kuuwawa kwa mshikadau wa vita ya ujangili ni jambo lililomgusa Mhe. Rais Magufuli. Rais ameagiza wahusika wasakwe na kuchukuliwa hatua. Agizo la Rais si la mchezo. Majangili wakae mkao wa maumivu makali. Kutamba kwao kunafikia mwisho tena kwa haraka.

Majangili wasisahau pia kuwa Katibu Mkuu,mtendaji mkuu wa Wizara,Wizara ya Maliasili na Utalii ni Meja Jenerali Millanzi. Naye wamembeep,wasubiri awapigie akilenga kulinda heshima na kuaminiwa kwake.
 
Back
Top Bottom