Rais Magufuli akutana na Viongozi wa vyama vya Siasa nchini, Maalim Seif(ACT-Wazalendo), Prof. Lipumba (CUF) na James Mbatia (NCCR-Mageuzi)

Kweli kabisa, siasa za kunyanganyana fito ilikhali wote mnajenga nyumba moja zimepitwa na wakati
Zitto karibu huku ushuhudie wanasiasa nguli wanaojua siasa. Wenzako matatizo ya nchi wanakaa chini na kuzungumza, wewe unaenda ugenini kuzungumza halafu unajiona mwamba wa siasa. Rudi darasani ukajifunze uzalendo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera sana Kwa Rais wetu mpendwa JPM Kwa kuonyesha Upendo Na umoja Kwa viongozi wa vyama vingine, hiyo ndio siasa safi tunayo itaka siasa sio uadui, sisi wananchi tunahitaji kuona siasa ya maendeleo sio matusi au ugonvi.

Viongozi wengine wa kisiasa waige mfano huu wa Maalim Seifu na hata Mbatia. Tanzania ni nchi yetu sote tuijenge Kwa pamoja bila kubomoa.

Mungu Ibariki Nchi yetu Tanzania
 
Si alisema ataenda kushitaki ICC kwamba uchaguzi wa Zanzibar umevurugwa?
Leo tena anasalimiana na rais kwa mbwembwe za miguu?
Tuamini lipi sasa sisi wana mabadiliko?

Kweli chadema majanga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli akiagana na Mwanasiasa Mkongwe ambaye ni Mwanachama wa Chama cha ACT Wazalendo

Maalim Seif Sharif Hamad mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam.View attachment 1375351

Sent using Jamii Forums mobile app

Salamu Yao sasa sio mchezo mwendo wa Miguu tu Saivi

Maalimu anacheza chess,wa ajabu fulani anacheza drafti
 
Hongera sana Kwa Rais wetu mpendwa JPM Kwa kuonyesha Upendo Na umoja Kwa viongozi wa vyama vingine, hiyo ndio siasa safi tunayo itaka siasa sio uadui, sisi wananchi tunahitaji kuona siasa ya maendeleo sio matusi au ugonvi,
Viongozi wengine wa kisiasa waige mfano huu wa Maalim Seifu na hata Mbatia.
Tanzania ni nchi yetu sote tuijenge Kwa pamoja bila kubomoa.
Mungu Ibariki Nchi yetu Tanzania
Sijaona ulipokemea matusi ya Magufuli kwa Wapinzani au wewe huwa huyasikii?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom