Rais Magufuli akamilisha uteuzi wa Baraza la Mawaziri, Makame Mbarawa abadilishiwa Wizara

Hili ndilo baraza la mawaziri lililosubiriwa kwa hamu zaidi ya mwezi mpja! Wengingine inabidi tuweke maneno ya akiba.
Mmh! Prof Magembe na Majangili wa tembo kweli jamani?
 
Napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza Dr John Pombe Magufuli kwa kumteua mmoja wa akina mama shujaa TZ, mama jembe, asiyeyumba na mchapakazi wa daraja la juu Dr Joyce Ndalichako. Ili taifa liweze kufaidika na kalama ya kipekee aliyojaliwa huyu mama, inabidi baadhi ya kazi za TAMISEMI-ELIMU azisimamie yeye. Ingependeza zaidi kama yeye ndiye angerithi cheo alichokuwa anasimamia Kassim Majaliwa, lakini halijaharibika jambo.Sasa ni wakati wa kuwaonyesha watanzania kuwa wapo wanawake mashujaa, wanaofaa hata kukabidhiwa taifa hii siku za mbeleni.

Nakushauri Dr utakapoanza kazi,pamoja na mengine,haya nayo uyaangalie;

  1. Agiza madai ya walimu ya siku nyingi,kama arrers,yahakikiwe na yalipwe mala moja
  2. Agiza sensa ya walimu ifanyike ili kujua kama kila mwalimu yupo daraja analostahili
  3. Agiza vyeti vya walimu vikaguliwe ili walimu vihiyo waondolewe
  4. Itisha kikao na CWT ili utatue matatizo sugu ya walimu
  5. Rudisha nidhamu ya utendaji kazi mashuleni kwa kuimarisha ukaguzi mashuleni
  6. Wakaguzi wa shule wapangwe katika level ya kata au tarafa, ili kuimarisha usimamizi wa ufundishaji
  7. Wakuu wa shule, maafisa elimu na wakurugenzi mizigo waondoe mala moja
  8. Ichunguze NECTA,maana uongozi wake unaonekana kuyumba,ikiwezekana mshauri rais afanye mabadiliko
  9. Rudisha heshima za shule kwa kufanya yafuatayo (a) Walimu wawepo shuleni muda wote wa kazi (b) Piga marufuku aina yoyote ya tuition kufanyika mashuleni (c) Himiza class journal,kila anapomaliza mwalimu kufundisha asaini (d) Agiza uchunguzi wa mwenendo wa kila mwalimu (bila kusahau mkuu wa shule) ufanyike ili kujiridhisha kama unafanana na maadili ya ualimu,maana mwalimu ni kioo cha jamii
  10. Ukigundua udhaifu kwa mtu yoyote yule mwondoe mala moja kama ulivyokuwa ukifanya NECTA
  11. Pendekeza kwenye baraza la mawaziri juu ya kuongeza maslahi ya walimu ili yafanane na kada zingine
  12. Fanyeni uchunguzi kama kuna ulazima wa kuendelea kuwa na ma-DEO wawili kwa kila wilaya,wa msingi na wasekondari

Ni jambo la kumshukuru mungu kuwa wizara nyeti wamepewa akina mama. Tunaamini mtafanya kila muwezalo kuiboresha elimu nchini. Kwa namna wafanyakazi wa wizara hii walivyojisahau na kulala! mna kazi ngumu ya kuwaamusha. Mtalazimika kuchukua maamuzi mengi magumu ikiwepo kushusha watu vyeo na wengine kuwafukuza.Msiogope,anzeni na wakubwa,safisheni wote walio wachafu kabla hawajawa kansa.Waonyesheni watanzania na ulimwengu mzima kuwa wanawake wanaweza. Nawatakieni kazi njema. Mkiiweza hii wizara,hatutashangaa kusikia rais wa 2025 akawa mwanamke, Dr Ndalichako.
 
Katika teuzi zote za Magufuli,
Hii ya wizara ya elimu ni bora zaidi,sababu hata wananchi walikua na kiu ya kumpata waziri kama huyu Mama
 
huo ni mpango wa maandalizi ya bajeti ya kihistoria kuwahi kutokea in contemporary dayz

Hakika Mkuu huyu mtu ni mtu wa greater Vision, Budget ijayo naamini kila mtu atashuhudia mabadiliko nasema tena huyu ni mzalendo kweli kweli
 
kote mi namuunga mkono , waliofanya vibaya huenda haikuwa kwa matakwa yao, JPM kawaweka weledi na naamini uadilifu ukitumika kuwaongoza tutafika tunakokuota.

Tugangeni yajayo TUFANYE KAZI!
 
Katika teuzi zote za Magufuli,
Hii ya wizara ya elimu ni bora zaidi,sababu hata wananchi walikua na kiu ya kumpata waziri kama huyu Mama

Mkuu huyu mama kuteuliwa waziri wa Elimu?
 
Katika teuzi zote za Magufuli,
Hii ya wizara ya elimu ni bora zaidi,sababu hata wananchi walikua na kiu ya kumpata waziri kama huyu Mama

BAKWATA Yataka Dk Joyce
Ndalichako Ajiuzulu:
Kisa Ukinyonga Katika Katokeo ya
Mitihani Form VI
BARAZA la Waislamu Tanzania
(Bakwata) limemtaka Katibu Mtendaji
wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk
Joyce Ndalichako kujiuzulu wadhifa
huo akimtuhumu kuwafelisha mitihani
ya dini ya Kiislamu wanafunzi wa
kidato cha sita wa dini hiyo.
Kauli hiyo ya Bakwata imetolewa na
Mufti wa Tanzania, Sheikh Issa Bin
Shaaban Simba katika mkutano wake
na waandishi wa habari jijini Tanga jana
kuelezea msimamo wa Waislamu
nchini kuhusu matokeo ya kidato cha
sita, hujuma inayoandaliwa kufanyika
katika zoezi la sensa pamoja na
vurugu zilizotokea Zanzibar.
Kuhusu hujuma ya mtihani, Mufti
Simba alisema kuwa matokeo ya
mtihani ya dini hiyo ya Kidato cha Sita
yaliyotangazwa Mei Mosi 2012,
yaliwashtua wanafunzi Waislamu
waliofanya mtihani wa elimu ya dini ya
kiislamu (Islamic Knowledge), ambayo
yalionyesha kuwa asilimia 70 walifeli
kwa kupata daraja F.
Alisema matokeo hayo yalionyesha
kuwa ni asilimia 30 ndiyo waliofaulu
kwa kupata daraja D, ambapo
waliopata alama za juu kabisa nchi
nzima ni wanafunzi saba
pekee.?Matokeo haya yaliwashtua
wanafunzi na wazazi, taasisi
mbalimbali za kiislamu zilimua kukata
rufaa kuonyesha kutokubaliana na
matokeo hayo, hatimaye baraza hilo
likabaini kuwa lilikosea na likaidhinisha
kutolewa matokeo
mapya,? alisema Mufti Simba.
Tayari Ndalichako ametoa ufafanuzi
kuwa kosa lililotokea akisema si
hujuma bali ni la kiufundi lililotokana na
kubadili utaratibu wa kufanya mitihani
mitatu ya somo hilo kuwa miwili, lakini
mfumo wa ujumlishaji maksi
ulisahaulika kubadilishwa.
Ndalichako alilieleza gazeti dada la
Mwananchi, The Citizen, kuwa awali
matokeo ya mitihani mitatu yalikuwa
yanajumlishwa na kugawanywa kwa
tatu kwa kutumia mfumo wa kompyuta,
ili kupata alama rasmi za mtahiniwa,
lakini safari hii zilipojumlishwa alama
za mitihani miwili ya somo hilo
ziliendelea kugawanywa kwa tatu
badala ya mbili kimakosa.
Habari zilizopatikana kutoka Necta
zimesema kuwa baada ya kupata
malalamiko ya wanafunzi hao,
uchunguzi ulifanyika na kubaini kasoro
hiyo ambapo ilirekebishwa.Mei 30,
mwaka huu Necta ilikutana na Baraza
la Wakuu wa Shule za Kiisilamu na
kufafanua suala hilo, ambapo
ilionekana tatizo hilo si hujuma bali
kosa la kiufundi.
Mwenyekiti wa Islamic Education
Panel, Pilly H.H alimwandikia barua
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi na nakala kwa
Katibu Mtendaji wa Necta, Amir,
Jumuia na Taasisi za Kiislamu
Tanzania akishukuru wizara kwa hatua
zilizochukuliwa.
?Tunashukuru kwa jinsi Wizara ya
Elimu na mafunzo ya ufundi ilivyopokea
suala hili kwa uzito unaostahiki?Tun
atoa shukurani za pekee kwa katibu
mtendaji wa baraza la mitihani kwa
hatua alizochukua ndani ya muda
mfupi sana, nashukuru kwa
ushirikiano,? ilisema barua hiyo
iliyoandikwa na Mwenyekiti wa Baraza
la Wakuu wa Shule za Kiislamu.
Hata hivyo, akisistiza hoja yake Mufti
Simba alisema kuwa matokeo
yaliyotolewa upya yalionyesha
kwamba wanafunzi zaidi ya asilimia 70
ya wanafunzi walifaulu, jambo ambalo
Waislamu wanaamni kwamba ni
hujuma inayolenga kupunguza idadi ya
wanafunzi wa Kiislamu wa kujiunga na
vyuo vikuu.
Mufti huyo alisema jambo
lililomshangaza yeye pia pamoja na
Waislamu wote nchini ni tamko
lililotolewa na Ndalichako kupitia
vyombo vya habari Jumanne iliyopita
aliposema kuwa Baraza la Mitihani
halikukosea kutoa matokeo hayo kwa
kuwa waliosahihisha ni walimu wenye
sifa.
?Bakwata inamshangaa Katibu Mtendaji
wa Baraza la Mitihani, Ndalichako kwa
kauli yake aliyoitoa kupitia vyombo vya
habari juzi 5/6/2012 akisema hakuna
hujuma na mitihani inasahihishwa na
walimu wenye sifa na wanachaguliwa
na wakuu wa shule zao,?alisema Mufti
Simba.
Alisema hoja iliyotolewa na Ndalichako
kwamba wanaosahihisha ni wenye
uzoefu haina mashiko kwa sababu
Waisalmu wanacholalamikia ni mfumo
mzima wa ?Conveyor Belt?, aliodai
umewekwa kuwahujumu wanafunzi
Waislamu.
Alisema matokeo hayo ya mtihani wa
somo la kiislamu umeonyesha kuwa
upo wasiwasi kwamba kilichofanyika
huko ndicho wanachofanyiwa
wanafunzi wa kiislamu katika masomo
mengine kuanzia darasa la saba,
kidato cha nne na hata vyuo vikuu kwa
lengo la kupunguza idadi ya wasomi
waislamu.
?Waislamu tunaamini kwamba hila
kama hii inafanyika pia kwenye
masomo mengine, kwa maana hiyo
tunataka Ndalichako na watendaji
wengine wajiuzulu ili kuondoa kashfa
hii kwa Serikali, pia kuleta imani ya
Waislamu kwa Serikali yao, ?alisema
Mufti Simba.
Alifafanua kuwa baada ya kujiuzulu,
Serikali iunde tume ya kuchunguza
hujuma zilizotendeka katika baraza
hilo dhidi ya Waislamu kwa kipindi cha
miaka 10 iliyopita akieleza kuwa
Waislamu wanaamini kwamba
wanafunzi wengi
wamefelishwa kwa kusudi maalumu la
kuzorotesha kizazi chao.
SUALA LA SENSA YA WATU NA
MAKAZI.
Kuhusu Sensa, Mufti Simba alisema
kuwa kalenda iliyotolewa na Ofisi ya
Waziri Mkuu, takwimu zinaoonyesha
kuwa idadi ya Watanzania ni 43 milioni
ambapo Wakristo ni asilimia 52,
Waislamu asilimia 32 na dini nyingine ni
asilimia 16 akieleza kuwa takwimu hizo
si sahihi.
Alisema kuwa Bakwata inalaani kitendo
hicho alichosema kinapotosha
wananchi kwa kuwa sensa iliyofanyika
mwaka 2002 kipingele kinachobainisha
dini za Watanzania kiliondolewa.
MGOGORO WA ZANZIBAR
Akizungumzia matukio yauvunjifu wa
amani vilivyotokea visiwani Zanzibara
hivi karibuni Mufti Simba alisema
Bakwata inalaani kitendo inalaani
kitendo hicho ikiamini kwamba
waliofanya vurugu hizo siyo Waislamu
bali ni
wahuni.
Alishauri kuundwa kamati ya pamoja
kati ya Serikali na kikundi cha
Waislamu cha Uamsho ili kuchunguza
waliohusika na vurugu hizo na
waliohusika kuchukuliwa hatua.
Bakwata yataka Dk Ndalichako ajiuzulu
mwananchi.co.tz
June 7, 2012 at 4:59am ? Public
 
Mbona Makame Mbarawa tayari yeye ni waziri wa Maji na Umwagiliaji, inakuwaje tena awe waziri wa mawasiliano na uchukuzi?
Mmh hii kitu ni uongo kabisa.
Kahamishiwa wizara nyingine,usipende kubisha kitu usichokijua,wakati mwingine sio lazima utoe maoni yako kama huna uhakika a unachokiandika,hilo la inakuwaje tena mwenye jibu ni Mh raisi Magufuli ambaye anateua ,anatengua,anafukuza n.k
 
Hata angechagua ngo'mbe aongoze kwangu sawa tu cha msingi kile chama cha kigalatia a.k.a waoza meno kimepigwa chini pamoja na yule mzee wa kujinyea
 
Hongera ndalichako sisi tunskupokea kwa mikono miwili ila tafadhalii kuwa makini na kompyuta hzo hspo wzarani mama
 
BAKWATA Yataka Dk Joyce
Ndalichako Ajiuzulu:
Kisa Ukinyonga Katika Katokeo ya
Mitihani Form VI
BARAZA la Waislamu Tanzania
(Bakwata) limemtaka Katibu Mtendaji
wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk
Joyce Ndalichako kujiuzulu wadhifa
huo akimtuhumu kuwafelisha mitihani
ya dini ya Kiislamu wanafunzi wa
kidato cha sita wa dini hiyo.
Kauli hiyo ya Bakwata imetolewa na
Mufti wa Tanzania, Sheikh Issa Bin
Shaaban Simba katika mkutano wake
na waandishi wa habari jijini Tanga jana
kuelezea msimamo wa Waislamu
nchini kuhusu matokeo ya kidato cha
sita, hujuma inayoandaliwa kufanyika
katika zoezi la sensa pamoja na
vurugu zilizotokea Zanzibar.
Kuhusu hujuma ya mtihani, Mufti
Simba alisema kuwa matokeo ya
mtihani ya dini hiyo ya Kidato cha Sita
yaliyotangazwa Mei Mosi 2012,
yaliwashtua wanafunzi Waislamu
waliofanya mtihani wa elimu ya dini ya
kiislamu (Islamic Knowledge), ambayo
yalionyesha kuwa asilimia 70 walifeli
kwa kupata daraja F.
Alisema matokeo hayo yalionyesha
kuwa ni asilimia 30 ndiyo waliofaulu
kwa kupata daraja D, ambapo
waliopata alama za juu kabisa nchi
nzima ni wanafunzi saba
pekee.?Matokeo haya yaliwashtua
wanafunzi na wazazi, taasisi
mbalimbali za kiislamu zilimua kukata
rufaa kuonyesha kutokubaliana na
matokeo hayo, hatimaye baraza hilo
likabaini kuwa lilikosea na likaidhinisha
kutolewa matokeo
mapya,? alisema Mufti Simba.
Tayari Ndalichako ametoa ufafanuzi
kuwa kosa lililotokea akisema si
hujuma bali ni la kiufundi lililotokana na
kubadili utaratibu wa kufanya mitihani
mitatu ya somo hilo kuwa miwili, lakini
mfumo wa ujumlishaji maksi
ulisahaulika kubadilishwa.
Ndalichako alilieleza gazeti dada la
Mwananchi, The Citizen, kuwa awali
matokeo ya mitihani mitatu yalikuwa
yanajumlishwa na kugawanywa kwa
tatu kwa kutumia mfumo wa kompyuta,
ili kupata alama rasmi za mtahiniwa,
lakini safari hii zilipojumlishwa alama
za mitihani miwili ya somo hilo
ziliendelea kugawanywa kwa tatu
badala ya mbili kimakosa.
Habari zilizopatikana kutoka Necta
zimesema kuwa baada ya kupata
malalamiko ya wanafunzi hao,
uchunguzi ulifanyika na kubaini kasoro
hiyo ambapo ilirekebishwa.Mei 30,
mwaka huu Necta ilikutana na Baraza
la Wakuu wa Shule za Kiisilamu na
kufafanua suala hilo, ambapo
ilionekana tatizo hilo si hujuma bali
kosa la kiufundi.
Mwenyekiti wa Islamic Education
Panel, Pilly H.H alimwandikia barua
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi na nakala kwa
Katibu Mtendaji wa Necta, Amir,
Jumuia na Taasisi za Kiislamu
Tanzania akishukuru wizara kwa hatua
zilizochukuliwa.
?Tunashukuru kwa jinsi Wizara ya
Elimu na mafunzo ya ufundi ilivyopokea
suala hili kwa uzito unaostahiki?Tun
atoa shukurani za pekee kwa katibu
mtendaji wa baraza la mitihani kwa
hatua alizochukua ndani ya muda
mfupi sana, nashukuru kwa
ushirikiano,? ilisema barua hiyo
iliyoandikwa na Mwenyekiti wa Baraza
la Wakuu wa Shule za Kiislamu.
Hata hivyo, akisistiza hoja yake Mufti
Simba alisema kuwa matokeo
yaliyotolewa upya yalionyesha
kwamba wanafunzi zaidi ya asilimia 70
ya wanafunzi walifaulu, jambo ambalo
Waislamu wanaamni kwamba ni
hujuma inayolenga kupunguza idadi ya
wanafunzi wa Kiislamu wa kujiunga na
vyuo vikuu.
Mufti huyo alisema jambo
lililomshangaza yeye pia pamoja na
Waislamu wote nchini ni tamko
lililotolewa na Ndalichako kupitia
vyombo vya habari Jumanne iliyopita
aliposema kuwa Baraza la Mitihani
halikukosea kutoa matokeo hayo kwa
kuwa waliosahihisha ni walimu wenye
sifa.
?Bakwata inamshangaa Katibu Mtendaji
wa Baraza la Mitihani, Ndalichako kwa
kauli yake aliyoitoa kupitia vyombo vya
habari juzi 5/6/2012 akisema hakuna
hujuma na mitihani inasahihishwa na
walimu wenye sifa na wanachaguliwa
na wakuu wa shule zao,?alisema Mufti
Simba.
Alisema hoja iliyotolewa na Ndalichako
kwamba wanaosahihisha ni wenye
uzoefu haina mashiko kwa sababu
Waisalmu wanacholalamikia ni mfumo
mzima wa ?Conveyor Belt?, aliodai
umewekwa kuwahujumu wanafunzi
Waislamu.
Alisema matokeo hayo ya mtihani wa
somo la kiislamu umeonyesha kuwa
upo wasiwasi kwamba kilichofanyika
huko ndicho wanachofanyiwa
wanafunzi wa kiislamu katika masomo
mengine kuanzia darasa la saba,
kidato cha nne na hata vyuo vikuu kwa
lengo la kupunguza idadi ya wasomi
waislamu.
?Waislamu tunaamini kwamba hila
kama hii inafanyika pia kwenye
masomo mengine, kwa maana hiyo
tunataka Ndalichako na watendaji
wengine wajiuzulu ili kuondoa kashfa
hii kwa Serikali, pia kuleta imani ya
Waislamu kwa Serikali yao, ?alisema
Mufti Simba.
Alifafanua kuwa baada ya kujiuzulu,
Serikali iunde tume ya kuchunguza
hujuma zilizotendeka katika baraza
hilo dhidi ya Waislamu kwa kipindi cha
miaka 10 iliyopita akieleza kuwa
Waislamu wanaamini kwamba
wanafunzi wengi
wamefelishwa kwa kusudi maalumu la
kuzorotesha kizazi chao.
SUALA LA SENSA YA WATU NA
MAKAZI.
Kuhusu Sensa, Mufti Simba alisema
kuwa kalenda iliyotolewa na Ofisi ya
Waziri Mkuu, takwimu zinaoonyesha
kuwa idadi ya Watanzania ni 43 milioni
ambapo Wakristo ni asilimia 52,
Waislamu asilimia 32 na dini nyingine ni
asilimia 16 akieleza kuwa takwimu hizo
si sahihi.
Alisema kuwa Bakwata inalaani kitendo
hicho alichosema kinapotosha
wananchi kwa kuwa sensa iliyofanyika
mwaka 2002 kipingele kinachobainisha
dini za Watanzania kiliondolewa.
MGOGORO WA ZANZIBAR
Akizungumzia matukio yauvunjifu wa
amani vilivyotokea visiwani Zanzibara
hivi karibuni Mufti Simba alisema
Bakwata inalaani kitendo inalaani
kitendo hicho ikiamini kwamba
waliofanya vurugu hizo siyo Waislamu
bali ni
wahuni.
Alishauri kuundwa kamati ya pamoja
kati ya Serikali na kikundi cha
Waislamu cha Uamsho ili kuchunguza
waliohusika na vurugu hizo na
waliohusika kuchukuliwa hatua.
Bakwata yataka Dk Ndalichako ajiuzulu
mwananchi.co.tz
June 7, 2012 at 4:59am ? Public
 
FaizaFoxy na Ritz waione hii.... Maulid imeingia nzi!!!! Dr. Ndalichako alisaini vyeti vyangu vya form four na six!
Namfagilia sana mama huyu! Haya majitu yaliua elimu kabisa!!!

Atakuwa ametubu dhambi zake, maana ngazi aliachia mwenyewe. Ni heri ametubu kiukweli lakini kama ametubu kiuongo-uongo ataumbuka tu kama alivyoumbuka Lowassa.
 
Atakuwa ametubu dhambi zake, maana ngazi aliachia mwenyewe. Ni heri ametubu kiukweli lakini kama ametubu kiuongo-uongo ataumbuka tu kama alivyoumbuka Lowassa.
Bibie, kumbe bado upo? Hujaanza kuisoma namba kama swahiba wako wa Msoga?
 
Back
Top Bottom