Rais Magufuli ajiandikisha kwenye daftari la mpiga kura kitongoji cha Sokoine. Asema amehamia Ikulu ya Chamwino, Dodoma

Mji wa Dodoma haukaliki, hauna hali ya hewa nzuri kwa Mabaharia.
Usiku baridi Kali, mchana joto Kali na Vumbi.
Ni ukame ukame Hadi mwarobaini unashindwa kustawi.
Kuhamishia Ikulu Dodoma Ni habari ya kusadikika.
Hakuna Raisi atakayeweza kuhamia Dodoma, labda mwezi mmoja kabla muda wake kuisha.
Ila hakuwa kwenye ile mood ya kawaida as if hakuridhia kuwepo pale, anyway, tumsubiri muda uongee, isiwe ofisi chamwino kulala magogoni.
 
Wakuu naomba kuuliza Mh. Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli anaishi Dodoma au Dar es Salaam.

Nauliza kwa sababu alituambia kahamia Dodoma ila namuona Dar kila siku.
 
Rais Magufuli na mke wake mama Janeth leo wamejiandikisha katika uchaguzi wa serikali za mitaa pale mtaani kwake Chamwino katika kitongoji cha Sokoine mjini Dodoma.

Rais Magufuli ambaye amefika mtaani kwake akitokea ziarani Mpanda imemlazimu kupanga foleni baada ya kuwakuta jirani zake wakiwa katika mstari wakiendelea kujiandikisha.

Bado siku 2 hima hima watanzania tukajiandikishe

Source Channel ten tv
Maendeleo hayana vyama!
Kanuni za mpiga kura zinasemaje, watu elfu moja wanaweza wakahamia leo na wiki ijayo wakajiandikisha hapo kupiga kura na wakimaliza wanarudi walikotoka! Hatuelewi tunachokifanya.
 
Rais Magufuli amejitokeza katika kitongoji cha Sokoine jijini Dodoma kwa ajili ya kujiandikisha kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Baada ya kujiandikisha, amewaambia wakazi wa eneo hilo kuwa kwa sasa yeye ni mwenzao na ameshahamia rasmi kwenye Ikulu ya Chamwino. Hivyo yeye ni mwenzao.

Amewaambia wananchi kuwa amehamia Ikulu ya Chamwino ingawa bado haijakamilika rasmi.


Chanzo: Chanel Ten
Sisi wengine haturuhusiwi kuhama tukajiandikisha kwenye makao yetu mapya mpaka tutimize muda wa miaka 10
 
Back
Top Bottom