Rais Magufuli ajiandikisha kwenye daftari la mpiga kura kitongoji cha Sokoine. Asema amehamia Ikulu ya Chamwino, Dodoma

Watumishi na wenye dhamana ya kushawishi raia kujiandikisha, mnaona Rais anavyojitahidi kutushawhishi...

Sasa ole wenu nyie, kama hamna plan...

Cc: mahondaw
 
Mji wa Dodoma haukaliki, hauna hali ya hewa nzuri kwa Mabaharia.
Usiku baridi Kali, mchana joto Kali na Vumbi.
Ni ukame ukame Hadi mwarobaini unashindwa kustawi.
Kuhamishia Ikulu Dodoma Ni habari ya kusadikika.
Hakuna Raisi atakayeweza kuhamia Dodoma, labda mwezi mmoja kabla muda wake kuisha.
 
Rais wa Tanzania, John Magufuli ametangaza kuhamia Dodoma kuanzia leo Jumamosi Oktoba 12, 2019.

Rais Magufuli amesema hayo mara baada ya kumaliza kujiandika katika orodha ya wapiga kura ya serikali za mitaa akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli.

Wawili hao wamejiandika katika kituo cha Sokoine kilichopo katika Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma baada ya kuwasili wakitoka mkoani Katavi.

Baada ya kujiandikisha, Rais Magufuli amesalimiana na wananchi wa Chamwino waliokuwa wamejitokeza kujiandikisha katika kituo hicho na kuwaeleza kuwa pamoja na kwamba miundombinu ya Ikulu ya Chamwino bado haijakamilika yeye ameshahamia Dodoma.

“Mimi nilikuwa Katavi, nimeamua kuja kujiandikisha nyumbani kwa sababu hapa ndio nyumbani kwangu, na nimeshakuja rasmi hapa, kwa hiyo kila siku tutakuwa tunaonana hapa, ndio maana nimeona nije nijiandikishe mimi pamoja na mke wangu” amesema Rais Magufuli.

Uamuzi huo wa Rais Magufuli umehitimisha ahadi yale aliyoitoa huko nyuma ya kuhamia Dodoma kwani tayari Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wizara na taasisi mbalimbali zilikwisha kuhamia Dodoma.

Kuhusu uchaguzi, Rais Magufuli amewataka Watanzania kuendelea kujitokeza katika vituo vya kujiandikisha vilivyopo nchi nzima ili Novemba 14, 2019 waweze kutumia haki yao ya kikatiba ya kuwachagua viongozi wa Serikali za Mitaa watakaowana wanafaa.

Aidha, Rais Magufuli amewapongeza waandishi wa habari wa Mkoa wa Dodoma waliofika katika kituo hicho kwa kutekeleza majukumu yao ya uandishi wa habari na amewasisitiza kuendelea kutimiza majukumu hayo kwa weledi na kwa kutanguliza maslahi ya Taifa.

Baadaye, Rais Magufuli amewaalika waandishi wa habari hao na kula nao chakula cha mchana, nyumbani kwake katika Ikulu ya Chamwino.
 
Nashukuru kupata nafasi kuwa wa pili kukomenti.
Hongera sana mheshimiwa rais kuhamia nyumbani rasmi.
 
Mwaka wa nne huu anatangaza tu kuhamia dodoma na haendidar kutamu bana
Rais Magufuli amejitokeza katika kitongoji cha Sokoine jijini Dodoma kwaajili ya kujiandikisha kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Baada ya kujiandikisha, amewaambia wakazi wa eneo hilo kuwa kwasasa yeye ni mwenzao na ameshahamia rasmi kwenye ikulu ya Chamwino. Hivyo yeye ni mwenzao.

Amewaambia wananchi kuwa amehamia Ikulu ya Chamwino ingawa bado haijakamilika rasmi.

Chanzo: Chanel TenView attachment 1230555
 
Karibu Dodoma Tata Mkulu!
 
Keeping your promises. Hongera sana JPM
 
Niko nae tayari kashasaini ila yule muhudumu alikuwa anajishtukia sana hadi kalamu kidogo ashindwe kuishika
Keshafika Dom tayari? Sialikuwa ufipa? Hakyamungu nchi hii inajengwa, kaendaje kutoka huko sumbawanga?

Nasikia Kuna ka bibi kila akikatiza kapo, mwishowe akauliza akaambiwa Ni mamayake na mlinzi wake, kumbe huwa anatembea nako mgongoni chezea mfipa wewe!
 
Kwa nini uandikishaji huu haukufanywa na Tume ya uchaguzi na kuboresha daftari la wapiga kura kwa uchaguzi serikali za mitaa pamoja na uchaguzi mkuu?

Baada uchaguzi serikali za mitaa, Tume ya uchaguzi nao watafanya zoezi la kuboresha daftari la wapiga kwa kuandikisha wapiga kura walewale na wachache watakaotimiza umri na vigezo vingine hapo 2020?

Kwa nini vitambulisho vya mpiga kura visitumike uchaguzi serikali za mitaa?
 
Back
Top Bottom