johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 104,319
- 183,600
Kasi ya Rais Magufuli katika kushughulikia kero mbalimbali za wananchi kumewafanya wakosoaji wake wakuu Chadema kuishiwa pumzi. Chadema ilikuwa ikiamini katika vita dhidi ya ufisadi lakini Magufuli anapambana na mafisadi kivitendo hali iliyowafanya Chadema wageuke kuwa watetezi wa mafisadi. Kwa upande wa elimu Bure huko Rais Magufuli ameshafunga kazi elimu ya msingi na sekondari ni bure hali iliyowafanya baadhi ya wabunge wa Chadema kuvua magwanda na kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kujiunga na CCM. Kimsingi Chadema imeshaondolewa relini na sasa imebakia kuendesha siasa za matukio.