Rais Magufuli acha kumdhalilisha Kikwete

Hilo ndo limekukwaza! Vipi wakati wa kampeni jk alisema amewatoa watz mbali hadi amewafikisha hapa! Na jpm akasema mafisadi ndo wametufikisha hapa
 
sina lengo baya Bali kama mtanzania nimeguswa na one man show anayofanya mh dk magufuli.
ushahidi.

kutembelea muhimbili na kuzungumzia mambo mazito.

"" Juzi rais Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza Muhimbili na kumwondoa mkurugenzi na bodi ingawa bodi ilishamaliza muda wake na mkurugenz kahamishiwa wizarani tu wala hajafukuzwa.

Ikulu ikadai Magufuli alikasirishwa sana kukuta mashine za MRI hazifanyikazi ndio maana kaisimanisha bodi,
Lakini jana kupitia Azam Tv Katibu mkuu wizara ya Afya Bw.Mbando alisema mashine haikutengenezwa kwa sababu Magufuli alisema bali ilikuwa tu kwamba akivyotenbekea pale mchakato wa kuikarabati mashine ulishakamilika.

Alisema tatizo lililokuwepo ni kwamba Phillips wanaidai serikali zaidi ya bil 7 ndio maana waligoma kuitengeneza hiyo nashine.

Sasa mchakato wa kupunguza deni ndio ulikuwa unaendelea na zilishapatikana bil3 kutoka hazina walizolipwa juzi hao Phillips ndipo wakakubali kuja kuifanyia mashine ukarabati.

Na hili linaleta maana zaidi kwa sababu wizara haiwezi kutoa bil3 ghafla tu bila kuwa zilikuwa kwenye mchakato.

Kwa hiyo hapa ikulu ilifanya usanii wa hali ya juu kuwaaminisha watanzania kwamba kulikuwa na uzembe pale muhimbili wakati uzembe ulikuwa serikalini. Serikali ilishindwa kulipa deni kwa wakati.

Na inasemeka hili jambo halikumfurahisha Kikwete kwa sababu lilipeleka picha kwamba serkali yake ilikuwa goigoi.

Wakati yeye anasema amefanya juhudi kubwa kuiboresha Muhimbili. Na kwamba tatizo km la juzi linajulikana kwamba ni ukata na ufinyu wa bajeti ndio kikwazo.
.
.safari za nje zimeiletea serikali fedha ambazo zimetumika kujenga barabara, kuboresha miundombinu ya umeme,ujenz wa bandari mpya, ujenzi wa chuo kikuu cha tiba na mambo mengi sana kwa juhudi za kikwete.
" kuna watu wamesafiri nje kuliko safari za kwenda kumsalimia mama yake" kauli hii ya magufuli haivumiliki na kauli iliojaa jeuri.

.kila kilichofanywa na kikwete kuonekana ni tatizo kwa mh magufuli.

kikwete aliunda baraza kubwa la mawaziri ili kurahisisha kuwahudumia wananchi kuliko kuwa na wizara chache kwa watu. million 50
sasa magufuli kudai kunawizara nyingi atazifuta naona lengo ni kuonyesha kuwa utawala wa kikwete ulikuwa dhaifu .

conclusion.
Haina haja kudhalilisha uongozi uliopita ili uonekane u nafanya kazi. rais kama unapitia hapa JF kuna wanachama hawako satisfied kwa namna unavoenenda.
asante.
Siamini kuwa katika utendaji wake wa kazi Magufuli amelenga kumdhallisha Jakaya
 
Ningekuelewa ungesema Magufuli atapata asilimia 99 lakni sio ccm maana watz sasa wanataka mtu wala sio chama maana aliyetufikisha hapa ni chama na JP anajaribu kututoa kwenye tope

Hahahaaa! Kwani we Ukisema chama unamaanisha nini?
 
we mtoa post unapigwa mbupu kama vipi
attachment.php
 

Attachments

  • 12299278_1650361578579985_7151444045452596312_n.jpg
    12299278_1650361578579985_7151444045452596312_n.jpg
    5.6 KB · Views: 1,180
Kwa hali ilivyo na inavyokwenda, nauliza tena muhishiwa bado unalala vizuri na usingizi unakujavizuri? Heehee, kazi kweli.
 
mtoa mada umeghafilika. pengine ulikuwa unataka kusema kitu kingine ukakisahau. hakuna mahali popote tingatinga jpm amemshutumu rais kikwete kwa kushndwa kutekeleza wajibu wake. hisia zako za kichochezi ni hatari kama kipindupindu. unataka kutuambia watz tingatinga jpm asidhubutu kufanya mambo yanayofaa kwa taifa hili kwa kuhofia atakuwa anawakosoa waliomtangulia? sasa kulikuwa na sababu gani ya kufanya mabadiliko ya uongozi? kuwa na amani nawala rais kikwete hajalalamika
 
Kwa hali ilivyo na inavyokwenda, nauliza tena muhishiwa bado unalala vizuri na usingizi unakujavizuri? Heehee, kazi kweli.
Bila shaka analala vizuri, ana mafao ya kutosha. Shida iko kwangu na kwako ambao salio halitoshi!!
 
Mtoto wake nasikia kila siku pressure inapanda inashuka. Na kaacha kabisa kupost picha za Magufuli Insta na FB.....
 
wacha afanye yake, watendaji walishindwa

Ila chodechonde magu, wengine wana presha... we fanya ziara zako, kesho tuanze kusikia una kesi za kuua watu kwa presha
 
Kikwete alikuja na yake na kuna watu walisema anamdhalilisha Mkapa. Mzee Mwinyi alishasema, kila zama na kitabu chake. Hii ya zama ya Magufuli, ya Kikwete ni historia.

Sasa unataka nini? Mbona hujaongelea ya TRA? Wenzio wametoa orodha ya makontena kukwepa wambea kama wewe. Maneno mengi hoja ya maana hamna.

Acheni Magufuli afanye kazi ili ahukumiwe kwa matendo yake. Nani asiyejua safari zisizo na tija za Kikwete kuzunguka dunia nzima. Alikuwa anashinda angani kuliko ma pilot wa mashirika kama KLM!
 
Akili zako ni ndogo,, huu ni awamu nyingine ya uongozi na mambo yake !
Mzee, pombe fanya mambo yako kwa uhuru
isitoshe hili jambo limetokea simu nyingi , wewe unatuletea hapa leo ili iweje ?
Leo tunaongelea issue ya kamishna mkuu wa TRA kupigwa chini

Ha! kumbe hata mafisiemu wanaisoma namba wenyewe kwa wenyewe?.can't believe this
 
Back
Top Bottom