Tetesi: Rais kuanza ziara ya siku 6 Canada mwezi ujao


Ndio maana nikasema Wakoloni hawakuondoka kwa sababu hatukuwataka, waliondoka kwa sababu ilikuwa ni lazima waondoke na hawakutaka kuishi hapa kwani wangetaka wangeishi kwa nguvu kama wanavyoishi AK, Amerika isitoshe Mzungu wa AK anayeitwa Boer ambaye ni Muholanzi asili yake maana au tafsiri ya Boer ni Mkulima na waliondoka Uholanzi wakitafuta sehemu ya kulima iliyofaa na Afrika Kusini ilifaaa na ndio maana waliseto huko, walipita kote huku kwetu lkn walishindwa ardhi na hali ya hewa siyo rafiki kama AK kwa kilimo chao …
 
Nyamuhanga watakuwa wameisha litafuna buyu lote.Ile Politburo 2025 itamsumkumia pembeni ikisema ,tupishe,umeharibu nchi.
 
Wanaume akina Thompom wanarudi🤣🤣
 
Bila Katiba mpya itakuwa kila Rais akija anafanya yake anavyojisikia.

Imagine Rais fulani anakuwa haamini katika kutembelea nchi nyingine mara nyingi halafu akija mwingine anafanya kinyume chake!

Sasa tuchukulie nani anafanya Kwa usahihi kati ya wawili?

Sasa hapa panakuwa na kitendawili ambacho kinapadwa kuteguliwa na Katiba.
 
Nani amekudanganya ? Unafikiri kwa nini Wakulima wa Kizungu hawa kuseto Afrika badala yake wakahamia Bara Amerika ? Hata Afrika yenyewe sehemu pekee waliohamia ni Afrika Kusini ambaye climate yake ni tofauti kabisa na Tanzania!
Wewe unaishi wapi?Wakulima wepi walihamia Marekani?
Una maana wahamiaji waliokimbia njaa Ulaya kutoka Nchi mbalimbali kama Ireland,Great Britain,Germany,Sweden na Norway?
Wazungu walowezi walikuwepo Tanzania na walikimbizwa na Azimio la Arusha,wapo Kenya mpaka sasa wana ardhi kubwa sana mmojawapo maarufu ni Lord Delaware.Walikuwepo Zimbabwe wakafukuzwa na Mugabe na kuporwa mashamba yao.
Wapo Zambia.
 
Vasco da gama wa kike huyu.
Tunataka aelekee china kupata viwanda sio kuhangaika kutumika na wenye mahoteli wa kitaliani kupata watalii wajaze mahoteli yao.
 
Hiyo si angeunganisha huko huko baada ya kutoka marekani....
 
Hapa si ndio inaitwa kubalance au nakosea??!

Sent from my SM-G9250 using JamiiForums mobile app
 
Vasco Dagama
 

Zimbabwe wapo wazungu kibao, nenda Kenya hapo wamejaa tele, nenda Arusha kuna wazungu wengi tu wanalima maua. Acha kulazimisha mambo yasiyokuwepo.
 
Tatizo kubwa kuliko yote ni umasikini wa fikra.
Hakuna atakayekuja kuwekeza kwa faida ya wananchi. Kila anayewekeza ni kwa faida yake.
Nchi inaendelezwa na wananchi wake yenyewe vinginevyo itakuwa ya hao wawekezaji wageni ili waiendeleze.
Hata hivyo, uwekezaji wa wageni ni muhimu kama chachu tu ya kuwaamsha wenye nchi na ni lazima kuwe na sera rasmi za kuwaibua wazawa.
Huwezi kutenganisha utajiri wa taifa na ile wa raia mmoja mmoja.
Raia masikini hufanya nchi kuwa masikini na kinyume chake.
 
Sasa ni dhahiri kwamba CCM wamefanya U-turn kuhusu dhana ya UBEBERU.

Hiki ndicho chama kitakachowaletea wananchi wa Tanzania maendeleo...Leo hivi kesho vile hakuna mwendelezo wa kisera ndani ya chama hiki kinachojinasibu ni kikongwe Africa nzima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…