Rais Kikwete Ziarani Japani

Rais ana pigana kupunguza umaskini wenu halafu mnaleta midomo.Asipotoka nje hamta enda chooni nyie.
 
Ndugu RPG nadhani wewe ungekua kiongozi usingesafiri kabisa ungekaa nchini mwako tu, ukitakiwa kwenye mkutano UN, AU, Ukialikwa na nchi marafiki na mahasimu hutaenda bali kote huko utatumia technolojia ya mawasiliano (teknohama).

Nafikiri hao Maraisi kama Obama wanaokuja na takribani watu 700 kama inavyosemwa au Hu Jintao alivyokuja wakati ule na watu 400 walipaswa kutumia facebook, jamii forum, skype, twiter etc kufanya mkutano wakayamaliza.

Jamani tuache majungu, kusafiri sioni tatizo tatizo tunaposafiri tunaleta nini? Kama Rais anasafiri analeta business exchange, au wawekezaji, au kufungua masoko, au kutengeneza mazingira ya kupata misaada/mikopo yenye masharti nafuu sioni tatizo lolote, lakini kama anaenda huko kuangalia miradi yake binafsi, kujirusha, kutembelea wachumba, etc hapo ndipo penye taabu. Sijaona kati yetu wote aliyeeleza raisi amesafiri akaleta hasara au faida gani; wote tunasema anatumia mamilioni ya pesa bila sababu yoyote ni bora angekaa nyumbani, haya n=mimi nasema ni majungu ya kiwivu wa uswahilini mtu akila mayai amekwiba au kahongwa.

Tuache kudanganyana hamna raisi asiyesafiri hapa duniani wengi wanasafiri na wanasafiri sana tu. Japani wanafanya biashara nyingi sana na nchi yetu kwanini raisi asiende huko? Rais ni kiongozi SADC na ni mwenyekiti wa ulinz na usalama wa maziwa makuu kwanini asihudhurie huo mkutano? Je kama Japani wanalipia safari nzima je unapata shida gani?

Eti wengine wanasema kuna jambo litatokea maana imekua kawaida alafu kesho matokeo mapya ya kidato cha nne yakitangazwa mtasema ndicho alichokimbia jamani sisi watu sisi taabu kwelikweli.

Jana nilikua airport kumsindikiza rafikiangu akaniambia "Mh. Raisi amepanda Emirates amefika kwa kuchelewa sana, masikini Mh. ananekana very tired" alafu hapa tunazungumza umbulula.
 
Rais wa watu kwa maendeleo ya watu wake.


Rais wa Zanzibar - Dr. Shein yuko CHINA ni kwanini baada ya ZIARA yake asiende JAPAN kwa huo MKUTANO wa JAPAN na NCHI za KIAFRICA? ni MKUTANO na SIO DIPLOMATIC OFFICIAL VISIT...

Hivyo Ingesaidia na Dr. Shein anaweza kuwakilisha VIZURI amekuwa Makamu wa Rais wa MUUNGANO kwa Miaka 6; Hapo tuneweza ku-save hizo pesa za KIGENI na angalau zingetengeneza MADAWATI kwa SHULE zote BAGAMOYO
 
Tunaomba kusikia mchango wa the Fast Jet..........Yaani tunaomba kupata audio au video kuona kama kuhudhuria kwake kuna manufaaa kwa taifa
 
kiwanda kikubwa cha sement,miradi ya bara2 nk nyie mtajua lini kila siku maandamano mtaani?

Unadhani bila kuwa kiguu na njia mambo hayo yasinge fanyika. Mbaya zaidi hizo barabara zajengwa na mikopo juu wakati rasilimali ziko kibwena
 
Angemtuma mzee wa kufungua matamasha na mikutano

Jamani huyu mzee mnamwonea tu. Namwona kama mpole mno asiyependa makuu. Pengine ndo maaana bosi wake hamtumi kumwakilisha. They say he is extremely brainy. Ni kifaa hasa ila basi tu.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Yule kazi yake ni kutembea na mkasi mfukoni kwaajili ya kukata tepe, kufungua na kufunga semina na makongamano, kupokea wageni wa Boss wake anapokuwa hayupo kama yule boss wa richmond. Hizo ndizo kazi kuu za makamu wake.
Duh... Hii kali kuliko!

Unamwambia vice president,kazi yake kutembea mkasi mfukoni na kukata tepe,kwa ajili ya ufunguzi wa shughuli mbalimbali?!

Hata hivyo nakubaliana umehit kwenye ukweli ingawa mchungu!

Maana ni kweli waTZ,tunaona jinsi kodi zetu zinavyotumika vibaya,kwa kuweka nafasi kubwa ya makamo wa Rais,ambayo inaambatana na mshahara mkubwa na malupulupu kibao,ambapo kazi yake kubwa ni kukata tepe za ufunguzi wa shughuli mbalimbali,kazi ambayo ingeweza kufanywa hata na mtoto anayesoma chekechea!!
 
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo jioni anatarajiwa kuwasili nchini japani kushiriki mkutano wa tano wa maendeleo ya Afrika-TICAD V

Frequent flier status =Diamond
Mileage= 10 million plus
Hongera kwa kuwa the most frequest flier (president) in the world
Vasco Da Gama
 
Hivi wapi nitapata list ya nchi zote rais wetu alizotembelea na idadi alizotembelea hizo nchi?

Msaada tafadhali

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Una unga nyumbani badala upike wewe kwa uvivu wako wa kuwasha moto unaenda kuomba ugali kwa jirani kila siku!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom