Ndugu RPG nadhani wewe ungekua kiongozi usingesafiri kabisa ungekaa nchini mwako tu, ukitakiwa kwenye mkutano UN, AU, Ukialikwa na nchi marafiki na mahasimu hutaenda bali kote huko utatumia technolojia ya mawasiliano (teknohama).
Nafikiri hao Maraisi kama Obama wanaokuja na takribani watu 700 kama inavyosemwa au Hu Jintao alivyokuja wakati ule na watu 400 walipaswa kutumia facebook, jamii forum, skype, twiter etc kufanya mkutano wakayamaliza.
Jamani tuache majungu, kusafiri sioni tatizo tatizo tunaposafiri tunaleta nini? Kama Rais anasafiri analeta business exchange, au wawekezaji, au kufungua masoko, au kutengeneza mazingira ya kupata misaada/mikopo yenye masharti nafuu sioni tatizo lolote, lakini kama anaenda huko kuangalia miradi yake binafsi, kujirusha, kutembelea wachumba, etc hapo ndipo penye taabu. Sijaona kati yetu wote aliyeeleza raisi amesafiri akaleta hasara au faida gani; wote tunasema anatumia mamilioni ya pesa bila sababu yoyote ni bora angekaa nyumbani, haya n=mimi nasema ni majungu ya kiwivu wa uswahilini mtu akila mayai amekwiba au kahongwa.
Tuache kudanganyana hamna raisi asiyesafiri hapa duniani wengi wanasafiri na wanasafiri sana tu. Japani wanafanya biashara nyingi sana na nchi yetu kwanini raisi asiende huko? Rais ni kiongozi SADC na ni mwenyekiti wa ulinz na usalama wa maziwa makuu kwanini asihudhurie huo mkutano? Je kama Japani wanalipia safari nzima je unapata shida gani?
Eti wengine wanasema kuna jambo litatokea maana imekua kawaida alafu kesho matokeo mapya ya kidato cha nne yakitangazwa mtasema ndicho alichokimbia jamani sisi watu sisi taabu kwelikweli.
Jana nilikua airport kumsindikiza rafikiangu akaniambia "Mh. Raisi amepanda Emirates amefika kwa kuchelewa sana, masikini Mh. ananekana very tired" alafu hapa tunazungumza umbulula.