Rais Kikwete ulimwelewa Dk. Slaa?

Rais Kikwete ulimwelewa Dk. Slaa?

Hapa hakuna cha CCM wala CHADEMA, swala la madawa ya kulevya ni issue ya kitaifa.
Alichofanya JK ni kutufumbua macho wengine tujue kumbe hii issue ya kukamatwa Riz ni kweli. Lingekuwa ni uzushi wala lisingetolewa taarifa maalumu kwa vyombo vya habari. Lisemwalo lipo.
umesomeka vizuri sana mkuu!
 
Kama kweli Raisi hakutaka kujibu tuhima za mtaani, nashangaa huyu aliyewashauri watu wake wa Ikulu waanze kutoa Press Statement.
 
Wewe unaleta uchambuzi wa fasihi hapa.muelewe kikwete kasema hana muda huo wa kubishana na wapuuzi kama slaa kwa maneno ya kutungwa na yasiyo ya kwel.kikwete haimbi taarabu mzee yupo kwa ajir ya taifa sasa slaa alikuwa anatafuta kick tu akijua atatengeneza debate.ndo maana sasa kaungana na ukawa wenzake kutafuta kick tena kwa kususia bunge kumbe wananch sasahiv wameelimika na kuona hawa watu sio kabisa
 
Hao hao watu wa mtaani tunamfanya asilale...

Na kwa hilil hachomoki, mwakani ana kesi ya kujibu baada ya kuwa mbangaji wa nyumba ya watu wa mtaani

Unaelewa nini kuhusiana na neno misemo ?
 
Kauli ya Rais Kikwete kuhusu tuhuma za mwanawe na dawa za kulevya aliyoitoa akizungumza na Watanzania waishio Marekani, na ambayo watu wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu 'wamepambana' kweli kweli kuhakikisha inapata uzito unaostahili stori 'kubwa' ya rais, inafikirisha na kuibua maswali kadhaa!

Walau kwa kuanzia tunaweza kuuliza swali moja la msingi na mengine kadhaa ya nyongeza;

1. Hivi watu wa mitaani ni akina nani, walau kwa context ya Rais Kikwete, familia yake, Taasisi ya Urais, Serikali yake, CCM na taifa letu kwa ujumla?

i. Mara ngapi huwa anawapuuza watu wa mitaani ambao sisi wengine tunaamini kuwa ndiyo wananchi wake?

ii. Huko mitaani si ndiyo barabarani? Kwa hiyo anathibitisha kuwa watu ambao yeye anawathamini na anaweza kuwasikiliza ni wale ambao HUWA HAKUTANI barabarani? Ref. Hatukukutana barabarani.

iii. Makabrasha ya Serikali yake na CCM na hata kauli za mawaziri wake, watendaji wake na viongozi wake ndani ya chama zinazosema 'watoto wa mitaani'...huwa zinamaanisha ni watu wa kupuuzwa vile?

Rais anasema urais ni taasisi kubwa, kweli kabisa watu makini watakubaliana naye, lakini watauliza;

iv. Rais ameanza kujua lini kuwa taasisi ya urais ni kubwa?

v. Je aliposema taasisi ya urais ni kubwa, alimaanisha inapaswa kulinda heshima yake, kutumia mamlaka yake ipasavyo kuongoza?

Maana ukubwa wa taasisi hiyo haijawahi kuwa issue kubwa tangu aingie madarakani. Watu wa mitaani kama alivyowaita yeye, wanachohoji ni uadilifu, UWAJIBIKAJI, heshima ya taasisi hiyo, ni mamlaka ya taasisi hiyo (imewahi kusamehe wakosaji wa jinai, EPA, badala ya kufikishwa mahakamani, imeshindwa kuwashughulikia majangiri, iliahidi maisha bora kwa Watanzania na sasa inayumbisha na hata kuvuruga mchakato wa Katiba Mpya) n.k.

Lakini pia Rais Kikwete katika majibu yake bila shaka ametusaidia kufumbua fumbo aliloliweka Dk. Slaa.

Mwaka juzi Dk. Slaa alipomtaka Rais Kikwete atoe kauli juu ya tuhuma kwamba mtoto mmoja wa kigogo mkubwa serikalini alikuwa amekamatwa na dawa za kulevya huko China, taarifa za vyombo vya habari vilivyomnukuu havikutaja jina la mtoto huyo!

Majibu ya Rais Kikwete yamekwenda hatua mbele kadhaa na kutuondolea utata wa jina la aliyekamatwa na kigogo huyo ni nani!

Watu wa mitaani wataendelea kuihoji taasisi yao ya urais kwa sababu wanakumbuka maneno ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere juu ya umuhimu wa taasisi hiyo! Tumwachie Rais Kikwete kazi ya kuwapuuza watu wa mitaani. Wananchi.
kwa wewe na wenzenu msio na akili na ambao mnashindia viroba ndio mtakaomuona SLAA kuwa sio wa mtaani. ila sisi wengine tunamuona ni mjinga tu wa mtaani na ndio maana anaishia kuwa mzinzi na ana promote uzinzi hadharani. kuhusu kauli yake ya eti''mtoto wa kigogo amekamatwa china na shehena ya drugs''' hilo litaaminiwa nwa wanywa gongo kama wewe kwa sababu wakati wa uchaguzi wa 2010 alitutangazia kuwa kuna CONTAINER LA KURA BANDIA LINATAKA KUVUSHWA MPAKANI TUNDUMA-MBEYA.
wajinga mlitoa macho na kushupaa lakini wenye akili zetu tulijua ni usanii wa kijinga na ikaja ikathibitika hivyo.
kwa mwenye akili na mjuzi(sio mzushi kama wewe na babu slaa),mtandao wa wasafirishaji(punda),waagizaji,wasambazaji na watumiaji.... kwa namna yoyote hauwezi kumfanya ridhiwani(kama kweli angekuwa anafanya hiyo biashara) akawa ni msafirishaji(punda) mpaka afikie mahali pa kukamatwa. yeye ni wazi angekuwa katika rank ya waagizaji.
ila sina haja ya kuwaelewesha kwa maana ujinga upo deep within you na ndio maana tunawadharau,tunawapuuza, na tuko dodoma tunawatungia katiba ambayo itawainamisha for the next 50 years
 
Kwani kunamtu amabye anamsikiliza dr slaa mtu ambaye hata familia ilishamshinda kuendesha.
 
Kweli kabisa Mkuu. Wanajidanganya sana hawa

Ngoja Lowassa aingie Ikulu hamna rangi mtaacha kuona! Mnadandia msiyoyajua cyo, Na huyo mtuhumiwa si ndo anampiga vita kwa nguvu sake zote? Atapanga nani awe waziri lkn la urais lipo nje yake.
 
Wewe unaleta uchambuzi wa fasihi hapa.muelewe kikwete kasema hana muda huo wa kubishana na wapuuzi kama slaa kwa maneno ya kutungwa na yasiyo ya kwel.kikwete haimbi taarabu mzee yupo kwa ajir ya taifa sasa slaa alikuwa anatafuta kick tu akijua atatengeneza debate.ndo maana sasa kaungana na ukawa wenzake kutafuta kick tena kwa kususia bunge kumbe wananch sasahiv wameelimika na kuona hawa watu sio kabisa

Mbona kabishana sasa?
 
Anatufanananisha na Kitaleee, ngoja naye hatoke hapo kunako samaki tuone ataenda wapi? au naye ataenda rushoto!!
 
nimeshangazwa na maelezo ya dr.dr.dr jakaya mrisho kikwete, kwani wakati wa kampeni alisema , naomba ninukuu.."Urais ni wa kwake na familia yake" sasa ni lini alifahamu kuwa Urais ni taasisi? au anafikiri hatukumsikia na kumuelewa? kweli rais wetu ni mwepesi kuongea na rahisi kusahau alichoongea.
 
JK ni mtu asiyejitambua hivyo msipate shida na huyo mtu
 
Rais hawezi kujibu mkusanyika wa mawazo ya kipuuzi rais ana mambo mengi ya kuwatumikia wananchi wake, hayo anawachia nyie na Dr.Slaa.

Majibu kama ya JK.... kukana ndo kawaida mliyoizowea....
unakumbuka LOLIONDO KUUZWA? UNAKUMBUKA ZANZIBAR KUJIUNGA NA OIC?
 
Rais hawezi kujibu mkusanyika wa mawazo ya kipuuzi rais ana mambo mengi ya kuwatumikia wananchi wake, hayo anawachia nyie na Dr.Slaa.
Ritz,
Mbona alijibu alipokuwa DC ingawa alikwepa swali? Si angenyamaza tu kama ana mambo mengi ya kuwatumikia wananchi?
By not answering he has answered a lot. We now believe he went to China to save his son Ridhiwani.
 
Back
Top Bottom