Rais Kikwete ulimwelewa Dk. Slaa?

Rais Kikwete ulimwelewa Dk. Slaa?

Tumaini Makene

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2012
Posts
2,650
Reaction score
6,088
Kauli ya Rais Kikwete kuhusu tuhuma za mwanawe na dawa za kulevya aliyoitoa akizungumza na Watanzania waishio Marekani, na ambayo watu wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu 'wamepambana' kweli kweli kuhakikisha inapata uzito unaostahili stori 'kubwa' ya rais, inafikirisha na kuibua maswali kadhaa!

Walau kwa kuanzia tunaweza kuuliza swali moja la msingi na mengine kadhaa ya nyongeza;

1. Hivi watu wa mitaani ni akina nani, walau kwa context ya Rais Kikwete, familia yake, Taasisi ya Urais, Serikali yake, CCM na taifa letu kwa ujumla?

i. Mara ngapi huwa anawapuuza watu wa mitaani ambao sisi wengine tunaamini kuwa ndiyo wananchi wake?

ii. Huko mitaani si ndiyo barabarani? Kwa hiyo anathibitisha kuwa watu ambao yeye anawathamini na anaweza kuwasikiliza ni wale ambao HUWA HAKUTANI barabarani? Ref. Hatukukutana barabarani.

iii. Makabrasha ya Serikali yake na CCM na hata kauli za mawaziri wake, watendaji wake na viongozi wake ndani ya chama zinazosema 'watoto wa mitaani'...huwa zinamaanisha ni watu wa kupuuzwa vile?

Rais anasema urais ni taasisi kubwa, kweli kabisa watu makini watakubaliana naye, lakini watauliza;

iv. Rais ameanza kujua lini kuwa taasisi ya urais ni kubwa?

v. Je aliposema taasisi ya urais ni kubwa, alimaanisha inapaswa kulinda heshima yake, kutumia mamlaka yake ipasavyo kuongoza?

Maana ukubwa wa taasisi hiyo haijawahi kuwa issue kubwa tangu aingie madarakani. Watu wa mitaani kama alivyowaita yeye, wanachohoji ni uadilifu, UWAJIBIKAJI, heshima ya taasisi hiyo, ni mamlaka ya taasisi hiyo (imewahi kusamehe wakosaji wa jinai, EPA, badala ya kufikishwa mahakamani, imeshindwa kuwashughulikia majangiri, iliahidi maisha bora kwa Watanzania na sasa inayumbisha na hata kuvuruga mchakato wa Katiba Mpya) n.k.

Lakini pia Rais Kikwete katika majibu yake bila shaka ametusaidia kufumbua fumbo aliloliweka Dk. Slaa.

Mwaka juzi Dk. Slaa alipomtaka Rais Kikwete atoe kauli juu ya tuhuma kwamba mtoto mmoja wa kigogo mkubwa serikalini alikuwa amekamatwa na dawa za kulevya huko China, taarifa za vyombo vya habari vilivyomnukuu havikutaja jina la mtoto huyo!

Majibu ya Rais Kikwete yamekwenda hatua mbele kadhaa na kutuondolea utata wa jina la aliyekamatwa na kigogo huyo ni nani!

Watu wa mitaani wataendelea kuihoji taasisi yao ya urais kwa sababu wanakumbuka maneno ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere juu ya umuhimu wa taasisi hiyo! Tumwachie Rais Kikwete kazi ya kuwapuuza watu wa mitaani. Wananchi.
 
leta updates za presconference yenu uliyotujuza hapa mitandaoni usitugeuze wala viroba kama wewe na babu yako.
 
Mimi sikuwahi kuamini kwamba huyu mgeni kutoka Msoga alifanya kitu cha namna hii, nilichukulia ni bahati mbaya tu kutokana na mikosi yake watu kudhania kwamba alifanya kitu cha namna hiyo.

Lakini kutokana na majibu yake, sasa naamini kwamba yeye na mtoto wake walifanya kitu cha namna hii, uchafu hauwezi kukuangukia alafu uupuze badala ya kujisafisha, anaogopa akijisafisha atajichuna na ngozi.
 
Bila shaka Makene umekurupuka. Dr Kikwete alijibu kwa mujibu wa swali aliloulizwa. Mtahangaika sana na JK lakini ndo hivyo siku zinayoyoma
 
Ccm nikichaka cha maovu,yahitaji akiri yawendawazimu kupindua ukweli huo maana ushahidi kila mtanzania mwenye akili timamu anao
 
Hapa hakuna cha CCM wala CHADEMA, swala la madawa ya kulevya ni issue ya kitaifa.
Alichofanya JK ni kutufumbua macho wengine tujue kumbe hii issue ya kukamatwa Riz ni kweli. Lingekuwa ni uzushi wala lisingetolewa taarifa maalumu kwa vyombo vya habari. Lisemwalo lipo.
 
Kauli ya Rais Kikwete kuhusu tuhuma za mwanawe na dawa za kulevya aliyoitoa akizungumza na Watanzania waishio Marekani, na ambayo watu wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu 'wamepambana' kweli kweli kuhakikisha inapata uzito unaostahili stori 'kubwa' ya rais, inafikirisha na kuibua maswali kadhaa!

Walau kwa kuanzia tunaweza kuuliza swali moja la msingi na mengine kadhaa ya nyongeza;

1. Hivi watu wa mitaani ni akina nani, walau kwa context ya Rais Kikwete, familia yake, Taasisi ya Urais, Serikali yake, CCM na taifa letu kwa ujumla?

i. Mara ngapi huwa anawapuuza watu wa mitaani ambao sisi wengine tunaamini kuwa ndiyo wananchi wake?

ii. Huko mitaani si ndiyo barabarani? Kwa hiyo anathibitisha kuwa watu ambao yeye anawathamini na anaweza kuwasikiliza ni wale ambao HUWA HAKUTANI barabarani? Ref. Hatukukutana barabarani.

iii. Makabrasha ya Serikali yake na CCM na hata kauli za mawaziri wake, watendaji wake na viongozi wake ndani ya chama zinazosema 'watoto wa mitaani'...huwa zinamaanisha ni watu wa kupuuzwa vile?

Rais anasema urais ni taasisi kubwa, kweli kabisa watu makini watakubaliana naye, lakini watauliza;

iv. Rais ameanza kujua lini kuwa taasisi ya urais ni kubwa?

v. Je aliposema taasisi ya urais ni kubwa, alimaanisha inapaswa kulinda heshima yake, kutumia mamlaka yake ipasavyo kuongoza?

Maana ukubwa wa taasisi hiyo haijawahi kuwa issue kubwa tangu aingie madarakani. Watu wa mitaani kama alivyowaita yeye, wanachohoji ni uadilifu, UWAJIBIKAJI, heshima ya taasisi hiyo, ni mamlaka ya taasisi hiyo (imewahi kusamehe wakosaji wa jinai, EPA, badala ya kufikishwa mahakamani, imeshindwa kuwashughulikia majangiri, iliahidi maisha bora kwa Watanzania na sasa inayumbisha na hata kuvuruga mchakato wa Katiba Mpya) n.k.

Lakini pia Rais Kikwete katika majibu yake bila shaka ametusaidia kufumbua fumbo aliloliweka Dk. Slaa.

Mwaka juzi Dk. Slaa alipomtaka Rais Kikwete atoe kauli juu ya tuhuma kwamba mtoto mmoja wa kigogo mkubwa serikalini alikuwa amekamatwa na dawa za kulevya huko China, taarifa za vyombo vya habari vilivyomnukuu havikutaja jina la mtoto huyo!

Majibu ya Rais Kikwete yamekwenda hatua mbele kadhaa na kutuondolea utata wa jina la aliyekamatwa na kigogo huyo ni nani!

Watu wa mitaani wataendelea kuihoji taasisi yao ya urais kwa sababu wanakumbuka maneno ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere juu ya umuhimu wa taasisi hiyo! Tumwachie Rais Kikwete kazi ya kuwapuuza watu wa mitaani. Wananchi.
Rais hawezi kujibu mkusanyika wa mawazo ya kipuuzi rais ana mambo mengi ya kuwatumikia wananchi wake, hayo anawachia nyie na Dr.Slaa.
 
Hao hao watu wa mtaani tunamfanya asilale...

Na kwa hilil hachomoki, mwakani ana kesi ya kujibu baada ya kuwa mbangaji wa nyumba ya watu wa mtaani
 
Back
Top Bottom