Rais Kikwete sio kigeugeu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete sio kigeugeu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SIR_KIMANYO, Aug 26, 2011.

 1. S

  SIR_KIMANYO Member

  #1
  Aug 26, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [FONT=Century Gothic, sans-serif]UNITEDREPUBLIC OF TANZANIA[/FONT]
  [FONT=Century Gothic, sans-serif]DIRECTORATEOF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS[/FONT]


  [TABLE]
  [TR]
  [TD="width: 239"] [FONT=Book Antiqua, serif]Telephone: 255-22-2114512, 2116898 [/FONT]
  [FONT=Book Antiqua, serif]E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com[/FONT]
  [FONT=Book Antiqua, serif]press@ikulu.go.tz [/FONT]
  [h=4]Fax: 255-22-2113425[/h]

  [/TD]
  [TD="width: 104"]

  [/TD]
  [TD="width: 252"] PRESIDENT’S OFFICE,
  THE STATE HOUSE,
  P.O. BOX 9120,
  DAR ES SALAAM.
  Tanzania.
  [h=5][/h] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  [FONT=Palatino Linotype, serif]TAARIFAYA UFAFANUZI[/FONT]
  [FONT=Palatino Linotype, serif]Tarehe 21 Julai,mwaka huu, 2011, Katibu Mkuu Kiongozi Bwana Phillemon Luhanjo,akitumia madaraka yake ya Mamlaka ya Nidhamu ya Watumishi wa Umma,alitangaza hatua ya kumpa likizo ya malipo Katibu Mkuu wa Wizara yaNishatai na Madini, Bwana David Kitundu Jairo, ili kupisha uchunguzialiokuwa ameuagiza ufanyike dhidi yake. [/FONT]
  [FONT=Palatino Linotype, serif]Bwana Luhanjoalichukua hatua ya kumsimamisha Bw. Jairo kufuatia tuhuma zilizokuwazimeelekezwa dhidi yake na baadhi ya wabunge wakati wa mjadala kuhusuMakadirio na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka2011/12 katika kikao cha Bunge kilichofanyika tarehe 18 Julai, 2011. [/FONT]
  [FONT=Palatino Linotype, serif]Katika mjadalahuo, baadhi ya wabunge walihoji uhalali wa Wizara kuomba michango yafedha kutoka kwenye Taasisi zilizoko chini ya usimamizi wake ilikusaidia Bajeti ya Wizara hiyo kupita kwa urahisi.[/FONT]  [FONT=Palatino Linotype, serif]Kufuatia hatuahiyo ya kumsimamisha kazi Bw. Jairo, Katibu Mkuu Kiongozi alimwombaMdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bwana LudovickUtouh kufanya ukaguzi maalum na uchunguzi wa awali juu ya tuhumahizo.[/FONT]
  [FONT=Palatino Linotype, serif]Tarehe 9 Agosti,mwaka huu, 2011, Bw. Utouh aliwasilisha Ripoti yake kwa Katibu MkuuKiongozi, na tarehe 23, Agosti, 2011, Katibu Mkuu Kiongoziakiambatana na Bw. Utouh alitangaza mbele ya waandishi wa habarimatokeo ya ukaguzi huo maalum na uchunguzi wa awali juu ya tuhumadhidi ya Bw. Jairo. [/FONT]
  [FONT=Palatino Linotype, serif]Katika Ripoti yakembele ya waandishi wa habari, Bw. Utouh alihitimisha:[/FONT][FONT=Palatino Linotype, serif]“Ukaguzi maalum haukuthibitisha kuwepo kwa usahihi wa tuhumazilizotolewa dhidi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw.David Kitundu Jairo.”[/FONT]
  [FONT=Palatino Linotype, serif]Kufuatia Ripotihiyo ya Bw. Utouh, Katibu Mkuu Kiongozi naye aliwaambia waandishi wahabari: [/FONT][FONT=Palatino Linotype, serif]“Matokeoya uchunguzi huo ni kwamba tuhuma zilizotolewa Bungeni tarehe 18Julai, 2011, hazikuweza kuthibitika. Kutokana na matokeo haya yauchunguzi wa awali, mimi kama Mamlaka ya Nidhamu ya Katibu Mkuu,Nishati na Madini, Bwana David Kitundu Jairo, sitaweza kuendelea nahatua ya pili ya kumpa taarifa ya tuhuma (notice) na Hati yaMashitaka kwa sababu Bwana David Kitundu Jairo, hajapatikana na kosala kinidhamu (disciplinary offence) kwa mujibu wa Taarifa ya UkaguziMaalum.”[/FONT]
  [FONT=Palatino Linotype, serif] Alihitimisha:“[/FONT][FONT=Palatino Linotype, serif]Kufuatiamatokeo ya taarifa hii ya awali na kwa mamlaka niliyonayo kwa mujibuwa Sheria Na. 8 ya Utumishi Umma ya Mwaka 2002 na kanuni zake zaMwaka 2003, NINAAMURU BWANA DAVID KITUNDU JAIRO AREJEE KAZINI KUANZIASIKU YA JUMATANO, TAREHE 24 AGOSTI, 2011.” [/FONT]
  [FONT=Palatino Linotype, serif]KURUGENZI YAMAWASILIANO YA RAIS, IKULU,[/FONT][FONT=Palatino Linotype, serif]inapenda kutoa ufafanuzi kuwa baada ya kupokea taarifa ya uchunguziya CAG na uamuzi wa Katibu Mkuu Kiongozi kuhusu suala hilo asubuhi yatarehe 25 Agosti, 2011, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliamua kuwa Ndugu Jairo asirudikazini mpaka kwanza yeye Rais atapoamua namna gani ya kurudi kazini,lini na wapi.[/FONT]
  [FONT=Palatino Linotype, serif]Katibu MkuuKiongozi alifikisha uamuzi huo wa Rais kwa Ndugu David Jairo ambayemapema asubuhi ya siku hiyo alikuwa ameripoti kazini. Ndugu Jairoalitii uamuzi huo wa Rais. [/FONT]
  [FONT=Palatino Linotype, serif]Tunapendakusisitiza kuwa Mheshimiwa Rais hawaja kigeugeu kwa sababu alifanyauamuzi mmoja tu baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Katibu MkuuKiongozi. Na uamuzi huo aliufanya kabla ya Bunge kulizungumzia sualahilo na hivyo uamuzi huo wa Rais haukutokana na shinikizo la Bunge.Pamoja na kumweleza Katibu Mkuu Kiongozi, Rais pia alimfahamishaWaziri Mkuu kuhusu uamuzi wake huo asubuhi hiyo ya tarehe 25, 2011.[/FONT]
  [FONT=Palatino Linotype, serif]Aidha, tunapendakufafanua zaidi kwamba Katibu Mkuu Kiongozi ametimiza wajibu wakeipasavyo kama Mamlaka ya Nidhamu kwa Katibu Mkuu kwa mujibu waSheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma. Mheshimiwa Rais, kwaupande wake, ametumia madaraka yake kama Mamlaka ya Ajira ya KatibuMkuu. Hakuna suala la kujichanganya wala ukigeugeu ndani ya Serikalikuhusu suala hili.[/FONT]
  [FONT=Palatino Linotype, serif]Mwisho.[/FONT]
  [FONT=Palatino Linotype, serif]Imetolewana Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,[/FONT]
  [FONT=Palatino Linotype, serif]Ikulu[/FONT][FONT=Palatino Linotype, serif],[/FONT]
  [FONT=Palatino Linotype, serif]Dares Salaam[/FONT][FONT=Palatino Linotype, serif].[/FONT]
  [FONT=Palatino Linotype, serif]26Agosti, 2011[/FONT]
   
 2. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Salva utamtetea sana raisi kikwete lakini katika hili mkuu ameshinikizwa na azimio la bunge.
   
 3. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa siyo kigeugeu. Ni mtu makini na mahiri katika maamuzi ambayo labda yangeiweka nchi katika hali mbaya sana.
   
 4. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  sio kigeugeu bali ni lege lege
   
 5. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Ni uamuzi mzuri kwa wakati wa sasa.
   
 6. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Salva, unatumia taaluma yako vibaya kwa kutoa taarifa potofu. Hivi nani mkubwa kimadaraka kati ya Waziri Mkuu na Katibu Mkuu Kiongozi? Tunakumbuka maneno aliyosema Waziri Mkuu ni nini angefanya kama angekuwa na mamlaka ya kutoa maamuzi juu ya kashfa ya Jairo, mwenye mamlaka hayo (si Katibu Mkuu Kiongozi) alikuwa nje ya nchi wakati huo aliahidi kumpigia simu baadae. Na simu ilipopigwa tukaambiwa kuna maelekezo (kutoka kwa rais) mengine kuhusu Jairo - ndo KMKiongozi akaibuka na maelekezo ya Cag kufanya uchunguzi.
  Kakangu Salva huo mchezo wa kuigiza wa kitoto unaofanywa na hao unaowakurugenzia habari kwani ripoti imemtakasa Jairo kwamba hakutoa mlungula. Hivi hizo pesa zilitoka ktk bajeti ipi? Hizo pesa ni nyingi kutolewa kama hongo huku wanchi wakitaabika sana.
  Nasikia Jairo siku aliporipti kazini alipokelewa kama shujaa hadi gari lake kusukumwa, mwambie rais jambo hilo lilituudhi sana.
  Rais huyo huyo kaamuru Jairo arudi likizo kupisha uchunguzi wa tume ya bunge! KAMA SI UKIGEUGEU NI NINI?
  Itafika siku hata kuhutubia watakuwa wanakuja watoto tu.
   
 7. Chromium

  Chromium JF-Expert Member

  #7
  Aug 26, 2011
  Joined: Apr 17, 2008
  Messages: 598
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35

  Wewe lazima utakuwa Ridhiwani
   
 8. Prof Gamba

  Prof Gamba JF-Expert Member

  #8
  Aug 26, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 390
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Si kigeugeu bali ni mwoga zaidi ya kungulu na ni legelege.
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  Aug 26, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Huyo aliyetoa hii Press Release mbona hakusema chochote wakati wa mgomo wa mafuta? Where was he?
   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  Aug 26, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  marekani anaenda lini maana ni nuksi aondoke zake akatalii na siku 30 zina hesabika bengaz itakuwa Arusha...
   
 11. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #11
  Aug 26, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Sina uhakika kama Mh Raisi amesoma barua hii kabla ya kwenda hewani... hainiingilii akilini kuwa imeandikwa na Ikulu, maana ina mapungufu mengi sana ni aibu kwa kweli hata ujumbe uliokusudiwa umekaa vibaya sana naasikitika
   
 12. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #12
  Aug 26, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kulikuwa na ulazima kwa hii threat kupostiwa hapa!??
  Naogopa tu kutukana hapa Mods ataniban
   
 13. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #13
  Aug 26, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  anapulizia pafyumu...
   
 14. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #14
  Aug 26, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,079
  Likes Received: 877
  Trophy Points: 280
  I smell ban kudadadadeki...
   
 15. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #15
  Aug 26, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,831
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 280
  Mi naona bado wanazidi kujichanganya na kujidhalilisha mbele ya umma....Bungeni Pinda alitamka kuwa laiti angekuwa na mamlaka angechukua uamuzi wa kumwadhibu Jairo mara moja,na aliahidi atamfahamisha rais kwani ndiye mwenye mamlaka.Sasa ikiwa Rais amefanya uamuzi mmoja tu kusitisha agizo la Luhanjo kwa Jairo kurejea kazini ,je ni nani aliyemwagiza Luhanjo kumpa likizo Jairo na kumtaka CAG kufanya uchunguzi?Je ni hatua/uamuzi gani aliyochukua Rais baada ya kujulishwa jambo hili na Pinda?Kama hakuwahi kuchukua hatua zozote awali,ni kipi kimemsukuma sasa?
   
 16. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #16
  Aug 26, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Hapo ndipo ukigeu geu unapoanzia.
  Kwa nini huu uamuzi tunaoambiwa "aliamua kuwa Ndugu Jairo asirudi kazini mpaka kwanza yeye Rais atapoamua namna gani ya kurudi kazini,lini na wapi." hatukuisikia kabla hadi kelele za kina Zitto zilipoungwa mkono?? Je rais anataka kucheza sinema ya "Super Hero???"
  Taarifa inaleta maswali zaidi kuliko majibu.
  Rais alisema nini baada ya kupewa taarifa na Pinda tar 18/08???
  Luhanjo alitumwa na nani kufanya uchunguzi??
  Kama Luhanjo hakutumwa ni vipi kajiamria jambo wakati Pinda alishasema anawasiliana na rais kuhusu Jairo??
  Tukiamua kuchukua taarifa ya Salva kuwa ya kweli, haoni anamchafua rais kwamba ni legelege maana iweje jambo la mwezi Agosti 18 alifanyie kazi mwezi mmoja baadae???

  Kimsingi taarifa inaudhi zaidi na namwomba PAW awavumilie wachangiaji iwapo wataonyesha hasira zao!
   
 17. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #17
  Aug 26, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,831
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  Umenena vema sana mkuu.
   
 18. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #18
  Aug 26, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,031
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 133
  Hii kitu iko mbofumbofu hakuna jinsi ya kuelezea![​IMG]
   
 19. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #19
  Aug 26, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Wewe ambae si legelege mbona huna hata ujumbe wa nyumba kumi? unanchekesha.
   
 20. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #20
  Aug 26, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  ban hiyoooooooo inanukia
   
Loading...