Hivi ni kwanini mnapenda kuwafanya watanzania kuwa ni wapumbavu kwa kiwango hicho?
Rais alimuagiza Katibu Mkuu Kiongozi kulifanyia uchunguzi suala la katibu mkuu wa wizara ya madini, ni dhahiri baada ya uchunguzi alitakiwa airudishe kwa mheshimiwa rais kabla ya kutolewa hewani?
Je kwa mchezo uliochezeka hapa tuamini kuwa rais siye anaefanya maamuzi pale ikulu? je tuamini kuwa pale ikulu tuna zaidi ya rais mmoja, je tuamini kuwa hata Ikulu sasa wanampuuza rais?
Kama hivyo sivyo basi ukweli ni kuwa Katibu Mkuu kiongoz asingejikurupukia kupeleka kwenye vyombo vya habari report jambo ambalo hata waziri mkuu alizuiwa kulichukulia hatua yoyote. Rais ni lazima alionyeshwa hii taarifa wakaijadili na kuafikiana kuwa sasa ni sahihi kuitoa kwenye public,, na hapo ndipo ukigeu-geu linapoibuka, na bahati nzuri katikajambo hili taarifa ya Ikulu ndiyo imekuwa ya kwanza kutumia hili neno'kigeu-geu'.
Ili taarifa ya ikulu iweze ku-make sense ilitakiwa iwe na tamko la kumsimamisha kazi au kumfukuza kazi Katibu mkuu kiongozi kwa ku-play behind the presidnet's back na kutoa taarifa kinyume na utaratibu na hivyo kuhatarisha usalama wa taifa....bila ya hivyo hali ya ukigeu geu inabaki