Rais Kikwete safarini Marekani

Rais Kikwete safarini Marekani

Watu kama wewe ndo mnaliweka taifa letu nyuma. Yaani wewe unaamini huyu mtu akisafiri kuna hela inaletwa ndani ya nchi? Kama wewe ni mzee, basi unasema hivyo kwa sababu ya uzee. Kama kijana, basi unaumwa na unastahili marafiki wa kukuchallenge na uwasikie kwa sababu una upungufu wa mawazo usio wa kawaida.

Ngoja tuojiane hapa. Juzi tu tulikuwa na sherehe za uhuru wa taifa letu uwanja wa taifa. JK alikuwepo peke yake (hapa naongelea viongozi wa nchi zilizotuzunguka). Hakuna aliyekuja. Ila baada ya hapo, Kenya wakafanya sherehe kama hiyo. Nakwambia JK aliwahi ile sherehe. Sasa nambie, huo ni urafiki gani? Yaani wewe unatembelea watu wasiokutembelea?

OK, turudi kwenye point yako kwamba akisafiri kuna pesa inaingia kwenye taifa letu. Kama kusafiri ni njia ya maendelea, tuangalie viongozi waliotuzunguka, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Congo. Au tafuta kiongozi yeyote Afrika. Akikosa tafuta duniani kote kiongozi anayesafiri kama JK. Si unatwambia kusafiri ni maendeleo? Kwa nini viongozi wote hawa wasiige mifano ya JK hili kuletea mataifa yao maendeleo?

Haya ni matumizi mabaya ya madaraka. Ni kutojari wananchi na kutumia dhamana aliyopewa kiongozi vibaya.

Tufanyeje?

Inabidi Katiba inayokuja ikemee tabia za namna hii. Safari zipangiwe badget. Ikiisha, basi. Tusipofanya hivyo, basi huu ni ufisadi mzuri na uliohararishwa. Yaani kiongozi anaweza kuwa tajiri wa maisha kwa safari tu kwa sababu analipwa posho, kwa JK itakuwa haipungui dollar 5000 kwa siku. Akipiga siku tatu ni dollar 15000 (mil.24). Hii ndo inamfanya anyatie safari kama Simba anavyomnyatia Swala. Yaani aende South Africa mara ya kwanza, arudi tena within a week, aende Kenya, then aende America.......who knows what next. Hizo elfu 5000 hazijumuishi maradhi na chakula na kina Michuzi na Camera zao.

Mwisho, tunahitaji viongozi waadirifu. Hawa hawatoki CCM hata wakija kwa style gani. Tunahitaji kuwa wapenzi wa taifa letu. Mataifa anayokimbilia kutembelea huyu JK, wao wanaheshimu misingi na maisha ya watu. Ndo maana hachoki kutembelea hayo mataifa.

Tujifunze kuwa wapenzi wa taifa letu. Tuache kuongwa kofia na kanga tukauza utu wetu. Mimi binafsi nikipewa nichague kati ya mtu anayeiba meno ya tembo na kubeba wanyama kwenye ndege (majangiri) na mtu anayesafiri kila siku na kulipwa mamillion akiwa safarini, bado mshahara wake, ntachagua yule anayeua Tembo. Wote wanafanya maovu kwa taifa lakini wa Tembo anaiba kidogo ukilinganisha na msafiri (wenye ubongo wamenielewa).

Inabidi lianzishwe somo la ethics mashuleni. Watoto wajifunze kwamba kuiba ni kubaya. Akiingia kiongozi mwingine, kigezo kimojawapo kiwe kuweka wazi gharama alizotumia JK safarini. Nakuhakikishia watu wakijua, atakuwa the most hated guy nchini mwetu.

Then, we need rule of law. Sheria ifanye kazi yake. Pasiwepo mtu aliyeko juu au chini ya sheria. Sheria mbovu ndo zinafanya mambo yanayoendelea nchini. Mpaka leo hakuna mtu wa kuuliza safari zinalipwa na nani? Zina tija gani na nchi yetu. Inabidi watu waende jela kwanza ndo tutajifunza discipline.

Watanzania tujue kuwa kupiga kura ni homework na si mchezo. Hii ni sawa sawa na kupanda mazao. Ukipanda mahindi, utavuna mahindi. Ukipanda maharagwe, utavuna maharagwe. Ukipanda magamba, utavuna magamba. Siamini kama hiki chama kinaweza kutoa mtu akalikomboa taifa letu. Mfumo wa wizi wao ni kujuana. Niwape mfano mmoja. JK anachagua mawaziri. Baadae anajua kwamba baadhi yao si watendaji wazuri, badala ya kuwafukuza, anahitisha kikao hili kujadili. Kumbuka hicho kikao watu wanakaa na kulipwa tena pesa ya walala hoi. Huu ni udhaifu na ni uzembe.

Mfano mwingine, mnakumbuka kuvua magamba? Magamba ni neno tu linalosimama badala ya wizi, utoa rushwa, ugawaji rushwa, mauaji nk. Sasa nani kavua gamba?

Hiyo mifano inatosha sasa kuonesha kuwa hawa watu sio tu hawako serious na taifa letu bali hawalipendi taifa letu. Tuwekeze sasa kwa mtu ambaye atakuwa si rafiki yao. Akiingia tu rafiki yao, basi tutakuwa ni watu wa kulalamika na kuishia mitandaoni.

Habari njema tulionayo ni kwamba, wao wanaweza kutuibia, kutuma polisi wakatuwekea vyuma sehemu za siri, wakatutesa, wakatupiga, wakaua watoto wetu ila kuna kitu hawawezi kutunyanganya, HAKI YA KUPIGA KURA. Tumia vema nafasi hii mtanzania. bado tunao muda wa kuwaondoa hawa wezi.

Nawasilisha.



!
!
sasa baba na hizi sarakasi za tume kweli tutafika kwa kupiga kura?
sio kwamba tunahitaji vijana msituni kupambana?
 
Kumbe hakuna mawaziri mizigo wanaohubiriwa na Kinana na Nape. Rais ndie mzigo. Wiki iliyopita alienda Uganda, Ufaransa, Dubai, South Africa, Kenya, South Africa, Dubai,USA...Huyo lazima awe rubani msaidizi. Hata kama waziri mkuu hasimamii vizuri mawaziri rais atajua saa ngapi wakati mda wote yuko juu angani kama kizibo cha soda.
 
Tabia aliyonayo baba yako si Tabia yetu sote.

Tangu niishi na Dr miaka Sita sasa sijawahi kumpeleka hospitali nje ya nchi kwa Maradhi yoyote,kwa hili namtukuza Mungu anayemtunza Na maombi ya watanzania wengi yanampa Afya njema.

Kwa taarifa yako,Afya Zetu ni imara Sana maana Yupo aliyebeba magonjwa yetu toka mwanzo.
Mara ya mwisho Dr kwenda hospitali ni Muhimbili alipofanyiwa operation ya mkono.

Naomba mtangaze uwongo wote lakini si juu ya Afya Zetu.

Narudia tena,magonjwa yetu yote yalizikwa Kalvari.

Amen mamá
 
Kikwete alipokutana na President Barack Obama kwenye mazishi ya Mandela ilikuwa hivi:

Barack: Watoto wangu Malia na Shasha wanapata kipaimara wakati wa x-mas karibu kwenye Party

Kikwete:Nashukuru sana kwa mwaliko huo nitakuja na Mama Salma kadi nitumie kwa e-mail

Barack: hakuna tatizo ila na wewe kwa kusafiri upo juu sasa unatumia hela ya serikali au binafsi?

Kikwete: Ha ha ha ha ni hela za watz tu hizi, hii ni Bongo.
 
Wakati huu wa kukaribia X-mas dunia nzima inaingia wakati wa kipindi cha mapumziko na sherehe nyingi za hapa na pale.
Katika kipindi hiki ofisi nyingi zinafungwa au kubakiza wale wafanyakazi wa emergency tu.
Tanzania nayo haina tofauti ,mabasi ya kwenda mikoani ndo hayakamatiki kwa nauli kupanda, alimradi mtu asherekee X-mas na wapendwa wake.
Kwa wale walioko majuu wanafahamu jinsi muda huo unapokuwa mtihani mgumu sana kutokana na baridi na watu wengi wakiwa wamejifungia majumbani kwao na familia zao.

Hivyo basi tunazipokea kwa huzuni kidogo kwa rais wetu kuugulia mbali na nyumbani, tena sehemu ambaxo baridi ni kali kwaa kipindi .
Tunachoweza kufanya ni kumpa pole tu maana kwa wafuatiliaji wa shughuli za rais,amekuwa extra busy kipindi hiki.
Kwa waratibu wa safari za JK panahitaji uangalifu kidogo hasa baada ya safari za Afrika Kusini mara mbili,Kenya na hatta hapa nchini.

Tunasoma vyombo vya habari kuwa katika moja ya safari za rais, amekoswakoswa na treni liendalo bara hapa jijini!
Daktari wake rais anashauriwa kumlazimisha rais wakati mwingine apunguze safsri zake ili asilazimike kuangaliwa au kutibiwa wakati wa mapumziko.
 
huyu mbona ni mgonjwa tokahata hajagombea urais...kama isingekuwa urais tungeshakula ubwabwa zamaniiiii
 
Msingi wa hoja yangu ni hiki tulichokisikia juzi na habari ya Mh. Rais kwenda kuangalia afya nchini Marekani na atakaa huko kwa muda wa siku 4. Je ni kweli kwamba hapa Tanzania hatuna madaktari wa kupima afya ya mtu na wakatoa majibu. Ningekubaliana bila wasiwasi kama tungeambiwa Mh. Rais amenda kutibiwa hilo hakuna mtu ambaye angeweza kupinga.
Kama kweli hatuna madaktari nchini wa kutupima na kutoa majibu juu ya afya zetu basi afya za watanzania ziko hatarini kabisa.
Naomba kwa wale watakao changia hoja hii tusiongee yale maneno mengine ya kuudhi au kudharirisha nafasi ya Mh. Rais wetu ila tujadili kwa kuangalia uhalali wa safari za viongozi wetu wakuu kupenda kwenda nje ya nchi kuangalia afya wakati haya yangeweza kufanyika hapa hapa nchini na kama viongozi wetu wakuu wanaamini kuwa madaktari wetu waliopo nchini hawana uwezo angalau wa kumpima mtu na kujua ana tatizo gani basi ipo haja kubwa ya kuboresha vifaa katika hospitali zetu

Kwa hili la Mh. Rais kwenda kupimwa afya nje ya nchi kwa kuhofu kuwa hapa nchini hakuna huduma hiyo nashawishika kuamini kwa asilimia mia moja kuwa mgomo na madai ya madaktari ulikuwa sahihi kabisa

Nawasilisha
 
Unajiringanisha na Rais? mwisho utasema kwa nini Rais akae Ikulu.
 
Tulikosea sana kumchagua huyu baba. kila siku kiguu na njia!!!
kwa kweli tuna kila sababu ya kuichukia ccm.
Haya mwigulu haujachunguza mrembo gani safari hii katangulizwa kwenye safari? Sijawahi katika maisha yote tangu uhuru kuona rais anayekata anga kwa sampuli hii. Tunaposema tunaambiwa tunaona wivu! Lakini hizi ni fedha zetu tunazokatwa kodi bila kupenda!
 
Back
Top Bottom