Umeongea kwa machungu sana hadi umeniliza
Usilie ila chukua hatua. Hatuwezi kuwa taifa la mazezeta, yaani mashabiki wa wezi na ujinga. Tunashabikia hata watu wanaokula taifa letu mchana kweupe?
Kama huamini ona watu wanavyo comment humu. Wote wametegwa na mtego mmoja tu, "..kaenda kutibiwa." Miaka nane ilopita tulidanganywa na vijimaneno "nguvu mpywa na kasi mpya." Sasa leo, "...kaenda kutibiwa" as if sio mtu huyo huyo aliyetimiza safari 392. Napenda kuwapa challenge moja wale wote wanaoamini kuwa kaenda kutibiwa, hizo safari 391, alikuwa anaenda kutibiwa?
Watanzania amkeni na teteeni taifa letu. Tunaibiwa kweupe!!! mtu mmoja humu kaja na hesabu za safari. Wengine wakambeza. Hivi kama Ikulu haiweki gharama za hizi safari wazi, inaficha nini, uovu? kama hizo gharama zingekuwa nzuri tungeambiwa tu. Ni kubwa na hivyo lazima wafiche.
Kwa sasa hatuna la kufanya. Kikatiba Jk anaruhusiwa kumaliza muda wake ila watanzania wenye mapenzi mema tuache mchezo na taifa letu. Maovu yanayofanya na viongozi mengine hayatakuw areversible. Matokeo yake litakuwa taifa la wehu kama Somalia na kwingineko. Dalili za hawa watu tunazisoma au kuambiwa haraka.
Huyu JK watu walishasema mapema kwamba he was not fit (alikuwa hafai kuwa kiongozi). Lakini kwa ushabiki tukamchagua, kwamba ni hundsome. Sasa mmeona he? kama mnabishi angalia watendaji wake wote; Mwema, mawaziri (tena siku hizi anawaita mawaziri mizigo).
Sasa hivi tunapewa warning tena ya EL. Kwamba tusipoangalia, tutaleta wauza madawa Ikulu. Watu, hasa viongozi wa dini waishaanza kuchukua michango yake. Mara utasikia ni boda boda day. Maafa watakayosababisha hawa watu kwa taifa ni makubwa sana.
Tuwakatae na uwezo tunao. Wanaweza kutuibia then waje watoe sadaka. Wanaweza kusafiri, kutuma polisi na kutupiga lakini hawawezi kupiga kura. Tuwakatae kabisa na tuandae maisha ya watoto wetu. Wao wameishajenga maisha yao na watoto wao nje ya nchi. Sisi tuijenge Tanzania.
Asanteni.