Rais Kikwete ni kweli umepewa Rushwa na TANECU?

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,277
6,673
Sio kwamba nakutuhumu muheshimiwa isipokuwa kama hupewi Taarifa na watu wako haya ndiyo yanayozungumzwa sana na watu wa Mtwara na kusababisha chuki dhidi yako kuwa kubwa mno.

Kumekuwa na ufisadi mkubwa ndani ya TANECU ambao unaonekana kufumbiwa macho na serikali yako, kila watu wanapohangaika kutaka kuivunja TANECU ili kuhakikisha hayo mambo yanakomeshwa kumekuwa na nguvu kubwa sana kutoka serikalini ya kuwakingia kifua, mifano ni mingi lakini wa karibu zaidi ni huu wa juzi ambapo Fax inasemekana imetoka kwako ili kuzuia usifanyike uchaguzi wowote ndani ya TANECU lengo ikiwa ni kuwalinda watu wako ambao inasemekana kila msimu wa korosho unapoisha wanakuletea kiasi kikubwa cha fedha. Inasemekana kila shilingi mia katika kilo ya korosho ni ya kwako,

Sijui kama taarifa hizi zinakufikia maana nina wasiwasi huenda wapasha habari wako wakaamua kukakaa kimya bila kuona madhara ya udhalilishaji huu.

Tuhuma hizi si mzuri kwa Taasisi ya uraisi zinadhalilisha sana na kuishusha hadhi yako. Tena hata kichama bado si zuri kwani madiwani kadhaa wa CCM nao wamesimama kidete kukipinga chama hiki cha ushirika ambacho kimekuwa na makusanyo makubwa kuliko Halmashauri za Wilaya lakini kikiwa na matumizi yasiyoeleweka, Moja ya mambo ya kushangazwa yaliyofanywa na TANECU ni kuchukua mkopo mkuwa wa dola Bilioni kadhaa ambazo watazilipia RIBA benki wakati wenyewe wana fedha ambazo zingetosha kujenga maghala.

Gharama hizi zinaenda kwa wananchi, hawa watendaji wa TANECU ambao inasemekana ni watu wako hawaumii kwa lolote.

RUSHWA imekuwa ni silaha kubwa sana inayotumiwa na hawa jamaa, Nikunong'oneze tu ni kwamba hata waziri wako wa KILIMO hana nguvu kwa TANECU..... Tunajua na hatubahatishi, hivi ninavyokueleza ni Muda mrefu sasa MKUU WA WILAYA YA TANDAHIMBA hayupo kituoni kwake, yaani anakaimu Wilaya nyingine wakati kwake hakuna mtu, unajua kwanini? waulize watu wako mkuu....... wasiwe wasiri kiasi cha kuhatarisha hadhi na usalama wako.

ANGALAU mara hii MKUCHIKA kasimama upande wa WANANCHI, ameona UFISADI mkubwa ndani ya TANECU na amesimama kwa nguvu zote kuhakikisha inavunjwa ili kila WILAYA inakuwa na chama chake cha ushirika lakini tatizo nguvu ya fedha ni kubwa kiasi cha kumfanya asipate ushirikiano wa kutosha kutoka kwa watendaji wako.

USHAURI WANGU KWAKO MUHESHIMIWA RAISI

Ufisadi unaofanyika kwenye Chama hiki cha ushirika ni mkubwa mno, Nashindwa kusema waziri wa kilimo asimamie hili kwani naye ni walewale......

1.Tafuta wakaguzi makini na wa kuaminika ambao hawataweza kuangushwa na nguvu ya TANECU uhakikishe TANECU na watendaji wake wanakaguliwa kwa kina. (kwa kukudokeza tu, mmoja wa watendaji wa TANECU ambaye ameanza kazi hivi karibuni anamiliki kituo cha mafuta NEWALA)

2.Wachunguzwe pia mkuu wa MKOA, na wakuu wa Wilaya juu ya uhusiano wao na TANECU.

3.Wakurugenzi wa Wilaya hususani TANDAHIMBA nao waingizwe kikaangoni.

4. Maafisa usalama nao waangaliwe kama wanatekeleza majukumu yao.

5. KAMA SI MTU WAKO, Basi ufanyike ukaguzi makini kwa MWENYEKITI WA TANECU ndugu NANNILA.

6.MWISHO, kusiwe na usiri kwenye minada ya korosho kwani hii inasababisha kutengenezwa kwa mianya ya ufisadi, MNADA uwe wa wazi na ikiwezekana urushwe moja kwa moja na redio au vituo vya Runinga.

HII SASA NI SIRI
Waambie watu wako wafuatilie kwa makini watu wanajiandaa kufanya nini iwapo dhuluma na ufisadi huu utaendelea? maana wameshajua kuwa Watendaji wa vyama vya msingi waliohudhuria mkutano mkuu wa TANECU walipewa 200,000 kila mmoja ili kuwanyamazisha.

Pengine hawajui lakini nakunong'oneza tu Muheshimiwa, kuna watu wameshaanza kuchonga mikuki na mishale.

Nenda mtaa wa KONGO (TNHMB) kuna watu wengi wameanza kumiliki zana hizo wakijiandaa na matokeo ya msimu, kinachonitisha ni jinsi walivyo makini na kufanya mambo kwa ukimya mkubwa.

Nimekuambia yote haya kwa sababu ninaamini hauhusiki isipokuwa ni matatizo mawili tu ndio unakabiliana nayo kama si kuoelezwa ukweli na watoa habari wako basi ni wewe mwenyewe kukosa umakini au kupuuza.

NAKUTAKIA KAZI NJEMA

===========
Mojawapo ya majibu:

Hongera sana Mwandishi kwa bandiko lako refu; Pia nakupongeza kwa wewe kuwa mkazi wa Mtwara kwani uliyoyaandika yanajionyesha wazi kuwa wewe ni mwana Mtwara.

Kabla sijaanza kuchambua ulichokileta humu jamvini ningependa usome uzi huu https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-mh-george-mkuchika-dhidi-ya-tanecu-ltd.html inaelekea umepewa kazi hii ya kuandika humu bila kufanya uchambuzi wa kutosha. Ugomvi baina ya Mh. Mkuchika na viongozi wa Tanecu haukuanza jana.Mh. John

Mnyika aliposema JK ni dhaifu baadhi ya wachambuzi walimshukia Mnyika na kumrushia maneno kuwa hana nidhamu. Ila hichi nachokiona hapa nakiri kwamba JK ni dhaifu. Haingii akilini kuona Waziri wa Utawala bora Mh. Mkuchika anaweka vijana nyuma ya Computer na kuanza kuichafua Ikulu kwa maslahi binafsi. Hakuna ubishi kuwa aliyeleta bandiko hili ni mfuasi wa Mh. Mkuchika ,huhitaji elimu ya Chuo Kikuu kutambua hili.

Sasa narudi kwenye Bandiko lako Bwana GazetiUmezungumzia wana Mtwara kana kwamba ulishafanya utafiti kwa haya uliyoyaandika . Sijui kama kweli ulifanya utafiti wa kweli ama ni uandishi tu umekutuma ukichanganya na mihemko binafsi. Vikao ambavyo vingekupa majibu ya utafiti wako ni Mkutano Mkuu wa TANECU wa tarehe 26/06/2014 uliofanyika Newala na Mkutano Mkuu wa Wadau wa Korosho cha tarehe 9-10/8/2014 kilichofanyika Masasi. Kwasababu umeandika kwa mihemko na ukitumia maneno yasiyoeleweka (Maneno ya mtaani -mfano ''Wamefanya ufisdi mkubwa mno'' bila kutaja huo ufisadi na kiwango).

Ushirika maana yake ni Umoja wa hiyari wa wanachama walioamua kujiunga ili waweze kujikwamua kiuchumi. Kuna maneno umeyaandika nimeshindwa kuelewa ulikuwa unamaanisha nini. Nanukuu, ''kila watu wanapohangaika kutaka kuivunja TANECU ili kuhakikisha hayo mambo yanakomeshwa kumekuwa na nguvu kubwa sana kutoka serikalini ya kuwakingia kifua''Mwisho wa kunukuu. Huu ni wimbo wa Mkuchika tokea enzi za MARCU akazalisha MAMCU na TANECU, kuvunja vunja hivi vya vya Ushirika pindi vinaposonga mbele kiuchumi. Kama kuna ufisadi unaousema wewe, kwani suluhu ni kuvunja hivi vyama ?.

Chama kikuu cha Ushirika Mkoa wa Mtwara -MARCU kilipovunjwa na huyu aliyekutuma uandike haya kilizaliwa chama Kikuu cha Mtwara na Masasi -MAMCU,Tandahimba na Newala -TANECU . Vyama hivi vilishindwa kujiendesha vikiagubikwa na madeni yasiyolipika takribani bilioni 800 -Tanecu takribani bilioni 200 na Mamcu takribani bilioni 600. Serikali mwaka 2007 ikaamua kuyachukua madeni hayo ili vyama hivyo vianze upya. Kama MARCU isingevunjwa kusengetokea hasari hiyo kwani MARCU ilikuwa inafanya vizuri. Fedha hizo zingejenga madarasa mangapi na zahanati ngapi?

Nukuu yako ''Moja ya mambo ya kushangazwa yaliyofanywa na TANECU ni kuchukua mkopo mkuwa wa dola Bilioni kadhaa ambazo watazilipia RIBA benki wakati wenyewe wana fedha ambazo zingetosha kujenga maghala''Una uandishi wa kishabiki bila kujua unachokiandika unakandia ama una pongeza . Hapo sikuelewa kuwa ulitaka kumaanisha nini! Kwasababu moja ya sifa za taasisi kukopesheka ni kwamba inafanya vizuri katika kazi zake hususani kwenye masuala ya fedha.

Ngoja nikusaidie kwasababu inaelekea hujui ila hukuomba upewe elimu ili uelewe . TANECU wana mpango wa kujenga kiwanda kikubwa cha kubangua Korosho Tandahimba chenye uwezo wa kuzalisha takribani tani 30,000 kwa mwaka . Wameomba Mkopo TIB wa takribani bilioni 40 za kitanzania ( Mabilioni yako ya dola ni upotoshaji na hujui ulichoandika). Kama mapato ya TANECU mwaka 2013/14 yalikuwa 1,376,364,753/= fedha za Kitanzania huo uwezo wa Mabilioni ya fedha wameyatoa wapi?.

Nukuu yako ''Nenda mtaa wa KONGO (TNHMB) kuna watu wengi wameanza kumiliki zana hizo wakijiandaa na matokeo ya msimu, kinachonitisha ni jinsi walivyo makini na kufanya mambo kwa ukimya mkubwa.''

Kama Mh. Mkuchika anaingia mtaani na vijana wake basi hizi ni taarifa za kufanyiwa kaziVikao nilivyovitaja hapo juu -Mkutano Mkuu wa TANECU na Mkutano Mkuu wa Wadau wa Korosho Mh. wako Mkuchika alipingwa vikali na hoja zake. Kwa ufupi ni kwamba wamegundua kuwa Mh. Mkuchika ni mbinafsi na hawatakii wanachi wake mema- Masasi alizomewa na hao wakulima wawakilishi wa wana Mtwara na Mkuatano ule ulirushwa live na kituo cha kimoja cha Radio -Mtwara.

Ushauri kwa Wana Mtwara na Kwako:

Nimetembelea Mkoa wa Kilimanjaro mwezi wa tano nikastaajabu kuona wilaya takribani zote zimeunganishwa kwa kiwango cha lami. Barabara ya kutoka Mwanga kuelekea Usangi na Vuchama inasonga kwa kasi ya ajabu kwa kiwango cha lami.

Wilaya za Tandahimba na Newala ndizo zinazozalisha korosho kwa wingi nchini Tanzania Takribani 45% ya korosho inatoka Tandahimba na Newala ila wilaya hizo hazijaunganishwa na Makao makuu ya Mkoa kwa barabara ya kiwango cha lami,achilia mbali changamoto nyingine kama Maji nk.

Zao la Korosho kwa mwaka 2013/14 - Kwa mujibu wa Takwimu za Benk Kuu ya Tanzania zilizotolewa mwezi wa nne mwaka huu, zao la Korosho limekuwa la pili kwa kuliingizia Taifa letu fedha za kigeni (Dola za kimarekani 133.4milioni) lkiongoza Tumbaku.

Viongozi wa Mtwara mwache malumbano ya wenyewe kwa wenyewe ,wenzenu wanasonga mbele ninyi mmekalia majungu fitna na uzindaki. Mkoa wa Mtwara una Malighafi nyingi sana za kuwawezesha wana Mtwara na Watanzania tukaondokana na Umasikini unaotung'ata kila kukicha.

Gombanene na Mawazi wenzenu huko kwenye baraza la Mawaziri muwaletee maendeleo wana Mtwara kama wenzenu wa Mbeya, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha na Kagera. Mnatia aibu kuweka vijana kwenye social Media kuandika majungu na upuuzi kama huu.
 
unyonyaji kila mahali huko kwenye korosho ni tangu enzi hizo nakua nausikia tu
 
Kweli watanzania nani kawaroga jamani?! Mleta mada anaonesha dhahiri kuwa anauhakika na anachosema japo kuna baadhi ya wachangiaji wanambeza! Kwa maslahi ya nani? Rais achunguze kuna watu huenda wanataka kumchafua rais wetu kwa kumpa taarifa zisizo sahihi. Usalama wa taifa sina hakika kama wanafanya kazi yao kwa umakini na uadilifu! Iweje wasijue jambo kama hili na kuliripoti mahali husika? Mungu tuokoe waja wako.
 
Umenena vema kabisa na hii leo ndio wanakalia Tenda ya maghala huko Newala,, na habari za uhakika kabisa watendaji wa Tanecu wamesajili kampuni yao kwa mgongo wa mtu anaeitwa Mkata tena huyo Mkata mwenyewe anaumwa yuko hosptal kwa mda mrefu,,
 
Na wametoa rushwa kwa wajumbe ili kampuni ya Mkata ambayo kiukweli wana maslahi nayo ishinde ghala la Tandahimba yani Tanecu inanuka rushwa vibaya mno.
 
kuna mtu kaenda kula hiyo mihela(posho) ya tanecu namjua.

mtaje basi na uthibitisho ndugu, maana hii nchi kila sehemu inaliwa, nimeona ile video ya uwindaji haramu nimesikitika sana, sasa hivi kwenye tanecu, Tanzania imeshatoboka kila mahali.
 
GAZETI wewe ni mmbea mkubwa na una tabia za kishangingi,jk hana muda mchafu huo, kama una hoja iwasilishe kistaarabu

Umeelekeza kwa GAZETI ukatuma wote tukasoma. Nini maana ya Ustaarabu. Nini ktk maandishi yake ni kinyume na ustaarabu? Au ni tuhuma kwa Rasi. Africa hii haina wezi madarakani? hebu nawe eleza.
 
Last edited by a moderator:
Waziri mkuu anajua maana walishamuendea dodoma kujiliza na uchaguzi umesitishwa kuna nini??
 
Too late the hero

Yeye amepata nafasi hiyo kwa rushwa iliyokubwa, mbona unalalamika cha mtoto? Kesi ya mbuzi kwa fisi?

Na bado tutalia na kusaga meno
 
Hongera sana Mwandishi kwa bandiko lako refu; Pia nakupongeza kwa wewe kuwa mkazi wa Mtwara kwani uliyoyaandika yanajionyesha wazi kuwa wewe ni mwana Mtwara.

Kabla sijaanza kuchambua ulichokileta humu jamvini ningependa usome uzi huu https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-mh-george-mkuchika-dhidi-ya-tanecu-ltd.html inaelekea umepewa kazi hii ya kuandika humu bila kufanya uchambuzi wa kutosha. Ugomvi baina ya Mh. Mkuchika na viongozi wa Tanecu haukuanza jana.Mh. John

Mnyika aliposema JK ni dhaifu baadhi ya wachambuzi walimshukia Mnyika na kumrushia maneno kuwa hana nidhamu. Ila hichi nachokiona hapa nakiri kwamba JK ni dhaifu. Haingii akilini kuona Waziri wa Utawala bora Mh. Mkuchika anaweka vijana nyuma ya Computer na kuanza kuichafua Ikulu kwa maslahi binafsi. Hakuna ubishi kuwa aliyeleta bandiko hili ni mfuasi wa Mh. Mkuchika ,huhitaji elimu ya Chuo Kikuu kutambua hili.

Sasa narudi kwenye Bandiko lako Bwana Gazeti.
Umezungumzia wana Mtwara kana kwamba ulishafanya utafiti kwa haya uliyoyaandika . Sijui kama kweli ulifanya utafiti wa kweli ama ni uandishi tu umekutuma ukichanganya na mihemko binafsi. Vikao ambavyo vingekupa majibu ya utafiti wako ni Mkutano Mkuu wa TANECU wa tarehe 26/06/2014 uliofanyika Newala na Mkutano Mkuu wa Wadau wa Korosho wa tarehe 9-10/8/2014 uliofanyika Masasi. Kwasababu umeandika kwa mihemko na ukitumia maneno yasiyoeleweka (Maneno ya mtaani -mfano ''Wamefanya ufisdi mkubwa mno'' bila kutaja huo ufisadi na kiwango).

Ushirika maana yake ni Umoja wa hiyari wa wanachama walioamua kujiunga ili waweze kujikwamua kiuchumi. Kuna maneno umeyaandika nimeshindwa kuelewa ulikuwa unamaanisha nini. Nanukuu, ''kila watu wanapohangaika kutaka kuivunja TANECU ili kuhakikisha hayo mambo yanakomeshwa kumekuwa na nguvu kubwa sana kutoka serikalini ya kuwakingia kifua''Mwisho wa kunukuu. Huu ni wimbo wa Mkuchika tokea enzi za MARCU akazalisha MAMCU na TANECU, kuvunja vunja hivi vya vya Ushirika pindi vinaposonga mbele kiuchumi. Kama kuna ufisadi unaousema wewe, kwani suluhu ni kuvunja hivi vyama ?.

Chama kikuu cha Ushirika Mkoa wa Mtwara -MARCU kilipovunjwa na huyu aliyekutuma uandike haya kilizaliwa chama Kikuu cha Mtwara na Masasi -MAMCU,Tandahimba na Newala -TANECU . Vyama hivi vilishindwa kujiendesha vikiagubikwa na madeni yasiyolipika takribani milioni 800 -Tanecu takribani milioni 200 na Mamcu takribani milioni 600. Serikali mwaka 2007 ikaamua kuyachukua madeni hayo ili vyama hivyo vianze upya. Kama MARCU isingevunjwa kusengetokea hasari hiyo kwani MARCU ilikuwa inafanya vizuri. Fedha hizo zingejenga madarasa mangapi na zahanati ngapi?

Back
Top Bottom