Mdudu halisi
JF-Expert Member
- May 7, 2014
- 2,730
- 4,771
Ndg yangu Sina Jina1, kwanza nikushukuru sana kwa mchango wako ambao umejaa ushahidi wa kina wenye kuandamana na data. Ni dhahiri ya kwamba hata mimi naungana nawe katika baadhi ya masuala uliyoyachambua na kuyaeleza kwa kina. Suala mojawapo ambalo nakuunga mkono ni kwamba SULUHISHO la changamoto zinazoikabili TANECU si KUKIVUNJA chama hicho kikuu cha Ushirika katika wilaya za Tandahimba na Newala, bali ni kutafuta kiini kinachosababisha changamoto hizo kisha kuzifanyia kazi bila kuathiri muundo wa sasa wa chama.Hongera sana Mwandishi kwa bandiko lako refu; Pia nakupongeza kwa wewe kuwa mkazi wa Mtwara kwani uliyoyaandika yanajionyesha wazi kuwa wewe ni mwana Mtwara.
Kabla sijaanza kuchambua ulichokileta humu jamvini ningependa usome uzi huu https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-mh-george-mkuchika-dhidi-ya-tanecu-ltd.html inaelekea umepewa kazi hii ya kuandika humu bila kufanya uchambuzi wa kutosha. Ugomvi baina ya Mh. Mkuchika na viongozi wa Tanecu haukuanza jana.Mh. John
Mnyika aliposema JK ni dhaifu baadhi ya wachambuzi walimshukia Mnyika na kumrushia maneno kuwa hana nidhamu. Ila hichi nachokiona hapa nakiri kwamba JK ni dhaifu. Haingii akilini kuona Waziri wa Utawala bora Mh. Mkuchika anaweka vijana nyuma ya Computer na kuanza kuichafua Ikulu kwa maslahi binafsi. Hakuna ubishi kuwa aliyeleta bandiko hili ni mfuasi wa Mh. Mkuchika ,huhitaji elimu ya Chuo Kikuu kutambua hili.
Sasa narudi kwenye Bandiko lako Bwana Gazeti.
Umezungumzia wana Mtwara kana kwamba ulishafanya utafiti kwa haya uliyoyaandika . Sijui kama kweli ulifanya utafiti wa kweli ama ni uandishi tu umekutuma ukichanganya na mihemko binafsi. Vikao ambavyo vingekupa majibu ya utafiti wako ni Mkutano Mkuu wa TANECU wa tarehe 26/06/2014 uliofanyika Newala na Mkutano Mkuu wa Wadau wa Korosho wa tarehe 9-10/8/2014 uliofanyika Masasi. Kwasababu umeandika kwa mihemko na ukitumia maneno yasiyoeleweka (Maneno ya mtaani -mfano ''Wamefanya ufisdi mkubwa mno'' bila kutaja huo ufisadi na kiwango).
Ushirika maana yake ni Umoja wa hiyari wa wanachama walioamua kujiunga ili waweze kujikwamua kiuchumi. Kuna maneno umeyaandika nimeshindwa kuelewa ulikuwa unamaanisha nini. Nanukuu, ''kila watu wanapohangaika kutaka kuivunja TANECU ili kuhakikisha hayo mambo yanakomeshwa kumekuwa na nguvu kubwa sana kutoka serikalini ya kuwakingia kifua''Mwisho wa kunukuu. Huu ni wimbo wa Mkuchika tokea enzi za MARCU akazalisha MAMCU na TANECU, kuvunja vunja hivi vya vya Ushirika pindi vinaposonga mbele kiuchumi. Kama kuna ufisadi unaousema wewe, kwani suluhu ni kuvunja hivi vyama ?.
Chama kikuu cha Ushirika Mkoa wa Mtwara -MARCU kilipovunjwa na huyu aliyekutuma uandike haya kilizaliwa chama Kikuu cha Mtwara na Masasi -MAMCU,Tandahimba na Newala -TANECU . Vyama hivi vilishindwa kujiendesha vikiagubikwa na madeni yasiyolipika takribani milioni 800 -Tanecu takribani milioni 200 na Mamcu takribani milioni 600. Serikali mwaka 2007 ikaamua kuyachukua madeni hayo ili vyama hivyo vianze upya. Kama MARCU isingevunjwa kusengetokea hasari hiyo kwani MARCU ilikuwa inafanya vizuri. Fedha hizo zingejenga madarasa mangapi na zahanati ngapi?
Nukuu yako ''Moja ya mambo ya kushangazwa yaliyofanywa na TANECU ni kuchukua mkopo mkuwa wa dola Bilioni kadhaa ambazo watazilipia RIBA benki wakati wenyewe wana fedha ambazo zingetosha kujenga maghala''Una uandishi wa kishabiki bila kujua unachokiandika unakandia ama una pongeza . Hapo sikuelewa kuwa ulitaka kumaanisha nini! Kwasababu moja ya sifa za taasisi kukopesheka ni kwamba inafanya vizuri katika kazi zake hususani kwenye masuala ya fedha.
Ngoja nikusaidie kwasababu inaelekea hujui ila hukuomba upewe elimu ili uelewe . TANECU wana mpango wa kujenga kiwanda kikubwa cha kubangua Korosho Tandahimba chenye uwezo wa kuzalisha takribani tani 30,000 kwa mwaka . Wameomba Mkopo TIB wa takribani bilioni 40 za kitanzania ( Mabilioni yako ya dola ni upotoshaji na hujui ulichoandika). Kama mapato ya TANECU mwaka 2013/14 yalikuwa 1,376,364,753/= fedha za Kitanzania huo uwezo wa Mabilioni ya fedha wameyatoa wapi?.
Nukuu yako ''Nenda mtaa wa KONGO (TNHMB) kuna watu wengi wameanza kumiliki zana hizo wakijiandaa na matokeo ya msimu, kinachonitisha ni jinsi walivyo makini na kufanya mambo kwa ukimya mkubwa.''
Kama Mh. Mkuchika anaingia mtaani na vijana wake basi hizi ni taarifa za kufanyiwa kaziVikao nilivyovitaja hapo juu -Mkutano Mkuu wa TANECU na Mkutano Mkuu wa Wadau wa Korosho Mh. wako Mkuchika alipingwa vikali na hoja zake. Kwa ufupi ni kwamba wamegundua kuwa Mh. Mkuchika ni mbinafsi na hawatakii wanachi wake mema- Masasi alizomewa na hao wakulima wawakilishi wa wana Mtwara na Mkuatano ule ulirushwa live na kituo cha kimoja cha Radio -Mtwara.
Ushauri kwa Wana Mtwara na Kwako:
Nimetembelea Mkoa wa Kilimanjaro mwezi wa tano nikastaajabu kuona wilaya takribani zote zimeunganishwa kwa kiwango cha lami. Barabara ya kutoka Mwanga kuelekea Usangi na Vuchama inasonga kwa kasi ya ajabu kwa kiwango cha lami.
Wilaya za Tandahimba na Newala ndizo zinazozalisha korosho kwa wingi nchini Tanzania Takribani 45% ya korosho inatoka Tandahimba na Newala ila wilaya hizo hazijaunganishwa na Makao makuu ya Mkoa kwa barabara ya kiwango cha lami,achilia mbali changamoto nyingine kama Maji nk.
Zao la Korosho kwa mwaka 2013/14 - Kwa mujibu wa Takwimu za Benk Kuu ya Tanzania zilizotolewa mwezi wa nne mwaka huu, zao la Korosho limekuwa la pili kwa kuliingizia Taifa letu fedha za kigeni (Dola za kimarekani 133.4milioni) lkiongoza Tumbaku.
Viongozi wa Mtwara mwache malumbano ya wenyewe kwa wenyewe ,wenzenu wanasonga mbele ninyi mmekalia majungu fitna na uzindaki. Mkoa wa Mtwara una Malighafi nyingi sana za kuwawezesha wana Mtwara na Watanzania tukaondokana na Umasikini unaotung'ata kila kukicha.
Gombanene na Mawazi wenzenu huko kwenye baraza la Mawaziri muwaletee maendeleo wana Mtwara kama wenzenu wa Mbeya, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha na Kagera. Mnatia aibu kuweka vijana kwenye social Media kuandika majungu na upuuzi kama huu.
Ndg yangu Sina Jina1, licha ya umakini wa hoja zako ambazo umezileta hapa kwenye hii hoja, umeonekana kutotenda haki kwa kuushambulia upande mmoja tu huku ukiubeba upande mwingine. Mengi uliyoyaeleza kwa upande wa TANECU ni mazuri na umeshindwa kubainisha mapungufu waliyonayo. Ni kweli kwamba suala la rushwa ambalo kaka yangu, Bw. Gazeti ameliongelea linachukua nafasi kwa kiasi kikubwa miongoni mwa watendaji wa TANECU na wala sio UZUSHI.
Nimewahi kushuhudia mimi mwenyewe, makatibu wa vyama vya ushirika vya msingi wakitakiwa kutoa kiasi cha sh. 100,000 (laki moja) kama rushwa ili waweze kupatiwa marobota ya magunia ambayo yanatumika kuhifadhia korosho zilizo tayari kusafirishwa. Ukiachilia mbali RUSHWA hiyo ya magunia, kuna rushwa nyingine ambayo watendaji wa TANECU wamekuwa wakiidai toka kwa makatibu wa vyama vya msingi vya ushirika, nayo ni kiasi cha sh. 100,000 (laki moja) kwa ajili ya kuwapatia makatibu hao idhini (kusaini hundi) ya kwenda kchukua fedha benki. Ni matumaini yangu kwamba, endapo uchunguzi wa kina utafanyika dhidi ya Meneja wa TANECU tawi la Tandahimba Bw. Udede, madudu mengi sana yanayofanywa na watendaji hao kama hujuma dhidi ya mfumo huu wa stakabadhi ghalani yatagundulika.
Kupitia vitendo vya RUSHWA vinavyoendeshwa na watendaji hawa wa chama kikuu cha ushirika huku Bodi ya chama hicho inayoongozwa na Bw. Yusuf Nannila ikionekana kukaa kimya, ni dhahiri ya kwamba ushirika utaendelea kudumaa katika wilaya hizi mbili za Tandahimba na Newala huku wakulima wakiendelea kuwa maskini wa kutupwa licha ya UTAJIRI mkubwa walionao wa rasilimali
.
Serikali nayo haiwezi kuepuka lawama kwa kuweka mfumo mbovu wa mauzo ya korosho za wakulima, hasa kutokana na uendeshaji wa MNADA. Katika shughuli za uuzaji kuna KIKOSI KAZI (task force) kimeteuliwa kikimhusisha mkuu wa mkoa na wadau wengine. Hawa jamaa hawauzi korosho kwa njia ya MNADA kama ilivyopendekezwa bali huuza korosho kwa njia ya ZABUNI (tender). Njia ya MNADA, mauzo huwa ya wazi huku yakishuhudiwa na Bodi ya zao husika pamoja na wadau wengine (fuatilia mnada wa zao la kahawa kule Kilimanjaro) wakati kwa njia ya zabuni mauzo huwa ya siri ambapo ni watu wachache tu huhusika, na hivi ndivyo ilivyo kwenye mauzo ya zao la korosho ambapo watu wachache tu ndiyo hushuhudia mchakato mzima hasa wajumbe wenyewe wanaounda kikosi kazi huku wakulima na wadau wengine wakitengwa. Mfumo huu wa uuzaji hupelekea makampuni yanayonunua korosho kuwarubuni wajumbe hao wa kikosi kazi na hivyo kujihusisha na vitendo vya RUSHWA hatimaye wakulima kutopata bei inayoridhisha ya mazao yao.
Kwa ujumla huu mfumo wenyewe una mapungufu makubwa kwani unaruhusu kuwepo kwa mianya ya RUSHWA, kwa hiyo bila kufanya marekebisho katika uendeshaji, wakulima wa korosho wasitarajie kuufikia UKOMBOZI WA KIUCHUMI.
Nawasilisha.