Rais Kikwete ni kweli umepewa Rushwa na TANECU?

Rais Kikwete ni kweli umepewa Rushwa na TANECU?

Haiwezekani kuvunjwa Tanecu.

Huyo mkuchika unaemsema kwamba ana uchungu na Tanecu mnafiki mkubwa ndie huyo huyo alieimaliza na kuifisidi NDF...i.e Newala Development Fund.

Mfuko wa maendeleo ya wilaya ya newala kaufilisi huyo mkuchika ndani ya miaka yake 10 ya ubunge.

Amefuta utawala wooote na kuhamishia nyumbani mwake.

Kama unabisha nenda kwenye website ya NDF...uone kulivyo na madudu.

Hakuna uchaguz...hakuna ukaguz wwte wa mahesabu.

Pesa yasemekana anachukua kiholela tuh toka kwa wahisani kisha atatia mifukoni mwake.

Kikwete mpeni lawama kwa mengine lkn hili ya Tanecu hahusiki.

Labda uniambie kuwa kinachoifilisi Tanecu ni uongozi mbovu na ufisadi hapo nitakubali.

Lkn siyo kumpa lawama kikwete.

Mkuchika anataka Tanecu ivunjwe ili pawepo na na Nanecu ili aweze kuifilisi kama alivyoifilisi NDF.

Ujinga huo watu wa newala na tandahimba hawawez kuufanya pamoja na umbumbumbu wetu lkn hilo hatulipi nafasi hata kidogo.

Mkuchika ukae ukilijua hilo.
 
SINA JINA1

Mkuu umeongea kweli kabisa.

Huyu mleta mada atakuwa katumwa na mkuchika.

Mkuchika kafanya njama mwaka jana hadi yule mmakonde mwenzetu afisa ushirika wa wilaya kahamishwa kwa kisa tuh alikuwa anapinga njama zake za kuivunja Tanecu.

Siku zooote umoja ni nguvu..sasa yeye mkuchika anataka Tanecu ivunjwe ili iweje.

Anadhani watu tumesahau ufisadi alioufanya NDF?

Ni kweli kbs wilaya ya newala na tandahimba ndizo huongoza kwa zao la korosho na kuwa la pili kwa kwa pato la taifa inasikitisha kuona bado wilaya hiyo bara bara hazijaunganishwa na lami hadi makao makuu.

Kiufupi viongoz waliopo wameshindwa kuweka uzalendo mbele.

Mkuchika aache unafiki wake.
 
Last edited by a moderator:
Kinachotuma wana Tandahimba ni ufisadi wanaofanya watendaji wa Tanecu au nyie hamuuoni?

Mimi nina uhakika Rais hajui madudu ya Tanecu,, watendaji wanasajili kampuni wanajiombea kazi na wanajipa wenyewe wakati kampuni za wazawa zipo na zimeomba na wana sifa zakufanya kazi alafu nyinyi mnadai Tanecu isivunjwe na kumsema Mh. MKUCHIKA...

Tunajua ufisadi wote wanaofanya ule wa magunia na jinsi walivowapa wajumbe.rushwa ili wapitishe kapuni yao
 
Hili la Tanecu mimi nitalibeba mpaka kwa Rais wa Nchi najua yeye hajui haya madudu na hawezi kufumbia macho.
 
Roho inaniuma sana ninapoona baadhi ya watu wako humu ndani kuitetea TANECU.
 
Mimi kitu kinachonikera MNADA kuwa SIRI ,yan Makampuni ya Ununuzi wa korosho Bei wanaweka kwenye bahasha alafu wanafungua watu awazidi Wanne kisha wanaitaja kampuni lioshinda,huu ni Ufisadi piga Mnada LIVE watu waone,siri siri yanini!!!
 
Wakuu SINA JINA1 na THE BIG SHOW nina wasiwasi kuwa ninyi ni miongoni mwa watu
wenye maslahi mapana na TANECU, hata kama mkuchika atakuwa na mapungufu vipi
bado hili la kuivunja TANECU litakuwa na manufaa makubwa kwa namna moja au nyingine
hususani kwa wakulima wa TANDAHIMBA.

SINA JINA1 Nashangaa umetumia maarifa makubwa kuitetea Tanecu kwa bandiko zuri la kitaalamu lakini
lisilotofautiana na maneno mazuri ya wakili ambaye anamtetea mtuhumiwa wa mauaji wakati
anafahamu wazi kuwa ni muuaji.

THE BIG SHOW na SINA JINA1 tuwe waungwana na tuwe wazalendo nawaombeni, hivi ni kipi
kikubwa inachofanya TANECU kama si kumdidimiza mkulima? pamoja na maslahi mapana muliyonayo
ndani ya TANECU hebu muogopeni MUNGU, hivi hamkumbuki pale UWAKOTA iliposimama ikaleta
upinzani mkubwa kwa TANECU na kuifanya bei ya korosho kuwa juu?

Kwanini TANECU ilisimama kidete kuhakikisha kuwa hakuna yeyote ambaye atahusika na zao hilo
kwa Wilaya ya NEWALA na TANDAHIMBA zaidi yao? Tusidanyane kwa kauli za kisiasa hapa
TANECU inatutesa na kutukandamiza sisi wakulima.

Pamoja na uchangiaji wenu hakuna aliyefafanua kwanini minada ya korosho inatawaliwa na usiri
mkubwa, Pia hakuna aliyefafanua kwa nini TANECU wanalipa awamu tatu tena baada ya vikao
vya kujadili ni kiasi gani mkulima alipwe. Yaani mazao tulime sisi, ushuru tukatwe na bado baada
ya hayo makato kuwe na mjadala mwingine wa nini tulipwe katika kile kilichobaki.

BAADHI YA VIPENGERE VYA HOJA ZAKO NA MAJIBU YAKE.
Ushirika maana yake ni Umoja wa hiyari wa wanachama walioamua kujiunga ili waweze kujikwamua kiuchumi.
kwa TANECU si hiyari kila mkulima analazimishwa kupitia huko ndio maana ushirika mwingine wa aina yoyote si Ruhusa
kwa taarifa tu, mimi ni miongoni mwa wakulima ambao Korosho zetu zilikamatwa baada ya kuamua kuuza kupitia umoja
wetu UWAKOTA, unakumbuka? au kwa kuwa uko nyuma ya keyboard ukipokea posho basi unajionea sawa tu?

Ngoja nikusaidie kwasababu inaelekea hujui ila hukuomba upewe elimu ili uelewe . TANECU wana mpango wa kujenga kiwanda kikubwa cha kubangua Korosho Tandahimba chenye uwezo wa kuzalisha takribani tani 30,000 kwa mwaka . Wameomba Mkopo TIB wa takribani bilioni 40 za kitanzania ( Mabilioni yako ya dola ni upotoshaji na hujui ulichoandika). Kama mapato ya TANECU mwaka 2013/14 yalikuwa 1,376,364,753/= fedha za Kitanzania huo uwezo wa Mabilioni ya fedha wameyatoa wapi?.

Suala sio mpango wa ujenzi na hayo mengine unayoyataja, jambo la msingi ni je hayo yatamnifaisha mkulima,
Utaalamu wako wa kuandika na kupamgilia maneno bado haufuti udhalimu unaofanywa na TANECU, hata kama
watajenga nini bado kwa TANECU hii tunayoifahamu hakitamnufaisha mkulima. Sisi ndio tunaoumia wewe hujui
hata jinsi ya kufagilia mkorosho mmoja na leo unaonekana kuibuka hapa na kutaka kuitetea TANECU.

Halafu mwisho unasema hujafanya utafiti, mimi ndiye ninayedhulumiwa na TANECU unataka nifanye utafiti
gani? Na huyo mkuchika unayemtaja hajanituma, kilichonituma ni maumivu na mateso ambayo ninayapata
katika kilimo cha korosho pale ninapoona yanawanufaisheni zaidi watu mlioko ndani ya TANCU kuliko wakulima
wenyewe.

Ukirudi hapa naomba majibu ya mambo matatu tu
1.kwanini minada ya korosho inatawaliwa na usiri mkubwa.
2. Kwanini watu wa NEWALA walilipwa malipo makubwa ya korosho yale ya awamu ya tatu kuliko wa TANDAHIMBA?
3.Umesema ushirika ni hiyari, kwanini huu umekuwa ni wa lazima?
 
SINA JINA1

Mkuu umeongea kweli kabisa.

Huyu mleta mada atakuwa katumwa na mkuchika.

Mkuchika kafanya njama mwaka jana hadi yule mmakonde mwenzetu afisa ushirika wa wilaya kahamishwa kwa kisa tuh alikuwa anapinga njama zake za kuivunja Tanecu.

Siku zooote umoja ni nguvu..sasa yeye mkuchika anataka Tanecu ivunjwe ili iweje.

Anadhani watu tumesahau ufisadi alioufanya NDF?

Ni kweli kbs wilaya ya newala na tandahimba ndizo huongoza kwa zao la korosho na kuwa la pili kwa kwa pato la taifa inasikitisha kuona bado wilaya hiyo bara bara hazijaunganishwa na lami hadi makao makuu.

Kiufupi viongoz waliopo wameshindwa kuweka uzalendo mbele.

Mkuchika aache unafiki wake.

THE BIG SHOW,
Kwa mara ya Kwanza toka nikufahamu nimejikuta nikishangazwa nawe,
unaifahamu vizuri TANECU au nawe ni katika mnaopata mgao? Nakutilia mashaka
THE BIG SHOW kitendo cha kuitetea TANECU tu tena na kusisitiza
haiwezi kuvunjwa kinanifanya nikose Imani nawe.

nampongeza sana Uvahi anajua hali halisi.
 
Ningependa kumuuliza maswali huyu THE BIG SHOW, Una shamba la mikorosho?
Kama huna umewahi kulima korosho angalau kwa kukodi shamba?

Kuhusu SINA JINA1 sina wasiwasi kuwa ni mtu wa ofisini tu kwani hoja zake zina mpangilio
sawa na wa INSHA za skondari ambazo zinakuwa bora kwa mtiririko tu lakini si kilichoandikwa
hawezi kuwa Mkulima wa korosho huyu ni walewale wanaokula fedha za TANECU.
 
Mimi kitu kinachonikera MNADA kuwa SIRI ,yan Makampuni ya Ununuzi wa korosho Bei wanaweka kwenye bahasha alafu wanafungua watu awazidi Wanne kisha wanaitaja kampuni lioshinda,huu ni Ufisadi piga Mnada LIVE watu waone,siri siri yanini!!!
Ni kweli mkuu, halafu watu wanakuja kusimama hapa na kuitetea TANECU kwa hoja
za kitoto kabisa, Hili dudu halivumiliki kabisa.
 
Mkuu Gazeti.

Mimi mwenyewe ni mkulima wa korosho.

Ninayo mashamba mdimba mnyoma...ninayo mashamba kitama namonde na ninayo mashamba luagala.

Meengi ya mashamba hayo ni ya urith na mengine ni ya familia na ukoo.

Kwahiyo aza ya kilimo hiko naijua.

Suala hapa ni kwamba mimi sipo hapa kuishabikia Tanecu.

Mimi napinga hilo unalolisema bila ushahid hapo unaposema kwamba kikwete anahusika ktk kuifilisi Tanecu hilo si kweli.

Cha umuhimu hapo ni kuungana na kuundoa uongozi wa Tanecu lkn sio kuuvunja umoha huo wa Tanecu moja kwa moja.

Hata ukiuvunja na kufanya kila wilaya iwe na chama chake cha ushirika utasolve nn kama hulka za viongoz ni hizo hizo??

Suala hapo ni kuuvunja uongozi na sio kuivunja Tanecu.

Mimi sipo hapa kushabikia madudu ya Tanecu.

Nipo kupinga kuvunjwa kwa Tanecu.

Tanecu kama chama cha ushirika hakina kosa wala tatizo lolote.na watu dunian koote huendelea kwa kuungana kwa ushirika.

Hatuwez kuvunja chama hiko.

Sema tupige kelele chama hiko kibadilshe uongozi.
 
Ni kweli mkuu, halafu watu wanakuja kusimama hapa na kuitetea TANECU kwa hoja
za kitoto kabisa, Hili dudu halivumiliki kabisa.

Mkuu Gazeti.

1.uliposema kikwete anahusika na madudu yanayoendelea Tanecu napinga sio kweli labda weka ushahid na sio maneno matupu.

2.mimi sipo kuwashabikia viongozi wa Tanecu ho kina Nannila.

Kama wameboronga wabadilishwe.

3.Tanecu as Chama hakina kosa lolote kosa ni la hao viongozi.

Hatuwez kuvunja chama cha ushirika kwa madudu ya viongozi.

Hao viongozi waondoke watuachie chama chetu.

Pia huyo mkuchika unaemuona wa maana leo eti kwamba ni mkombozi wa kuivunja tanecu tuulize sisi tukueleza madudu aliyoyafanya N.D.F i.e Newala Development Fund.

Jins alivyoifilisi na kuiweka mfukoni mwake.

Hakuna management NDF...

Hakuna ukaguz wa hesabu NDF...leo sisi tuwe wajinga kumruhusu aivunje Tanecu ili aiweke mfukoni mwake kama NDF??

Hilo waambie wasiojua...

Sisi tunajua kinachoendelea hapo kiundani kabisa.

Na Tupo Imara kuilinda Tanecu.

By anymeans necessary ikibidi.
 
THE BIG SHOW nimekuelewa mkuu, lakini mimi sijamtuhumu muheshimiwa, ninachoeleza
hapa ni kuwa watu wanamtuhumu Muheshimiwa kuwa anahusika (Sio mimi ninayetuhumu)
Pengine hajafikishiwa kuwa anatuhumiwa kwa haya mambo ndio maana nataka afahamu.
Hata mimi siamini kuwa anahusika, ingawa nina mashaka sana na waziri wa Wizara husika.

Watu ambao ninawatuhumu mimi na nina uhakika ni baadhi ya viongozi wa Kimkoa na Halmashauri
ni wazi wamekuwa ni walaji wazuri wa Rushwa kuna vitu bado sijakamilisha ili niweke ushahidi hapa
jukwaani kwani najua sina nguvu ya kuwashinda mahakamani, Nguvu yao ni kubwa sana kifedha.

Nashukuru kwa mtazamo wako na sasa nimekuelewa, pengine jambo la muhimu zaidi ni kungeza vyama
ambavyo vitaleta upinzani kwa Tanecu kama ilivyo UWAKONA, UWAKONE na UWAKOTA.
 
Kinachotuma wana Tandahimba ni ufisadi wanaofanya watendaji wa Tanecu au nyie hamuuoni?

Mimi nina uhakika Rais hajui madudu ya Tanecu,, watendaji wanasajili kampuni wanajiombea kazi na wanajipa wenyewe wakati kampuni za wazawa zipo na zimeomba na wana sifa zakufanya kazi alafu nyinyi mnadai Tanecu isivunjwe na kumsema Mh. MKUCHIKA...

Tunajua ufisadi wote wanaofanya ule wa magunia na jinsi walivowapa wajumbe.rushwa ili wapitishe kapuni yao

Sawa nakubali hoja zako.

Wako nnumbuwangu choonde.

Vanu vene tunilaga lagaaa...!!

Tukave na chinu ndulu nkanya piii...tuve na chani??

Mgomvi wetu tuni mmala ake kikwete ake Tanecu.

Mchawi wetu ni hawa viongozi wa Tanecu.

Tuwabadilishe tu.

Hatuwez kumlaumu kikwete wala hatuwez kuilaumu Tanecu kama chama cha ushirika.
 
Mkuu, THE BIG SHOW

1.uliposema kikwete anahusika na madudu yanayoendelea Tanecu napinga sio kweli labda weka ushahid na sio maneno matupu.
(Mkuu wasikilize vizuri wanachoongea watu mtaani, sio mimi tena mimi nimejitahidi kupunguza ukali wa
kile kinachozungumzwa na ndio maana nimesema huu ni udhalilishaji kwa taasisi ya Uraisi hata nikafikia
kuomba minada iwe ya wazi, na hii wakati mwingine inatokana na majigambo na kiburi cha watu wa TANECU.

2.mimi sipo kuwashabikia viongozi wa Tanecu ho kina Nannila.

Kama wameboronga wabadilishwe.
Sawa mkuu hii ndio maana tulikuwa tunashabikia kuvunjika kwa TANECU ili uchaguzi
ufanyike waingie viongozi wengine, maana tummchoka sana huyo NANNILA.


Pia huyo mkuchika unaemuona wa maana leo eti kwamba ni mkombozi wa kuivunja tanecu tuulize sisi tukueleza madudu aliyoyafanya N.D.F i.e Newala Development Fund.
Mimi nilikuwa nashabikia tu huo mpango wake kwani kwa namna moja ungetusaidia kupata viongozi
wapya ambao kwa namna moja au nyingine pengine wangekuwa tofauti na hao walipita.


Hakuna management NDF...

Hakuna ukaguz wa hesabu NDF...leo sisi tuwe wajinga kumruhusu aivunje Tanecu ili aiweke mfukoni mwake kama NDF??

Hilo waambie wasiojua...


Mkuu hata TANECU wanafanana na hao jamaa kwa muda mrefu wamekuwa hawatoi
ripoti zao za mwaka, hata baada ya kulazimishwa sana bado ripoti zao si za kweli
kwa kiasi kikubwa.


Sisi tunajua kinachoendelea hapo kiundani kabisa.

Na Tupo Imara kuilinda Tanecu.

By anymeans necessary ikibidi.

TUNAOMBA MSIMAME PIA KUHAKIKISHA WAKULIMA WANAPATA MALIPO KULINGANA NA BEI
YA MNADANI NA SI KUHAKIKISHA HILI ZIMWI LINAENDELEA KUTUNYONYA.
 
Sawa nakubali hoja zako.

Wako nnumbuwangu choonde.

Vanu vene tunilaga lagaaa...!!

Tukave na chinu ndulu nkanya piii...tuve na chani??

Mgomvi wetu tuni mmala ake kikwete ake Tanecu.

Mchawi wetu ni hawa viongozi wa Tanecu.

Tuwabadilishe tu.

Hatuwez kumlaumu kikwete wala hatuwez kuilaumu Tanecu kama chama cha ushirika.
Mnungu akajalia namwaka korosho ilembekupa, hambi aneyo ake hatari kweli?
Ake kuntajirisha Nannila aneko? akusanye dihela ja kummika mwanawe kuva MBUNGE wa
kutandahimba? Maana tunipilikana kuchi aneo ndo mpango wake.
 
Kama kuna rushwa na ubadhirifu TANECU ...Mh.Mkuchika ni waziri wa Utawala bora TAKUKURU iko chini yake sasa je kwanini asiwaamuru wakachunguze na kupeleka kesi mahakamani?

Wamiliki wa TANECU ni wanachama wa vyama vya msingi wanauwezo wa kuwawajibisha Viongozi wa TANECU kwa kuitisha ukaguzi maalum kwa kumwandikia Mrajis wa Ushirika barua wanapohisi kina ubadhirifu.. kulalamika tu pekee haitoshi chukueni hatua...
Kuhusu kupanga bei ya korosho mhusika mkuu ni BODI YA KOROSHO ambamo TANECU ni mdau hivyo lawama pia zielekezwe kwa bodi ya korosho ambayo inaongozwa na wanasiasa wengine ni wabunge wa huko kusini
 
Wanachama wa ushirika hawana ufahamu wa ushirika....TANECU na vyama vingine vya Ushirika na serikali pia wanawajibu wa kutoa elimu kwa wanaushirika kuhusu haki na wajibu wao...na kwa kuwa Ushirika ni hiyari manufaa yangepatikana zaidi.
Hali halisi ilivyo elimu ya ushirika ni finyu na ukiona wakulima wanalazimishwa kupitia ushirika ambao kimsingi duniani kote ni hiyari ujue kuna tatizo au/na maslahi ya fulani yanalindwa
 
kuna walakini mahali suala la waziri mwenye dhmana kushindwa kushughurikia mambo yaliochini ya wizra yake kisha useme kuko vizuri hapo????? hii ni sawa na ile ya mwakyembe kushindwa kujua kama UDA iko chini ya wizara ya uchukuzi..kweli kuishi tz kujonea mengi
 
Back
Top Bottom