Rais Kikwete ndiye aliyempeleka Lowassa UKAWA

Rais Kikwete ndiye aliyempeleka Lowassa UKAWA

Planner12

Member
Joined
Dec 29, 2012
Posts
76
Reaction score
59
WanaJF

Ukweli ni kwamba kushindwa kwa Rais Kikwete kukiongoza chama kumepeleke upenyo wa Mhasimu wake Edward Ngoyai Lowassa kutimkia Ukawa. Binafsi naona kwamba chama hakikujipanga kwa kuwa waliyokuwa wanayasema kwenye majukwaa na vyombo vya habari hawakuvitenda.

Hebu jiulize swali hili: Nnape Nawuye amekuwa MROPOKAJI mkuu na MSEMAJI MKUU wa chama. Kwamba anaharibu au anajenga hiyo siyo issue kwake cha maana amezungumza.

Nikawa najiuliza hivi huyu jamaa hakuna watu wanaoweza kufikiri zaidi yake? Maana kama anaenda kwenye vyombo vya habari na kutoa matamko ya chama basi ana baraka za wakubwa. Hili Prof. Dr. Jakaya Kikwete kama Mwenyekiti hakuliona.

Lowassa amekuwa kwenye chama kwa muda mrefu. wamemtuhumu lakini tuhuma zake mpaka leo hazijathibitishwa. Nape amekuwa akitoa kejeli na maneno ya maudhi kwenye mitandao. Mara ukitaka kumuua kobe lazima ufanye timing, huwezi kuzuia mafuriko kwa mikono na kadhalika.

Maneno haya yanaashiria njama ambazo tayari zilishaandaliwa kuhakikisha Lowassa hatoboi. Lakini vijana wadogo kama kina makonda wamekuwa na sauti kubwa na za kutukana na kukashifu. Hili Kikwete hakuliona. Tunajiuliza hivi Lowassa ndiye mwovu, mchafu, mwizi, fisadi, asiye na adabu, kuliko wanachama wote wa ccm? Msigwa aliwaambia bungeni "Can't we think a little bit more" "Can't we stretch our minds a little bit"

Ni mwanamke gani duniani ambaye akili zake ni timamu ambaye anaweza akazaa mtoto akamvua nguo akamwacha barabarani kisha akaenda kujifu eti on mtoto wangu nilivyomwacha uchi. akafie huko mbali pumbavu!!! Hii ndiyo CCM tunayoifahamu. Kwamba Lowassa can't be cleansed!!! Really!!!

VISA, UBINAFSI na CHUKI haya yote yamechangia kuhakikisha Lowassa anatoka CCM. Kikwete kashindwa kudhibiti haya kwa kuwa na yeye hakutaka huyu mzee kuingia ukulu kwa chuki binafsi. Swali la kujiuliza ni je; kumtupa nje ya mfumo[system] ndio kumdhalilisha, kumdharau, au kumchafua? Je; sio wamemfungulia njia rahisi kabisa ya kujiweka wazi kwa wananchi na ikifika mwisho msemo huu ufuatao utawale "JIWE WALILOLIKATAA WAASHI LIMEKUWA JIWE KUU LA MSINGI?"

Naomba kuwasilisha.
 
Atakayeiua ccm atatoka ndani ya ccm by mwalimu Nyerere.
 
nataka nimuone riz 1 akifa pale alipotamka rais hawezi kutoka kaskazini .alitumia lugha ya kiukabila na kimsingi hili lingekuwa rungu LA kumnyima kugombea ubunge tusiwe na wabunge wabaguzi.Kwa hili wakuu wake hawakuliona .
 
kuna wakati mwingine hakuna haja hata ya kutumia akili nyingi sana kujadili mabadiliko, ktk kipindi hiki hata kama kikwete angemsaidia lowasa kuwa mgombea kupitia ccm bado kungekuwa na mabadiliko makubwa tu, kama sio urais basi ubunge na udiwan bado ilikiwa issue. Jinsi dunia inavyokwenda huwezi kuzuia mabadiliko kwa kubebana, zama za mvuto zimeishiwa na wakati watanzania wanataka mabadiliko chanya na sio ahadi za majukwaani, naamini hata kama lowasa angesimamishwa basi kuna watu wengi pia wangeasi ccm na bado upinzani ulikuwa na nguvu ya kuleta ushindan mkubwa, wamefanya hivyo kwenye serikali za mitaa bila lowasa. Kikwete hata kama angefanya nini badoabadiliko yangekuwepo tu.
 
Nyoka akiingia nda unampiga na chochote unachoweza kufikia bila kujali ni kitu gani.
 
Hakuna kipindi kibaya kwa CCM kama hiki,hakuna kipindi au utawala maadili ya uongozi yalishuka kama wakati huu..Huyu huyu Kikwete aliruhusu maraisi na viongozi wastaafu kudhalilishwa na vijana kama kina Makonda kwenye vyombo vya habari na mitandao,huku mwenyekiti akicheka na kutabasamu..!!!CCM ilimfia mikononi Kikwete tangu mwaka 2010 lakini kwa ukarimu wa wazee na waungwana wengine wenye mapenzi ya kweli na chama kama Lowassa walikuwa tayari na kumsaidia kwa mara ingine huyu jamaa
Ukitaka kuthibitisha maneno yangu tembea na kauli za Kikwete mahala popote,ni mtu ambae tayari anajua wapi chama kimefia na nani muasisi wa kifo hicho,hujiwahi kusema anaacha nchi ikiwa salama/chama kikiwa na umoja na mshikamano wakati kiuhalisia mambo ni mabaya na hata wananchi wakawaida wasio jua kiundani siasa wana ng'amua katika hili!!
 
nataka nimuone riz 1 akifa pale alipotamka rais hawezi kutoka kaskazini .alitumia lugha ya kiukabila na kimsingi hili lingekuwa rungu LA kumnyima kugombea ubunge tusiwe na wabunge wabaguzi.Kwa hili wakuu wake hawakuliona .

Babake mwenyewe ana hubiri haya mambo ya ukabila na udini,hapo inaonyesha kikwete ni mnafiki namba moja yeye ndio chanzo cha udini na ukanda
 
Ccm wanawezaje kusema Lowasa ni fisadi sasa wakati siku ya kutangazwa magufuli Kikwete alimsifia?!
 
Huyo ni mhitimu wa sheria na mtoto wa rais lakini anaongea kama mtoto wa mtaani na kuna wakati mwingine ninajiuliza huyu kijana kama kweli yeye ni msomi au ndiyo hivyo tena aina ya watoto kama hawa huwa hawafeli
 
Asije akafikiri kwamba hii ni Nchi ya familia moja ya Kikwete
 
Back
Top Bottom