Rais Kikwete na safari za nje

Jamani acheni asafiri...
Anacho kifanya Jk Kimataifa Ni Ki-zuri sana..Kwakweli Bado Nia imani nae kwa 70%---Nina mpenda JK...
 
Mapenzi na mtu huwa yanaondoa objectivity... kwa msingi huo; Gigo's father, weshould not take you seriously!

Investmentment za kweli kweli ni zile zitakazotokana na waTz, na isitoshe...hata huko nje akiende huwa hajajiandaa, kuna mkutano mmoja nilikuwa naye SA, when it came to issues of the economy.....jamaa ni mweupe, alishindwa kabisa kutetea hoja zake! Sasa mimi nikaona huyu jamaa afadhali hiyo embarassment basi zingekuwa kwa mawaziri...lakini kwa Rais wetu? Its pitty! Halafu akafanya kosa la kutumia urafiki kuchagua waziriwa fedha ambaye hata story za Demand and Supply inabidi aelezewe kabla ya kwenda mikutanoni...is this fair to a country ambayo ina wachumi lukuki?

JK, endelea kutembea...maana hilo ndilo uwezalo!
 
Mimi Nilivyo Muelewa Kikwete..
Na Ninavyo Muelewa JK ..
Ni kwamba- ana waamini sana watu.anajaribu kumpenda jirani yake kama Nafsi Yake..Hili si Kosa!!..tena ni Mafano mazuri..Huyu ni Mwalimu-Anawapenda sana watu- !! Hapa ana tufundisha Kusafiri- iwe ni sehemu ya utamaduni wetu..

Iliaweze kuelezea Hisia Zake, Hana budi kuwa-amini..wananchi na viongzi wanao mzunguka..
Sasa Kama watamdanganya Basi ..Si yeye atakae Aibika..Kama jambo hajui Akikuhusisha Kuna ubaya gani? sasa nashangaa watu HUMU wana-furaia-Pale anapo taka kushindwa..Inashindikana kwasababu..anao waamini..wana sauti ya Uongo...

Kwamfano Dito..Hakika hakua Mkweli tangu-zamani...Hakua mkweli hata kwa Muheshimiwa JK..Sasa Ona anavyo aibika!!

Wapo wengi..Watakao aibika..Kama si kizazi hiki basi Kizazi kinacho fuata..Mfano Magufuli-sijui ni kweli!!? Mbona Hasemi lolote kwenye media..

HakikaMzee enendelea kusafiri Ikibidi..

Najua Kazi ni ngumu!
Mungu akipenda Tutafanikiwa!!..Usibague mtu..kama uanavyo taka.. wao wenyewe watashindwa..Kwanini tushindwe kwani tuna makosa gani?

Hayo tulio nayo Tuyarekebishe..Tusamehe ili nasisi tusamehewe,,


Watu wanaaibika-.kwasababu Ya kuendekeza tabia Kama za mwanagu Gigo..

Watu wamechanganyikiwa -Watoto wame changanyikiwa-kwasababu wanayo yasema Wabunge si sawa na wanavyo wafanyia kwenye Magest Kule Dodoma..

Ok... Nikirudi Kwenye Safari za kikwete
Madhala ya safari hizi Utaona zina wapa nafasi sana wakina Gigo,Dito....Nk Kua huru.. Kwasababu hata wakitukana -Hawajari Raisi si ha-yupo?

Sijui Naeleweka?
 
Unaongea nini? Kweli hauko serious.

Hatuwezi kufanya mambo kwa kubahatisha. God is always looking for every1. All we have to do is to get our acts together. So if we keep doing this every time a new leader comes to power, we will be sorry on the outcome.
 
Wewe sirious..Mbona una sauti ya kulaumu..
Ulitarajia nini kutoka kwangu?

Kumbuka haya mambo Yanagengwa taratibu....Ina hitaji mafundi wengi...
lakini napenda kuku shukuru kwa ushauri wako!!
Asante sana Tatu..
 
Najua kuwa duniani kuna nchi karibu 245. Je Mzee atatembelea nchi zote hizo kujitambulisha ? Kwa vile safari kwa kila nchi inachukua takriban siku nne, kwa wastani huo Mzee atatumia karibu siku 1000 kwa kujitambulisha nje ya nchi tu. Hiyo roughly ni miaka mitatu hivi kati ya miaka mitano ya kipindi chake cha kwanza cha utawala. Huoni kuwa atakuwa ametumia muda wake vibaya badala ya kutatua matatizo ya nchi.
 
I think we need a system kama Mexico where the President's foreign trips have to be approved by the senate....like this story...are some of those trips really necessary? Should the people know the costs of each trip? I think it should be open to debate.


Mexican president is forbidden to travel

By E. Eduardo Castillo
Associated Press

MEXICO CITY - President Vicente Fox's press secretary Wednesday urged constitutional reform to let Mexican leaders travel abroad without congressional approval, a day after lawmakers irked Fox by blocking his planned trip to Australia and Vietnam.

Fox's press secretary Rubén Aguilar harshly criticized the legislators for their decision, which came amid rumors that Fox was going to Australia to visit his daughter. Aguilar decried ``the pettiness of Mexican political life,'' marked by ``childish positions that speak of a low level of discussion.''


``This administration believes that this article of the constitution has to be reformed because it causes unwarranted tension between the executive and legislative branches,'' Aguilar said.


The lower house of Congress voted 258-187, with six abstentions, to deny Fox permission for an official visit to Australia on Nov. 12-16. From there, he was to have traveled to Vietnam for the Nov. 18-19 Asia-Pacific Economic Cooperation summit.


The Senate approved the trip, but either chamber can block it.


The trip would have been Fox's last international trip. He leaves office Dec. 1.


Legislators said they were upset that Fox wanted to travel abroad as a political conflict in the southern state of Oaxaca continued to smolder and small bombs presumably planted by guerrilla groups exploded Monday in Mexico City.


Fox went on national television Tuesday night to express his disappointment in the lower house's vote, saying it ``goes against Mexico's interests'' and was ``clearly partisan.''


Fox singled out Mexico's opposition parties for criticism, particularly the Institutional Revolutionary Party, or PRI: ``I regret that lawmakers from the PRI refuse to listen to the voice of the people and aren't capable of acting responsibly to resolve local conflicts.''


That was an apparent reference to the refusal of the PRI governor of Oaxaca to heed calls to step down. Protesters have demanded the governor step down for months, sparking unrest that has left nine dead and driven tourists away from one of Mexico's top tourist destinations.


The PRI leadership called Fox's accusations ``offensive and baseless.''


Fox's statement ``constitutes an unacceptable discourtesy and an unforgivable challenge to the powers'' of the lower house of Congress, the PRI's national executive committee said.


It was the second time Congress has exercised its constitutional power to block one of Fox's trips. In April 2002, the lower house denied Fox permission to travel to the United States and Canada, saying he was focusing too much attention on international events.
 
Kwanza nampongeza Rais kwa kutambua umuhimu wa wafanyibiashara kuwa katika misafara yake.

Nashauri serikali kufanya jambo la ziada katika misafara hii ,wafanyibiashara wawezeshwe kwa kulipiwa sehemu ya gharama ya safari na vile vile wapewe majukumu ya kuhakikisha wanaleta manufaa kwa taifa. Wafanyabiashara waangalie zaidi katika kutumia nafasi ya kusafiri na Rais kukaribisha wawekezaji katika nyanja zenye faida hasa uzalishaji.

Ni aibu kushindwa kutumia nafasi ya rais kuleta biashara ya kunufaisha taifa. Naomba Rais aagalie katika msafara wake watu kutoka serikarini wengi wao ni kwa ajili ya mafao wanayo pata kutokana na posho hawawezi kutuambia ni faida gani wanapata ili watu wengi wafaidi kutokana na safari hizi.

Wafanyabiashara ni wawakilishi wazuri wa taifa kama watasaidiwa kwa nguvu zote,pia baada ya safari waeleze ni faida gani imepatikana kwa tukitilia mkazo ajira, uzalishaji kwa kutumia mali ghafi ya hapa nchini na kuongeza uuzaji wa bidhaa zetu katika soko la kimataifa.

Wafanyibiashara wa kitanzania tunapaswa kubadilika na kuachana na biashara ya uchuuzi tuangalie uzalishaji, kama kusafiri na Rais ni kwenda kutafuta uchuuzi hakufai kazi hizo zinafanyika kupitia internet . Tubadilike tutumie nafasi ya Rais kuleta viwanda, tekinolojia na mbinu za kisasa kukabiliana na ushindani tuachane na safari za kutafuta sifa.Taifa linatuhitaji sana kubadilisha maisha ya watanzania kwa kuleta ajira ili kusaidia Rais wetu kuleta maisha bora kwa watanzania. Tuwe na sauti ya kumwabia Rais atugharamie safari hizi na tuhakikishe safari zinaleta manufaa .Duniani kote wanasiasa wanatengeneza uwanja mzuri wa kufanya biashara hivyo basi tutumie nafasi hii kuleta manufaa kwa taifa letu tuachane na biashara ndogondogo.

Namalizia kusema safari za Rais Kikwete zinamanufaa kwa taifa.
 
Safari za JK hazina manufaa kwa TZ badala yake zinaongeza ufujaji wa pesa za walipa kodi.

Anatakiwa alimarishe uchumi wa ndani, utawala bora,na kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji wa ndani, mwekezaji sio lazima atoke nje ya nchi. Nchi yetu inakabiliwa na corruption ya hali ya juu, sasa mwekezaji gani mwenye akili atakuja kuwekeza TZ katika mazingira kama hayo?

Sasa ni mara ya pili tangu aingie madarakani anaenda kujitambulisha Uarabuni, kunani huko Uarabuni? Tunao mabalozi wetu karibia kila nchi kwa nini wasitumike hao kuitangaza TZ badala ya JK kwenda mwenyewe?Au anafikiri yeye bado ni waziri wa mambo ya nje?

Tangu aanze ziara zake kila siku tunasikia ahadi lukuki kutoka kwa MAULA Mwingira kila anapoenda JK lakini utakekezaji ni sifuri.Je baada ya ziara zake ndefu za nchi za magharibi USA na kwingineko alishakaa chini na kutathmini nini amepata na nini amekosa?Je kulikuwa na umuhimu wa kwenda USA na msafara wa watu zaidi ya 70?. Huu ni ufujaji mkubwa wa pesa za walipa kodi, mungu ibariki TZ.

Kwa kifupi safari za JK hazina manufaa kwa Tanzania.
 
Tumpe muda JK aendelee na safari zake za nje hadi Dec 31, 2006 halafu aje atupe feed backs ya kila alikotembelea. Kama mswahili mmoja alivyotaja hapa, inaelekea kweli JK hakupata fursa nzuri ya kutembelea marafiki (pen pals) aliojipatia wakati akiwa waziri wa nje.
Kukaa kwake nje sana kutakuwa dili kwa vyama pinzani mwaka 2010.
Si unaona Dito alijua kuwa Boss hayupo ndo maana aka..
 
epictanzania,
Hivi wafanyibiashara hamwezi kujilipia wenyewe safari zenu? Mnapotajirika mnawagawia walalahoi fedha zenu?
 
wafanyabiashara wa nje huwa hawangoji ziara za rais ,wanatumia ipasavyo information technology,kwa mfano wiki ijayo wafanyabiashara wa malaysia wanakuja bongo ...wao wameingia kwenye yellow page yabongo na wmehakikishia wanamtumia mualiko kila mfanyabiashara aliye kwenye yellow page kutokana namahitaji yao so wanayotaarifa [business inteliigence],hawaendi tu? nha wanahakikisha wanakupigia personelly kukukumbusha ...balozi yake kazi yake anapanga appointment ya man to man kwa kila mfanyabiashara kwenye delegation ..kwa kushirikiana na hamber of commerce.

sasa tatizo la wafanyabiashara wanaoambatana na jk ni wasanii tu ,,sioni mtu kama bakhresa na wengine wa aina yake wakienda ,,,wanaenda watu ambao kwa kweli hawana experince ,mimi naomba tuwe na list ya wafanyabiashara angalao 100 wazawa kila wakati[wanaopanda na kushuka ]ili rais anaposafiri angalao tuwe nakigezo sio watu wanapeleka mashogga zao.

sasa jana jk amerudi tunapenda atuambie tumefaidika nini...zaidi tuliona mabegi yamejaa tu yanashushwa kwenye ndege yetu ya kifahari gulfstream si mnajua tena HB wetu wa vimwana.
 
Phillemon,
mabegi yamejaa cell phones. Si unajua anavyopenda kuwazadia vimwana wake?
 
Mawaziri watetea safari za Kikwete

Ramadhan Semtawa na Elizabeth Mjata

MAWAZIRI wawili wa serikali ya awamu ya nne waliokuwa wameongozana na Rais Jakaya Kikwete katika nchi za mashariki ya mbali, wamezitetea ziara za Rais nje ya nchi, wakisema zina manufaa makubwa kwa taifa.

Wakati Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha Rose Migiro alisema ziara hizo zina manufaa makubwa kiuchumi na kidiplomasia, Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Basil Mramba, aliwabeza wanaopinga ziara hizo.Akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusiana na wingi wa ziara hizo, Dk Migiro, alisema Rais hawezi kufungwa miguu kwa kukaa Ikulu.Alifafanua kwamba Rais Kikwete alishinda uchaguzi kwa kutumia ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), hivyo lazima aende nje kutafuta njia za kutekeleza ilani hiyo.


Waziri Migiro aliongeza kwamba, hadi sasa haionyeshi kwamba Rais Kikwete amefanya ziara nyingi, ikilinganishwa na umuhimu zaidi wa kufanya ziara hizo."Kwanza labda niseme, hadi sasa Rais hajasafiri sana nje, bado anapaswa kusafiri zaidi ajitambulishe na pia kueleza sera na msimamo wa serikali yake, ikilinganishwa na zilizopita," alisema Dk Migiro na kuongeza:


"Lakini pia Rais hawezi kufungwa miguu kukaa Ikulu, amechaguliwa na wananchi kwa kutumia ilani ya chama, hivyo lazima angalie njia za jinsi ya kuitekeleza."Dk Migiro alisema kila nchi duniani inapoona kuna mabadiliko ya uongozi katika nchi fulani, huwa inataka kujua msimamo wa serikali mpya iliyoingia madarakani.


Akifafanua zaidi, Dk Migiro alisema Tanzania nayo imekuwa ikiongozwa na serikali tofuati tangu uhuru na imekuwa ikitekeleza mambo tofauti, hivyo ni lazima Rais Kikwete azihakikishie nchi rafiki kwamba atadumisha uhusiano uliokuwepo tangu uhuru.Katika kuelezea mafanikio ya ziara ya Rais kuanzia Oktoba 19, Dk Migiro alisema imekuwa na manufaa makubwa kuanzia Japan, China, Korea Kusini, Dubai na Falme za Kiarabu.


Kwa upande wake, kwa wakati tofauti, Waziri Mramba alitumia nafasi ya kuelezea mafanikio ya ziara hiyo, kumtetea Rais Kikwete kuwa amekuwa akitumia fedha nyingi katika ziara badala ya kutatua matatizo ya ndani, aliwashangaa wanaotoa shutuma hizo."Nawashangaa watu hawa, Rais Kikwete ana haki ya kwenda nje ili kuzungumzia masuala ya uchumi wa nchi yake na ikiwezekana apate wafadhili ambao watasaidia uchumi wa Tanzania kukua," alisema Mramba.


Mawaziri hao wametoa kauli hizo ikiwa ni miezi kadhaa baada ya Waziri Mkuu, Edward Lowassa kuutangazia umma wa Watanzania kuwa ziara za Rais Kikwete ni za manufaa kwa Watanzania, kwani amekuwa akipata misaada ya kutekeleza miradi mbalimbali, ikiwemo ujenzi wa miundombinu.Hatua ya mawaziri hao inafuatia kauli za Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, aliyesema Rais Kikwete amekuwa akisafiri zaidi nje kuliko kuangalia matatizo ya ndani.


Akizungumzia baadhi ya mafanikio hayo, Dk Migiro alisema ni pamoja na China kukubali ksaidia ujenzi wa barabara Maangaka-Masasi yenye urefu wa kilomita 54 ambao utaanza rasmi mwaka 2008.Alisema manufaa mengine kutoka China ni mkopo nafuu wa dola za Marekani 20 milioni (Sh25 bilioni) kwa ajili ya kusaidia bajeti ya maendeleo katika Mpango wa Taifa wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini (Mkukuta) na fedha za ujenzi wa barabara ya Arusha-Namanga.


Kwa upande wa Dubai na Falme za Kiarabu, alisema zimeonyesha nia hasa kwa wafanyabiashara wake kuja kufanyabiashara nchini na Japan imeonyesha nia ya kusaidia miradi ya maji mijini na vijijini, hasa Zanzibar.Kwa upande wake, Mramba alisema Wafanyabiashara wa Urusi wanashindwa kuja kuwekeza nchini kutokana na kukosekana kwa hoteli za kutosha na vyakula vya Kirusi.Alisema kutokana na hali hiyo, wizara yake imejitolea kuwasaidia wafanyabiashara wote ambao wanahitaji kuwekeza katika sekta ya hoteli kujitokeza kwa ajili ya kuunganishwa na wawekezaji kutoka nchi hizo.


"Wafanyabiashara wa Urusi na wengine wengi wanataka kuja hapa, lakini wanakumbana na kikwazo cha makazi na vyakula," alisema Mramba.Waziri Mramba alisema akiwa Japan, pia alipata malalamiko ya aina hiyo, kwani baadhi ya wafanyabiashara walikuja kama watalii na kushika nafasi kwenye hoteli moja nchini, lakini mwezi mmoja kabla ya safari yao, walitumiwa taarifa kwamba hoteli haina nafasi.


Alisema katika ziara hiyo, wamekutana na wafanyabiashara mbalimbali ambao wana uwezo wa kuwekeza katika sekta mbalimbali, lakini tatizo Tanzania imeshindwa kufikia vigezo wanavyotaka, ikiwamo miuondombinu.Aliwataka Watanzania watakaotaka kufanya biashara na wenzao wa Urusi kufika wizarani kwake, ili kuwaelekeza jinsi wanavyoweza kukuza biashara ya Tanzania na pato la nchi.Mramba, alisema wamebaini China walivyo na uwezo mkubwa wa kutengeneza umeme kwa kutumia vyanzo mbalimbali kikiwemo upepo. Tanzania ina sehemu nyingi ambazo zina upepo mkali.
 
There is really no point to such an excessive number of trips, these ministers are defending them because they themselves make good money on these trips. Some of these could have easily been made by Ministers, Principle Secretaries, Ambassadors etc on behalf of the President. I think it just reflects his nature of loving the five star treatment. Msishangae kama hataenda Fiji kutafuta wawekezaji.
 
jasusi.

wakati wa mapokezi small house aliingia na vogue range rover new model[namba...]wapambe wakapakia mabegi ya zawadi ,,,ndio mafanikio ya ziara ,,welll wanotetea wanasema pamoja na zipu clinton alifanikiwa kuliko bush muhafidhina,...so lets wait and see ,,.na presida wetu atafanya nini...
 
phillemon mikael said:
jasusi.

wakati wa mapokezi small house aliingia na vogue range rover new model[namba...]wapambe wakapakia mabegi ya zawadi ,,,ndio mafanikio ya ziara ,,welll wanotetea wanasema pamoja na zipu clinton alifanikiwa kuliko bush muhafidhina,...so lets wait and see ,,.na presida wetu atafanya nini...

Hivi kumbe bado hajaacha mambo hayo, watu walisema akikua ataacha. Je huwa anafanyia wapi siku hizi, kwa vile askari wanatakiwa wamzunguke? Zamani zile akiwa waziri wa fedha alikuwa akionekana na mavitusa kwenye mitaa mablimbali na hasa zaidi kwenye mojwapo ya hotel za pale Sinza.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom