Rais Kikwete kuongoza maziko ya Regia Mtema!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,
Tuendelee kupeana pole kwa msiba huu wa Regia, Rais Jakaya Kikwete, atawaongoza umma wa Watanzania katika maziko ya mpendwa na shujaa wetu Regia Mtema yatakayofanyika Ifakara siku ya Jumatano.

Kwa mujibu wa ratiba ya ziara ya rais Kikwete mkoani Morogoro, ratiba hiyo inaonyesha rais Kikwete atahudhuria maziko hayo siku ya Jumatano.
 
Marehemu atapata Heshima inayomstahiki kama mmoja wa Viongozi mashuhuri Vijana wa Watanzania.

RIP Regia!
 
Teh teh teh...JK bana!

Haishiwi vituko, lakini anaoneakana kuwafahamu watanzania vilivyo, at least kwenye nyanja flani.

Toka ile siku viongozi walipoenda Ikulu kunywa juisi or something, halafu JK akawageuzia kibao, basi nilijuwa huyu jamaa kwa politics ni kiboko.

Unaweza kushangazwa na the fact kuwa tendo hilo linaweza kuwapatia washabiki na wanachama wawili watatu ambao kwao si haba usawa huu...
 
Ni heshima kwa kamanda wetu marehemu Regia, lakini jk angetumia muda mwingi kuinua uchumi kama anavyotumia muda mwingi kwenye misiba nchi ingekuwa mbali
 
Kama pilau inanunua kura na wao wanajuwa, simpathy kama hii pia inawezekana inawapa wanachama,mambo ni mbaya kwa wenye njaa na kunako psychological warfare ndo masters hao gambas...
 
tayari umeshaupata u-Salva mkuu pasco??!!.......hahaha haya bwana ...
 
Ibada ya mazishi ya kamanda Regia itaongozwa na Paroko/Padre au Askofu wa Kanisa Katoliki.Baba,Mama Dada,Bibi,Viongozi wa CDM na Rais Kikwete pamoja na viongozi wengine wa Chama na Serekali watahudhuria katika Ibada ya mazishi ya mpendwa wetu Regia.
 
JK anashiriki misiba mingi sana na kwa hilo mimi siwezi kubania kumpa hongera zake.

Bado sijapofushwa na unazi au itikadi za kisiasa hadi kutoona hata yale mema ambayo mtu uliye tofauti naye anayafanya.

Ni jambo jema kabisa lisilo na ubaya wowote ule.
 
Nyie chekeleeni tu wenzenu wanakula vichwa...

Marehemu huwa wanagombaniwa hata kwasababu za kidini let alone za kisiasa.

Ndo bongo hii!
 
Viongozi wa CDM waliangalie hiklo, JK anatafuta kujikweza hapa baada ya mambo mengi ya nchi kumshinda. CDM wasimruhusu JK ku-steal the show katika shughuli hiyo na wajaribu kumbana kidogo aonekane kama ni muombolezaji wa kawaida tu. CDM wajitahidi kuonyesha kwamba huu msiba ni wa familia ya Regia, Chadema na Bunge, kwa mpangilio huo.
 
JK anashiriki misiba mingi sana na kwa hilo mimi siwezi kubania kumpa hongera zake.

Bado sijapofushwa na unazi au itikadi za kisiasa hadi kutoona hata yale mema ambayo mtu uliye tofauti naye anayafanya.

Ni jambo jema kabisa lisilo na ubaya wowote ule.
Kwenda kwenye misiba kama hiyo ingekuwa sawa na utendaji kwa maslahi ya Taifa basi tungekuwa mbali sana!

Haya mambo ya kisiasa si sawa na mambo ya kifamilia, tunataka kuona ushirikiano bora kati ya viongozi kwenye kutuletea maendeleo, na hayo mengine ya msiba, harusi nk, yatakuwa ya ziada tu.

Hii PR yote ni kwasababu wanataka tu kunufaika kisiasa mbele ya macho ya watanzania, lakini ukweli uko wazi, wangekuja pamoja nyakati zote na si za msiba tu.

Hapo ndo msimamo wangu ulipo, kwamba amekwenda na ni jambo jema, yes, but...
 
I still don't see what/where the problem is!
 
Back
Top Bottom