Rais Kikwete, baba mbakaji na utata wa mtoto aliyezaliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete, baba mbakaji na utata wa mtoto aliyezaliwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mikael P Aweda, Nov 28, 2011.

 1. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #1
  Nov 28, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wanajf,

  Hivi mama yako akikuambia kuwa baba yako alinibaka, nikapata mimba, ndo ukazaliwa wewe mwanangu X. utamkana baba yako hata kama ubakaji ni kosa la jinai? Huwezi kumkana baba yako kwa sababu huo ndio ukweli ambao huwezi kuubadili. Baba yako ni baba yako bila kujali alimtongoza mama au alimbaka. Hakuna mahakama ya kubadili ubaba wa baba yako.

  Nimekuwa nikijibu shutuma na propaganda nyingi zinazoelekezwa kwa makusudi au kwa kutojua kuhusu Chadema kumtambua au kutomtambua Rais. Propaganda hizi zimekuja hasa baada ya Chadema kwenda ikulu kuongea na Rais na kujadili mstakabali wa Taifa na kuepusha mgawanyiko wakati huu tunapotunga sheria itakayoongoza uundaji wa tume na uandikaji wa Rasimu ya katiba mpya. Nimekuwa nikijibu thread za namna hii, lakini nimeona niiweke ktk thread inayojitegemea ili nijibu once and for all.

  Na bahati nzuri nina open ID ambayo ukitaka waweza kunipigia simu au kuniandikia email kwa maelezo zaidi.

  Je, baada ya Chadema kuwa na uhakika kuwa kura zao zimeibiwa (mimi nina ushahidi wa jimbo la ubungo) na baada ya Rais kutangazwa na tume ya Taifa (ambao mpaka leo wameshindwa kuweka vizuri ktk website yao ya Tume) Chadema wangefanya nini?

  Kwa mujibu wa katiba hii mbovu, kikwete ni Rais mara tu baada ya kutangazwa na tume ya uchaguzi Mbowe na Slaa watake, wasitake. Hakuna mahakama ya kupinga kutangazwa kwake na sijasema ushindi wake. Ieleweke hivyo. Kwangu mimi mshindi ni Dr Slaa, japo huu ndio ukweli mchungu.

  Chadema hajawahi kusema hawamtambui rais, na hawawezi kufanya hivyo kikatiba, ila waliwahi kulalamika baba yao ( Rais) kubaka demokrasia akisaidiwa na tume ya Uchaguzi na usalama wa ccm (Taifa?) na kuzaliwa mtoto( Rais). Mtoto hana utata ila njia iliyotumika ndio tatizo ( ubakaji wa demokarasia)


  Tuache ushabiki, nchi yetu iko ktk hali tete sana kuliko wakati mwingine wo wote. Tunahitaji hekima na uvumilivu wa hali ya juu.

  Niliwahi kusema na narudia.

  Kama Dr Slaa angetangaza kuwa nina taarifa za uhakika kuwa kura za Chadema zinaibiwa kwa hiyo watu waingie barabarani, hivi leo huyo Kikwete angekuwa ikulu? Kama jibu ni ndiyo, basi makamu wake angekuwa Dr Slaa siyo Gharib Bilal. Hii ni baada ya damu nyingi za watanzaniakumwagika sana.

  Ifahamike tofauti kati ya Raila Odinga wa Kenya na Dr W Slaa ni uvumilivu. Raila aliwaambia watu waingie barabarani, Dr Slaa alivumilia akaweka Tanzania mbele kuliko urais. Wagombea urais wangapi Tanzania na Afrika ambao anapewa ushahidi wa jinsi kura zao zinavyoibiwa, halafu akakubali yaishe kama Dr Slaa?

  Inasikitisha viongozi wa dini zote waliokuwa wanamshauri akubali matokeo hayo tata, leo wako kimya na wengine wako busy wanajenga ccm makanisani na misikitini.

  TIME WILL TELL
   
 2. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #2
  Nov 28, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mwambie alete ushahidi
   
 3. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #3
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Dr slaa hakuibiwa kura na kama angeibiwa kweli asingekubali kirahisi hivyo ni propaganda tu za kisiasa kutafuta umaarufu
   
 4. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #4
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  tatizo lako hutaki kukubali kwamba Dr slaa alishindwa kwa sababu wewe ni chadema unajenga hoja dhaifu badala ya kumwaga ushahidi hapa unaosema unao. Haitoshi tu kusema tume na Usalama wa taifa waliiba lete hapa takwimu za majimbo yote ya tanzania na eleza jinsi ccm walivyoiba. tumechoka na wimbo huu
   
 5. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #5
  Nov 28, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  Huu ulinganisho hauingii akilini kabisa....hebu jaribu mfano mwingine
   
 6. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #6
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Hata kama dr slaa aliamua kuwa mvumilivu lakini bado anawajibika kwetu watanzania kuweka ukweli wazi wa alivyoibiwa kura na takwimu sahihi badala ya kila siku kutaja waliowaibia. Kutaja hata mimi naweza kutaja ni jambo jepesi
   
 7. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #7
  Nov 28, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  pipijojo david cameroon amekutetea sana lakini tanzania hiyo kitu haiwezi kukubaliwa kamwe.
   
 8. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #8
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  baba huwezi kumkana lakini unaweza kuvunja mawasiliano na mahusiano naye hadi kaburi
   
 9. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #9
  Nov 28, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu mbona ueleweki utaka kusema nini unachosema, mfano wako ni dhaifu sana.

  Kuhusu Dk Slaa na mtazamo wako ni hadithi za Abunuasi na mke wake Elizabeti, eti angetangaza watu waingie barabarani saizi angekuwa Makamu wa Rais.

  Mtazamo na muelekeo wako kisiasa na wasiwasi nao
   
 10. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #10
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  hata CUP ambayo ni CCM - B walianza hivyo hivyo wakilalamika huku wakipuliza mwisho wakanasa. Walianza kwa mazungumzo kati ya karume na Seif sharif Ikulu ya zanzibar.
   
 11. M

  Mzee Madoshi Senior Member

  #11
  Nov 28, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Inaonekana lengo lako ni kufafanua kwa nini uongozi wa CDM kwa sasa umeamua kufanya ilinachokifanya sasa, ila umeshindwa kutoa mfano wenye nguvu wa kuitetea lengo hilo.

  Kwanza kabisa Kenya, Misri, Libya au Syria haviwezi kukupa picha linganifu na Tanzania yenye Zanzibar ndani yake, Pili kutaka kuulazimisha umma kwa 'proof' ulizonazo wewe tu bila kuziweka hewani kunaidhoofisha sana hoja yako, na tatu nafikiri umeandika kiushabiki zaidi, ni sawa na kusema 'mimi ndio ninayejua, na mimi ndie ninaeujua na kuusema ukweli na ukweli ndio huo either mnakubali au hamkubali.

  Hii inamaanisha ukweli unaoujua wewe hauwezi kubadirika. Ushauri, jaribu kupitia upya lengo lako, na jaribu kuelezea tena
   
 12. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #12
  Nov 28, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,146
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  tunamshukuru dr.slaa kwa kutanguliza utanzanzania mbele.
   
 13. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #13
  Nov 28, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,158
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Samehe 7 mara 70 = 490
   
 14. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #14
  Nov 28, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,507
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Namnyonga baba na kama ikishindikana nampiga risasi ya ****
   
 15. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #15
  Nov 28, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  x akisema piipijojo mwizi na akatangaza ktk vyombo vya habari, nani anapaswa kutangulia mahakamani au nani amechafuliwa? Kwa maoni yangu Kikwete na CCM ndo waliopaswa kwenda kwa ndo waliochafuliwa. Wamekaa kimya pamoja na magazeti kuweka habari hiyo ukurasa wa kwanza kwa kuwa wanakubaliana na ukweli ambao hawawezi kuupinga - waliiba kura. La sivyo, Dr Slaa angeshashtakiwa.
   
 16. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #16
  Nov 28, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,571
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  umekuwa addicted na uchadema hata kufikiria unashindwa.......unamfananisha slaa na odinga?

  chadema vituo vingine hamkuweka wagombea na vituo vingine hamkuwa na mawakala, kusini hamkupiga campaign yet mlishinda urais.....utatukanwa siku nyingine!
   
 17. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #17
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mdada/Mkaka Hii CUP ni nini? Au kuna Chama kipya cha Siasa kimeanzishwa!
   
 18. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #18
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mkuu Wab,

  Mbaya zaidi badala ya kwenda maeneo ambayo CDM hawajawafikia wapiga kura wamekazana kila siku Arusha !.Pwana na kusini ndiyo maeneo yakutembelewa ianzishwe operesheni nyingine kama Sangara.Tazama uchaguzi wa mwaka 2010 Igunga hawakuweka mgombea kama kusingekuwa na uchaguzi wangesubiri mwaka 2015.   
 19. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #19
  Nov 28, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0


  1 Mkuu nchi zote ulizotaja hawakuingia barabarani wote, miji michache sana, hasa kenya ni rift valley, na Nairobi ndo walioleta machafuko yote. Unadhani kenya yote ingeingia mtaani wangekufa idadi ndogo kiasi hicho - 1000 na kitu?

  2 Hoja yako ya pili na tatu zinafanana,
  Tume ya Taifa ndo iliyopaswa kuweka matokea ya nchi nzima na pia jimbo mmoja baada ya jingine. Mpaka wanamtangaza Kikwete hawajafanya hivyo, kwa nini? Baada ya miezi sita na sasa mwaka bado wana kigugumizi, kwanini? Kwa sababu kadri watakavyokuwa wanaweka matokeo ktk website yao ndivyo wanavyoongeza idadi ya ushahidi. Mimi sijui majimbo yote ila kura alizopata Dr Slaa ktk Jimbo la Ubungo sizo zilizotangazwa na Tume. Kama wanaiba za Ubungo ambayo tulikuwa tumetimia, itakuwaje huko ambako hatukuwa na viongozi imara kwa wakati huo? sasa tuko nchi nzima nasubiri kwa hamu 2015.
  Sasa ndugu yangu, ukweli ni ukweli bila kujali umesemwa na mwanachadema au mwanaccm, mimi nimesema ninachojua, kuamini au kutoamini ni wewe. La msingi angalia mantiki.
   
 20. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #20
  Nov 28, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo waberoya,
  Unaipa nguvu hoja yangu kwa ccm ni wezi wa kura. Kwa sababu una maanisha kuwa kila mahali ambapo chadema hawajaweka wakala chadema hawapati kura kwa sababu mawakala wa ccm na wasimamizi wa serikali ya ccm kila kituo waliiba kura ya chadema. My goodness. Kwa hiyo, na kila kituo ambapo wakala alipata udhuru au aliugua kura zote zimekombwa na ccm. Kama ndivyo, tuna serikali au tuna wezi?
   
Loading...