Rais Kikwete aunda tume mgogoro UDOM

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
Saturday, January 15, 2011

Rais Kikwete aunda tume mgogoro UDOM

SAKATA la uongozi na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) limeingia katika hatua nyingine baada ya Rais Jakaya Kikwete kumwagiza Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo kuunda Tume tatu zitakazoshughulikia madai ya msingi ya wahadhiri hao.

Agizo hilo lilitolewa katika taarifa ya maandishi iliyopatikana jana baada ya wahadhiri hao kusisitiza kutoingia madarasani hadi kero zao zitakaposhughulikiwa ikiwemo ya kutolipwa mishahara mipya iliyoanza kutolewa Novemba, 2010.
Kauli ya Rais imekuja siku chache baada ya wahadhiri wa UDOM kutaka kumwona Rais na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ili kuwaeleza madai hayo na kero nyingine zinazohusu ustawi wa chuo hicho.
Miongoni mwa tume zitakazoundwa ya kwanza itakuwa chini ya Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ambayo itakua na kazi ya kukagua mishahara ya wahadhiri hao kazi iliyotarajiwa kuanza mapema kwa kukagua orodha ya mishahara ya ‘Pay roll’ za wafanyakazi wa chuo hicho.
Tume ya pili iliyoundwa ni ile ya Makatibu Wakuu ambayo itadadisi masuala mbalimbali yanayohusu UDOM ili kujua matatizo yaliyopo na chanzo chake.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo tume ya nyingine inamhusisha Kamishna wa Vyuo Vikuu vya Tanzania ambayo itaangalia masuala mbalimbali na masomo ya taaluma.
Wakati hayo yakiendelea, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, leo anatarajia kukutana na serikali ya wanafunzi pamoja na kuzungumza na wahadhiri wa chuo hicho kikubwa Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Umoja wa Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udomasa), Paul Loisulie Pinda, anakuja kushughulikia matatizo mbalimbali yanayojitokeza na yanayoendelea chuoni hapo.
Adiha, mwenyekiti huyo alisema wanaendelea na mkutano endelevu ambao pamoja na mambo mengine wanajadili namna ya kuufikisha mahakamani uongozi wa chuo chao.
 
Hivi tutaenda mpaka wapi kwa mwendo huu wa kuburuzwa na uongozi dhaifu namna hii. Kila kitu tume, tume, tume... Hili lilikuwa suala la kukaa ofisini na washauri wachache, kuwasikiliza wahadhiri na kutoa suluhisho. Matokeo ya kuwa na vilaza kwenye uongozi, wasio na uwezo wa kukabiliana na hoja za wasomi; wanajificha nyuma ya tume. Na wengine wanafurahia tume maana ni ulaji wao ndani ya matatizo ya watu na umaskini wa nchi.
Ni kiasi cha kupitia mafaili yanayoweka kumbukumbu za operations zinazodaiwa haziendi sawa, kama walivyofanya wahadhiri wenyewe.
Kama suala wazi kabisa kama hili linaundiwa tume, je bunge likianza na mijadala yake mizito, kila mjadala utaundiwa tume?
 
I wonder hizi pesa zakulipa tume huwa zinatoka wapi??? Kweli kabisa huu ni uvivu wakufikiri.
 
itaundwa na tume ya kutoa majibu, baada ya tume ya kuchunguza kumaliza kazi yake
 
Tume zinazoundwa na ofisi ya rais hazina lolote suala la msingi ni kuwawajibisha wahusika wote hayo mamilioni ya kuunda tume yangetumika kupunguza kero za wahadhiri.
 
Hiyo tume ilichangia kuleta tija gani katika mogogoro isioisha kati ya wanafunzi na waalimu dhidi ya uongozi wa UDOM, au juhudi zote zilikua ni zimamoto tu kama siku zote??????????????/
 
Hiyo tume ilichangia kuleta tija gani katika mogogoro isioisha kati ya wanafunzi na waalimu dhidi ya uongozi wa UDOM, au juhudi zote zilikua ni zimamoto tu kama siku zote??????????????/

Chuo chenyewe kimeanza zimamoto na kinaendeshwa zimamoto, matatizo yanaundiwa tume zimamoto yanatafutiwa utatuzi zimamoto.
Graduate wake wanaandaliwa zimamoto. Hatuwezi kutegemea lolote jipya zaidi ya zimamoto.
Sasa inabidi tukiite
Chuo Kikuu cha Zimamoto
 
Back
Top Bottom