Rais Kikwete asaini Muswada wa Katiba

Tusipoteze muda kujadili mapungufu ya sheria hii( sio muswada tena tangu jana Rais alipousaini). Tuwaandae watu wetu kutoa maoni juu ya KATIBA mpya. Najua tutapoteza muda pia kuwajadili watakaoteuliwa na Rais kuunda TUME kwa mujibu wa sheria hii. Tumpe Rais majina tunayoyataka yawemo kwenye tume hii sasa. Mimi naanza:
1. Salim Ahmed Salim- Mwenyekiti
2. Joseph Sinde Waryoba- Makamu
3. Profesa Issa Shivji- Mjumbe
4. Jenerali Ulimwengu- Mjumbe
5. Mohamed Said- Mjumbe
6.Mzee Mwanakijiji( Silifahamu jina lake)- Mjumbe
7.Askofu Elinaza Sendoro- Mjumbe
8.Hellen Kijo Bisimba- Mjumbe
9.Hawa Sinare- Mjumbe
10.Francis Stolla- Mjumbe
Wazanzibar watateuana wenyewe. Mpeni Rais majina. Wanasema ni MSIKIVU.
 
Wasi wasi wangu ni kuwa kama ni kweli basi Tanzania itachukua muda kupata uhuru kamili kulikoni huu ambao tunaigiza huku nchi ikishikiliwa na watu wachache wanaonufaika na raslimali zetu kwa mbinu zote.

Wakoloni weusi ni hatari sana.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Tatizo ni kwamba Mahanithi wa Kiislamu kila wakitoka swala za Ijumaa misikitini wana tabia ya kuvamia mitandaoni na maspikaa mitaani kutoka misikitini weekend nzima 24/7 wakijaribu kwa nguvu zao zote kupotosha jamii na harufu na kauli chafu vinavyotoka vinywani mwao...
Ndjabu Da Dude, kuwa kichaa si lazima uokote makopo!, ila kwa mwendo huu ndugu yangu, ni hakika, makopo pia utayaokota!.

Faiza Fox na ndungu zetu, Waislamu, msemeheni huyu kwa maana hajui atendalo, wala hata hahitaji 'fatwa', Mwenyeezi Mungu Mwenyewe (Alaah-SW), anayo namna yake ya kuwashughulikia watu wa namna hii!.

Poleni na asanteni kwa uvumilivu!
 
mgonjwa ameshakufa sasa utakaribishaje madaktari waendelee kuboresha afya yake zaidi?
 
Duh kwahiyo CDM walienda Ikulu kunywa chai na kushangaa fanicha za magogoni.
Hapana. Ujumbe ulimfikia vizuri JK kuliko kama wangeyasemea BUNGENI, laivu bila chenga za wabunge wa CCM. Hasa suala la ushiriki wa Zanzibar kwenye mchakato huu. Muungano wetu ni kama vile Zanzibar walishauvunja. Muungano uliopo ni wa Zanzibar na JMT kulingana na sheria hii.
 
With all crisis and frustrations from the failure to deal correctly with Magamba ... How do you expect the compensation work upon? Deal rightly with Mswaada and Katiba? ...

With the same driving forces which failed Magamba ... We should expect the same driving forces to fail us on Katiba ... Unless the forces are corrected and work perfectly with Magamba!! Then the corrected forces can deal correctly with Katiba ...something which I hope CCM will make sure it happens soon!!
 
kikwete imbecile, CCM imbecile, Mbowe imbecile, CDM imbecile, watanzania wote mapunguani.
:embarassed2:
 
With all crisis and frustrations from the failure to deal correctly with Magamba ... How do you expect the compensation work upon? Deal rightly with Mswaada and Katiba? ...

With the same driving forces which failed Magamba ... We should expect the same driving forces to fail us on Katiba ... Unless the forces are corrected and work perfectly with Magamba!! Then the corrected forces can deal correctly with Katiba ...something which I hope CCM will make sure it happens soon!!


Umesema ya kweli!
 
habari hiyo yawezakuwa yakweli kwasababu JK (Jua Kali) ni event driven yaana anaongozwa na si kuongoza.
 
Chadema walikaribishwa kunywa chai ikulu,kupiga story na mkuu au kuangalia African magic huku wakipiga soga za ulaya na jamaa yetu huyu Vasco dagama!? Kweli hii ni dharau kwa watanzania wote wapenda maendeleo!
 
Masaa kadhaa tu baada ya viongozi wa CDM kukaa na kushauriana na Rais kuhusu mswada wa katiba ukaeje,tayari jana rais amesha sain na kuufanya uitwe sheria! Hatujaskia lolote juu ya kilicho zungumziwa! Je,muafaka ulifikiwa au vipi? Alikubali mapendekezo? Na vipi,taarifa ya kuwa angesain jana bila ya marekebisho yoyote mliijua mkaamua kupiga mziki baridi au vipi?
 
Ni wazi kuwa ahadi ya kurekebisha Muswada wa Sheria ya Tume ya Katiba haitekelezeki.Ahadi hiyo ambayo ni kati ya mambo ambayo yamekubaliwa na pande mbili zilizokutana kwa siku mbili Ikulu(ambazo ni Ikulu na CHADEMA) haitekelezeki kwakuwa Sheria hairuhusu hilo.Masharti ya jumla ya Utungaji wa Sheria yanaainishwa chini ya Sehemu ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge,Toleo la mwaka 2007(kuanzia Kanuni ya 80 hadi kanuni ya 93).Hakuna Kanuni yoyote ambayo inaruhusu Bunge au Rais kuufanyia marekebisho Muswada ambao tayari umeshasomwa hadi mara ya tatu Bungeni na kupitishwa.Hakuna.Hivyobasi,Ikulu,kupitia Kurugenzi ya mawasiliano, imewadanganya watanzania na CHADEMA kwa kusema kuwa eti Muswada utafanyiwa marekebisho ili kuleta muafaka wa kitaifa.Je,Ikulu imetenda haki juu ya jambo hili?
 
Heading yako ni tofauti na ulichoandika,labda kama unamaanisha CHADEMA ni watanzania wote.
 
time interval between mazungumzo na kusign ni ndogo sana.anyway mchakato unatakiwa kuanza na sio kusubiri mezani.kama wamekubaliana juu ya hadidu rejea kurekebishwa na pia namna ya uteuzi wa tume kuwa na uwakilishi wenye uwiano nadhani sio chenga ni hatua.ila hiyo MoU ikikiukwa ndo tatizo
 
Napenda kuchukua nafasi hii kwa niaba ya watz wengi wapenda mabadiliko chanya, maendeleo na wazalendo wa kweli.

Kwanza niwapongeze sana viongozi na wabunge wa CHADEMA kwa kuibua na kulaani mambo mengi maovu ambayo yamekuwa yakifanywa na viongozi wa serikali ya CCM. Vile vile mmekuwa mstari wa mbele ktk kutetea haki za wananchi wanyonge na maskini wa nchi hii. Sidhani kama nina haja ya kuandika hapa harakati na jitahada zenu dhidi ya mapambano ya ufisadi na ukombozi wa taifa letu ambolo mpaka sasa liko mikoni mwa watu wachache wanaotuibia na walio juu ya sheria. Wafuatiliaji wote wa mustakabali wa hali ya siasa ya taifa wanajua na kiasi gani mnapambana.

Mmekuwa mwiba na sifingo kali sana kwa chama tawala kwa muda sasa. Lakini siku zote CCM imekuwa ikitumia mbinu mbalimbali za kuwaneutralize kama ilivofanikiwa kwa CUF hata hivo hamkonekana kutetereka hata kidogo. Watanzania wengi waliokosa matumaini na kukata tamaa, wanyonge, maskini, ambao wameporwa haki zao; wanaona nyie ndo tumanini jipya, nguvu mpya, wanaamini kupitia CDM iko siku haki zao zitarudi na misingi bora ya usawa ktk elimu, kazi, biashara na uongozi itarejeshwa ndani ya nchi yetu. Hiyo ilijidhihirisha baada ya matokeo ya uchaguzi uliopita, pamoja na hila zote za tume ya uchaguzi, polisi na usalama wa taifa lkn bado mliweza kuwaburuza CCM wakasahau kile walichozoea kuita ushindi wa kishindo!

Wakati wa kampeni zenu kuelekea uchaguzi mkuu 2010 moja ya ilani yeni ilikuwa ni kuanza mchakato wa kuandaa katiba mpya ndani ya siku 100 kama mngepata ridhaa ya wananchi ya kuongoza nchi. Kwa hila na njama kali sana kura hazikutosha, CCM kupitia rais wakawapora agenda yenu ya katiba. Kilichotokea toka siku JK anatangaza nia ya kuandika katiba mpya mpaka juzi mlivosusia mjadala wa muswada wa sheria ya kuandika katiba na kuomba kuonana na rais, kila mtu anajua. Macho na masikio ya wengi yalikuwa yakisubiri nini kitajiri baada ya CDM kukutana na JK. Tuliyoana na kusikia ni kinyume kabisa na matarajio ya wengi. Kwa ufupi tu kumekuwa na maoni na mitazamo tofauti kwa kile kilichodaiwa ni muafaka uliyofikiwa baina ya CCM na CDM. Mbaya zaidi tunaambiwa rais tayari ameshasaini huo muswada kuwa sheria. Watu wanataka kujua kiundani;

1. Muafaka gani huo uliofikiwa baina ya CCM na CDM? Ni mapendekezo gani mliyopeleka, yapi yamekubaliwa na yapi yamekataliwa? Msimamo wa CDM ni nn iwapo mapendekezo yenu yaliyokubaliwa hayatatekelezwa?
2. Rais sasa ameshaini; nafasi ya wananchi iko wapi katika maboresho ya hiyo sheria kabla machakato wa kuandika katiba haujaanza?

Tunahitaji majibu ya haya maswali, itisheni press conference mtueleze haya; vinginevyo hisia zilizotawala vichwani mwa watu sasa ni kwamba CCM ameshatoa posa kwa mke pili ndoa itafungwa karibuni. Binafsi sitaki kufikiria hivo bado nina imani na CDM, lakini bila majibu ya maswali haya mtatuacha njia panda tukijiuliza kama huu ndio mwisho wa CDM kama CUF.

Nawasilisha!!!
 
Du!. Nilijua alishausani ile Jumapili asubuhi kabla ya kukutana na Chedema!.

Kitendo cha kuusaini leo, ni uthibitisho kuwa JK ni rais msikivu na tena amewageshimu sana Chadema hadi kuwasikiliza kwanza kama wana hoja za msingi ndipo akausaini!.

Maadam umeshasainiwa, kazi sasa ni moja tuu, tuipe tume ushirikiano stahiki tupate katiba bora na sio bora katiba!.

Lazima ufanyiwe marekebisho, la sivyo wananchi hatukubali. Hakuna katiba bora itakayotokana na hiyo sheria.
 
Back
Top Bottom