Rais Kikwete asaini Muswada wa Katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete asaini Muswada wa Katiba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Halisi, Nov 29, 2011.

 1. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Novemba 29, 2011, ametia saini Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011.

  Hatua hiyo ya Mheshimiwa Rais kutia saini Muswada huo inakamilisha safari ya kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 baada ya Bunge kuwa limepitisha Muswada huo uliowasilishwa na Serikali katika kikao kilichopita cha Bunge.

  Aidha, kutiwa saini kwa Muswada huo ili uwe Sheria ni hatua kubwa na muhimu katika safari ya kutungwa kwa Katiba mpya ya Tanzania kama ilivyoahidiwa na Mheshimiwa Rais Kikwete katika salamu zake za Mwaka Mpya kwa wananchi Desemba 31, mwaka jana, 2010.

  Pamoja na kutiwa saini hiyo bado Serikali itaendelea kusikiliza maoni na mawazo ya wadau na wananchi mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha sheria hiyo.

  Hivyo, Mheshimiwa Rais Kikwete anatoa wito kwa mwananchi yoyote mwenye maoni ama mawazo ya namna ya kuboresha Sheria hiyo, ajisikie yuko huru kutoa maoni yake na Serikali itasilikiza na kuchukua hatua zipasazo.

  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu,
  DAR ES SALAAM.

  29 Novemba, 2011
   
 2. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #2
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Kaazi kwelikweli
   
 3. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #3
  Nov 29, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Yawezekana hayo ndiyo yalikuwa sehemu ya makubaliano kwamba kwanza mswada usainiwe kuwa sheria?

  Tanzania tumezoea vilaka kwenye kwenye sheria mpya hivyo sitachangaa mara tu Bunge lijalo kukutana, jambo la kwanza likawa kufanyia marekebisho sheria hiyo mpya.
   
 4. Z

  Zion Train JF-Expert Member

  #4
  Nov 29, 2011
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 503
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kwa mbwembwe mkuu Halisi??
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Nov 29, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,533
  Trophy Points: 280
  Du!. Nilijua alishausani ile Jumapili asubuhi kabla ya kukutana na Chedema!.

  Kitendo cha kuusaini leo, ni uthibitisho kuwa JK ni rais msikivu na tena amewageshimu sana Chadema hadi kuwasikiliza kwanza kama wana hoja za msingi ndipo akausaini!.

  Maadam umeshasainiwa, kazi sasa ni moja tuu, tuipe tume ushirikiano stahiki tupate katiba bora na sio bora katiba!.
   
 6. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #6
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Anadhani ameikomoa CDM lakini kumbe in future amehatarisha umaarufu wa chama chake!
  Najua watu watashabikia sana rais kutia saini muswada huo kama vile ulikuwa hauna mapungufu!
   
 7. M

  Mwanyava JF-Expert Member

  #7
  Nov 29, 2011
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama hilo ni kweli, Ina maana gani kuwakaribisha CDM Ikulu ilihali anajua hatapokea mapendekezo yao??? Sijakuelewa
   
 8. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #8
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Bure kabisa, hamna kitu hapo!! Katiba mpya bila wananchi wenyewe kushika ushukani HAIWEZEKANI!!
   
 9. M

  Mr. Clean Senior Member

  #9
  Nov 29, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 195
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Halisi, are you serious? hii kitu ni kweli?

  so alikuwa awasubiri mwende kumpa dondoo zenu ikulu juzi ili aongeza mzigo wa makaratasi yakutupwa dampo?

  for sure hashauriki! .. LOWASA UKO WAPI...?
   
 10. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #10
  Nov 29, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Siasa zetu ni usaanii mtupu!
   
 11. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #11
  Nov 29, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Si kweli
   
 12. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #12
  Nov 29, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Sasa makubaliano na CHADEMA yalikuwa ya nini?
   
 13. F

  FredKavishe Verified User

  #13
  Nov 29, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,090
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Jk ana vichekesho kuliko hata mr bean'
   
 14. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #14
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,936
  Trophy Points: 280
  Kweli JK ni Master! Duh!

  Ni top Don!

  Nimegundua humu mtandaoni tunapoteza tu muda!

  Wanasiasa ni wanafiki sana, sitaki kuwa mwanasiasa kwasababu mimi na unafiki ni mbalimbali.
   
 15. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #15
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Lakini itamcost,
   
 16. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #16
  Nov 29, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Very simple ccm wanataka waonekane wao ndio walioibadilisha katiba na huku cdm walitaka kuipiku na ionekane yenyewe ndio imemake move yaani ni suala la kuteka hoja nzima na ionekane ya watu fulani na ndio dhamira ya vyama vyote tawala na upinzani, ili kuweza kuwa na hoja 2015.

  Haya tumesikia na ninaamini wengine wamesikia kilichobaki tupeleke yale tuyatakayo kwa Rais ili yafanyiwe kazi ikiwezekana tuweke ushahidi tusije kurukana jua likizama.
   
 17. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #17
  Nov 29, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Sasa chadema walifuata nin ikulu?
   
 18. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #18
  Nov 29, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,315
  Trophy Points: 280
  Social climber.... slowly.... on his way up... to the top, like a camelion, climbing a tree..
   
 19. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #19
  Nov 29, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,076
  Likes Received: 1,812
  Trophy Points: 280
  safi sana... JK siku zote kiongozi mzuri anafanya maamuzi sahihi na sio kupelekwapelekwa na kikundi cha watu flani nazungumzia (CDM HAPA)
   
 20. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #20
  Nov 29, 2011
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ....# hakunaga Rais mwingine kama wewe, hakunaga!
  ....# hakunaga daktari mwingine kama wewe, hakunaga!


  ....# oya oyaa, kaa ukijua starehe ni gharama!!

  .....# unibebe, unibebe, unibembeleze.....
   
Loading...