Rais Kikwete asaini Muswada wa Katiba

Raisi anakaribisha maoni ya kuboresha sheria aliyoisaini,sheria aliyosaini inasema kujadili suala lolote linalohusiana na sheria hiyo ni kosa na adhabu yake ni kifungo miaka mitano.
Hayo ndiyo mambo ya hapa kwetu tz
 
CCM na rais wake ni sikio la kufa ......... lazima tuanze mikakati ya kuwaondoa kabla ya 2015 vinginevyo nchi hii imetumbukia na wanatumaliza.
 
Wee uliona wapi unampa Kaburu atunge katiba ya SA...Kitu kimoja msichofahamu ni kwamba kwetu sisi katiba iliyopo ni sawa kabisa na ya makaburu na kweli vigumu sana kwa mzungu kuelewa makosa yalokuwepo na hakika hata ukimwambia makosa hayo sidhani kama ataelewa. Wee endelea kushadadia maamuzi haya lakini kumbuka umeshika Kisu penye makali na inayokuumiza kila siku ni katiba ya CCM hii hayo mabadiliko yako hayakubaliki kama ulivyoshindwa kupata mahakama ya kadhi na kutambuliwa kwa mashujaa wenu wakati una wabunge wengi wa CCM.

Kama bunge ni makaburu basi ni wananchi walio wengi ndio waliwachaguwa. Hapo hauna hoja. Unatafuta "sympathy".
 
Hii nchi kweli tuna kazi.......after all the cries na nini from all parts of the country kuhusu mapungufu ya mswada....bado jama kasaini kwa kufuata tu matakwa ya chama chake ccm....

My take:
  • Sitegemei kama kutakuwa na mabadiliko ya msingi pale ambapo wataurudusha mswada bungeni.....kwani mtazamo wa rais na ccm wote ni kwamba ili kuleta mabadiliko ya msingi yanayopigiwa kelele lazima mapendekezo yote yapigiwe kura bungeni ili yapitishwe na tusisahau kuwa bungeni majority ni ccm...hivyo yale waliyokataa tangu mwanzo hawatayapitisha kwa wingi wa kura zao bungeni.......hapa ndipo jk alipoweka nguvu yake........
  • Jk kasaini mswada kwa shinikizo la wabunge wake na hivyo asingeweza kuacha kusaini kwani angeonekana kuwasaliti wabunge wake ambao kwa hali ilivyo wameonekana kuchangia kwa kiasi kikubwa madudu na uozo wa serikali hii......na pia wameamua kufanya maamuzi yoyote hata kama yatadhuru taifa ili kuwakomoa chadema.Tusisahau kuwa uozo mwingi nchini umekuwa unashabikiwa na wabunge wa ccm bungeni mpaka pale ukweli unapodhihirika ndipo nao huamka na kujifanya wameguswa.........hata kitendo cha kupandishiwa posho kichinichini ni ili wapitishe huu mswada feki.......sasa jk kwa kuwa shortsighted.......hawezi kuwapinga wabung wake pamoja na kwamba kwa mamlaka yake angeweza kabisa bila shida kutosaini mswada na kuurudisha bungeni ukajadiliwe upya......
  • Kwa wale wanaowalaumu chadema sioni mantiki kwani nadhani chadema wamefanya wajibu wao kama chama cha upinzani..........wametoka bungeni kupinga uozo.....kwani hata wangebaki na kujadili bado wangeshindwa kwa wingi wa kura, na pia wamejitahidi kuongea na rais......na wametoa mapendekezo yao...ambayo yanawakilisha asasi nyingine nchini.......kwa kweli wamefanya wajibu wao kichama.........................wao ccm kwa kupitia rais wameamua kupitisha mswada feki kwa maslahi yao ya baadae kama chama........na wanajua mabadiliko yatakuwa yale yenye kuwanufaisha wao na si vinginevyo..........kwani wana wingi wa kura bungeni.....tusitegemee mabadiliko ya msingi.......cha kuumiza zaidi hamna mahali pengine zaidi ya bungeni pa kufanyia mabadiliko ya sheria kwani tayari hili JK analifahamu......ndio sababu amesaini fasta..........sheria hubadilishiwa bungeni ambapo wao ccm ni wengi.....tutegemee nini???????????????????????????????????????
 
Well, a first Offence can build a clear defence strategy..
I'm sure the're hit 'cause I know where their guards are! and I can feel their pain..

Poor way of thinking, are you here to hurt others? you are too low as I said, politics are meant never to hurt anyone, politics is the process of wanting everyone to come out unscathed, winner and no losers. War is where no one wins.
 
Hao wote ni domo tu hawana uwezo wa kufanya lelote. Hata viongozi wao wameona ni upumbavu kuleta fujo kwenye siasa. Hawa wabinafsi ndio wenye mawazo ya kipuuzi. Kwakuwa hawakupata walicho kuwa wakikitaka basi wanataka kufanya fujo.
 
Tuunde TUME jamani. Ndio hatua inayofuata. JK ni msikivu tukimpelekea majina tunayoamini yatatusaidia kwenye mchakato huu atayapokea na kuyafikiria. Tusipoteze muda. Hii tayari ni sheria ya NCHI. Tusingoje ayataje majina kisha tuendelee kumlaumu!
 
Wanabodi,
Lazima tufike mahali tuwe tunakubali matokeo!. Mbona statement ni nzuri tuu. Milango iko wazi kwa marekebisho yoyote. Serikali yetu sasa ni serikali sikivu!.

Hii ni ndoto ya mchana kweupee! Muswada umesainiwa anaendelea na kinachofuata kulingana na sheria inavyosema. Kifupi hiyo sheria inampa mamlaka ya kukubali au kukataa mapendekezo yoyote hata yatakayowasilishwa na tume ambayo yanatoka kwa wananchi.

Na amejiweka mahali pazuri sana kwa sasa, sheria imempa mamlaka yote. Kifupi ni kwamba hawezi kukubali maoni ambayo anajua kabisa yatamkaanga yeye na chama chake. Hayo ni maumivu makubwa sana kwa watanzania na wapenda haki na tusijipe moyo kuwa atapokea maoni na kuyafanyia kazi.

Watanzania mmepiga kelele kuhusu ufisadi mara ngapi na amefanya nini mpaka leo muamini kuwa amebadilika. Mbona mnakuwa kama watoto wa jana?

Maslahi ya wananchi ni kinyume kabisa na maslahi yake na ya chama chake kwa sasa. Wananchi wangependa raisi apunguziiwe madaraka, aweze kushtakiwa kwa makosa aliyofanya, na mafisadi ambao ni jamaa zake washughulikiwe, hii ni ili kujenga taifa lenye maadili. Sasa hayo yote si maslahi kwa CCM, ni kuiangamiza.

Nnachokiona kitawork kuirescue hii nchi ni kustep up to the level of Arabs na kudai mabadiliko katika nchi hii, ni ghali ila hakuna njia ya mkato, unfortunately.
 
CHADEMA HOI tehe, tehe wameshindwa kupigania muswaada wa katiba mpya kama walivyokuwa wana pretend ni heri mara 100 Mh Kafulila kuliko Mbowe, Chadema ni wanafiki nawapo kimasilahi zaidi naichukia CCM, Chadema and CUF kwasababu wote ni wanafiki. Mh Kafulila pigania ule mchakato wa paralle process ya kutengeneza katiba nasi wananchi wote tutakuwa nyuma yako.
 
SOBY,

Kuna tatizo kubwa sana la watanzania wengi sana kugawanyika kivyama at the same time kimtazamo wa kidini.

Yani haya yananishangaza sana,utakuta waislam wengi either ni CCM ama CUF,na baadhi vyama vingine.

Ni mgawanyiko ambao umelazimishiwa na ni kama umekubalika na watanzania,maana sina la kusema,matokeo ya kura ndiyo yana onyesha wazi kabisa,na pia chuki za wazi humu kwa wale ambao wanajitambulisha kama ma anti CDM...Yani ni halali kutukana "Makafiri" wa CDM,utadhani CCM ni chama halali cha kiislam!

Nilitembelea Bongo like 3 yrs ago,i mean hapo Dar. Na nina rafiki yangu msomali nikawa namwambia mambo ya JF na CDM,haah,kutaja CDM nilijuta kwanini hata niliitaja,kutaja viongozi wa CDM tu,ni chuki mbaya sana na sikujua ni kwa nini...Maybe mapropagandist wa humu ndo wamehamaiza kazi mtaani na sasa humu?

Kuna watu wameaminishwa kabisa haya mambo na nyie ambao mko humu mmesoma na muna uelewa mkubwa zaidi,chuki za kidini zina manufaa gani kama hamataki civil war?

Na hayo yakitokea, ninyi ndo mtalaumiwa kwasababu mnachangia sana huu umaluuni.

Kama ulizungumza na Msomali sijui mawazo ya wasomali juu ya vyama vya siasa Tanzania.

Ushauri wangu kwako: Safari nyingine ukija Tanzania, Jaribu kuzungumza na Watanzania kwani vyama vya siasa vya Tanzania haviwakilishi mawazao au interest za watu nje ya Tanzania, yaani havivuki mipaka ya Tanzania.
 
Hapa ni kusubiri tu huruma ya Jakaya,sioni cha ziada..nilikuwa nafikiri hisia zangu zinanituma vibaya,kumbe ni kweri hii nchi haiwezi kuletewa mabadiliko na wanasiasa.tuendelee kungoja.
 
Hii ni ndoto ya mchana kweupee! Muswada umesainiwa anaendelea na kinachofuata kulingana na sheria inavyosema. Kifupi hiyo sheria inampa mamlaka ya kukubali au kukataa mapendekezo yoyote hata yatakayowasilishwa na tume ambayo yanatoka kwa wananchi.

Na amejiweka mahali pazuri sana kwa sasa, sheria imempa mamlaka yote. Kifupi ni kwamba hawezi kukubali maoni ambayo anajua kabisa yatamkaanga yeye na chama chake. Hayo ni maumivu makubwa sana kwa watanzania na wapenda haki na tusijipe moyo kuwa atapokea maoni na kuyafanyia kazi.

Watanzania mmepiga kelele kuhusu ufisadi mara ngapi na amefanya nini mpaka leo muamini kuwa amebadilika. Mbona mnakuwa kama watoto wa jana?

Maslahi ya wananchi ni kinyume kabisa na maslahi yake na ya chama chake kwa sasa. Wananchi wangependa raisi apunguziiwe madaraka, aweze kushtakiwa kwa makosa aliyofanya, na mafisadi ambao ni jamaa zake washughulikiwe, hii ni ili kujenga taifa lenye maadili. Sasa hayo yote si maslahi kwa CCM, ni kuiangamiza.

Nnachokiona kitawork kuirescue hii nchi ni kustep up to the level of Arabs na kudai mabadiliko katika nchi hii, ni ghali ila hakuna njia ya mkato, unfortunately.

Jamani tufunge ukurasa kuhusu MUSWADA, kwani tuliowatuma kukutana na Raisi wameshafanya kazi yao. Wamekwenda IKULU na kupokelewa vizuri tu kama waheshimiwa na kupata fursa ya kujadiliana na Rais kwa kina. Ndio wakafikia makubaliano yaliyomuwezesha Rais kusaini MUSWADA huo.

Kama wasingekubaliana, nahakika kabisa kuwa CHADEMA wangeitisha MAANDAMANO. Hata lugha zao kwenye vyombo vya habari wenyewe mmezisikia, ni nyoofu, laini na za kuridhika na makubaliano. Isitoshe kati ya waliotumwa huko ni wale wabunge NGANGARI kama Tundu Lisu ambaye asingempa hata sekunde mh Rais kama wasingekubaliana.

Kazi yetu kubwa sasa hivi ni kushughulika na Utungwaji wa katiba, na tuachane na mambo ya mswaada. Tushirikiane tutafika tu, Tanzania si mtu mmoja au chama kimoja, ni ya wote hata vyama pinzani. Tuijenge nchi yetu.
 
Ndicho ninachowasisitiza watu humu. Tuunde "TUME KIVULI" yetu. Ataiona tu. Ana macho na masikio NCHI nzima. Halafu huu sio muswada tena. Ni sheria ya NCHI tangu jana.
 
Poor way of thinking, are you here to hurt others? you are too low as I said, politics are meant never to hurt anyone, politics is the process of wanting everyone to come out unscathed, winner and no losers. War is where no one wins.
You have your way of twisting words. One thing I know for sure, when it comes to CCM your brain's perceptual systems operates on a slight delay signals..which results in different percepts on issues of the same nature to Islam. I meaned not to hurt anyone physically but feed your brains with touching, sensitive mult stimulus that you can actually see the percept shift from yourside to ours, trying to fit you in our shoe which hurts..One thing for sure is that your reactions to events depends on subject’s culture of THEM vs US..
 
Hao wote ni domo tu hawana uwezo wa kufanya lelote. Hata viongozi wao wameona ni upumbavu kuleta fujo kwenye siasa. Hawa wabinafsi ndio wenye mawazo ya kipuuzi. Kwakuwa hawakupata walicho kuwa wakikitaka basi wanataka kufanya fujo.
Mkuu nataka kukuuliza tu kitu kimoja maana hapa tunazungumzia haki za wananchi na uwezo wa rais ama niseme mamlaka. Nitakuuliza swali..
1. Kama Mkapa angetaka kujiongezea muda wa kutawala yaani kuweka awamu tatu kwa rais. Je, Nitaratibu gani zingefuatwa? Na zipi ungezikubali na kwa nini...Nakuomba unijibu hili kwanza kisha tuendelee taratibu bila misuguano..
 
Hapana. Ujumbe ulimfikia vizuri JK kuliko kama wangeyasemea BUNGENI, laivu bila chenga za wabunge wa CCM. Hasa suala la ushiriki wa Zanzibar kwenye mchakato huu. Muungano wetu ni kama vile Zanzibar walishauvunja. Muungano uliopo ni wa Zanzibar na JMT kulingana na sheria hii.
Mkuu najuwa wewe ni CCM bila "chenga"

Statement yako ingekuwa kweli ONLY kama bunge halitahusika tena kwenye mchakato huu...
 
Kama ulizungumza na Msomali sijui mawazo ya wasomali juu ya vyama vya siasa Tanzania.

Ushauri wangu kwako: Safari nyingine ukija Tanzania, Jaribu kuzungumza na Watanzania kwani vyama vya siasa vya Tanzania haviwakilishi mawazao au interest za watu nje ya Tanzania, yaani havivuki mipaka ya Tanzania.
Kwani Ismael Aden Rage si mtanzania?

Abdulrahman Kinana je?

Hivi Ngoda ni kitu gani mkuu?
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom