FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 92,883
- 109,213
Anadhani ameikomoa CDM lakini kumbe in future amehatarisha umaarufu wa chama chake!
Najua watu watashabikia sana rais kutia saini muswada huo kama vile ulikuwa hauna mapungufu!
Kama muswada una mapungufu itajionesha kwenye sheria. Na sheria hizi za kibinaadam hubadilika badilika kila mara na huwa "revised". Sioni hapa tatizo ni nini. Na kama bungeni majority ni wachama tawala unategemea utapata nini zaidi ya wanachokitaka wao? Inatakiwa hapa ndio wapinzani wawe wabunifu kwa kuweza kuwainisha wananchi wawachaguwe kwenye chaguzi zijazo na kuwa wabunifu pia kuwakinaisha wabunge "majority" wawe wanapigania maslahi ya nchi badala ya maslahi ya chama pekee.
Yote hayo yanawezekana ikiwa tu chama pinzani kitaanza kwa kukonga nyoyo za wananchi kwa siasa safi na uongozi bora na si kwa kuingia mitaani kuanza maandamano. Maandamano hayasaidii, jifunzeni kuwa wanasiasa na si wapiganaji.