Rais Kikwete aonya kuingiza dini katika siasa

Rais Kikwete aonya kuingiza dini katika siasa

Ni vizuri jk angetafakari umetuachaje kwanza maana vilio vya watanzania vitakulilia milele,
 
Ha ha ha haaa kichekesho hichi.. kuna mtu ameligawa hili taifa kwa udini kama yeye?
 
Huyu jamaa ni janga la Taifa, yeye ndiye kinara wa kusababisha udini nchini halafu leo anang'aka na kutaka kuwalaumu wengine. Alikuwa mmoja wa wale waliodai CHADEMA ni chama cha kidini na kikabila hakutafakari kwa kina athari ya maneno yake kwa Watanzania.

Well said!
 
BAK umesema vema kabisa,
Sitasahau nilivyoumia kwa propaganda chafu za kidini alizozifanya 2005 na 2010.
Nina hakika watanzania watafunguka zaidi pindi atapokuwa nje ya madaraka

DOUGLAS SALLU

Rais Kikwete, mbegu uliyoipanda italitafuna taifa letu...
Siyo siri kuwa muasisi wa siasa za maji taka hapa Tanzania ni JK na genge lake la wanamtandao. Mbinu hii aliizanza mapema kabla ya uchaguzi wa mwaka 2005, na wahanga wakubwa wa siasa hizi za kishenzi ni Fredrick Sumaye, Salim A. Salim, Prof.Mark Mwadosya na wengineo, na wahanga hawa walilengwa kwani walionekana kuwa tishio kwa malengo ya JK kuukwaa urais hivyo ilikuwa lazima wachafuliwe kiasi cha kutosha ili wanuke na wakati huo magazeti yakimpamba JK kwa sifa asizostahili, na kweli mbinu hii ya kishenzi ilifanikiwa na JK akawa rais.

Mwaka huu kwa vile kanuni za CCM zilikuwa zinamlinda JK asipate mpinzani toka ndani ya chama hicho hakuwa na haja ya kutumia mbinu hiyo na akawa anajiandaa kushinda kwa kishindo, lakini ghafla upepo ukabadilika baada ya mzalendo wa kweli Dr Slaa kuteuliwa na Chadema kugombea nafasi ya urais, JK baada ya kuona kuwa maji ni marefu kwake na chama chake akarudia tena mbinu yake ya maji taka na ndipo zikasikika habari za Dr Slaa kuchukuwa mke wa mtu, lakini kwa vile watanzania wa leo siyo wale wa mwaka 47, waliimpuuza JK na siasa zake hizo chafu wakaendelea kumuunga mkono Dr Slaa.

Baada ya JK na genge lake kuona kuwa mbini hii haifanyi kazi akaamua kutumia SILAHA YA MAANGAMIZI -
UDINI.

Ukazushwa uvumi kuwa Dr Slaa ametumwa na Kanisa Katoliki, mbinu hii ilikolezwa na magazeti ya fisadi Rostam Aziz na mengine kama Habari Leo, AL HUDA, AL NUR, na kama haitoshi zikatumwa sms kwa mamilion ya wapiga kura kumchafua Dr Slaa na kuhusisha na udini.

Siyo siri kuwa silaha hii imeacha majeraha mengi miongoni mwa Watanzania na mfano hai ni hata hapa jamvini hangover ya siasa hizi za udini zilizo asisiwa na Kikkwete mwenyew e ipo. Dini ni jambo nyeti sana na likitumiwa vibaya linaweza kuilipua nchi nzima na hiki ndicho alichokifanya JK.


https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...uliyoipanda-italitafuna-taifa-letu-print.html

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa kuna ushahidi sasa unaothibitisha kuwa baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini wamekuwa wanachaganya dini na siasa wakitumia dini kuunga mkono baadhi ya vyama vya siasa na shughuli za kisiasa nchini.

Aidha, Rais Kikwete amewaomba mabalozi hao “kuiokoa” Tanzania katika majanga makubwa yanayoweza kuipata kwa kutumia dini kuendeleza siasa, hatua ambayo ameielezea kama “njia ya hatari kweli kweli.”

Rais Kikwete alikuwa anazungumza usiku wa Jumatatu, Oktoba 6, 2014, wakati wa chakula cha usiku ambacho alikula na viongozi wa dini nchini ambao wanaendelea na mkutano wao wa mwaka kwenye Hoteli ya White Sands ya Dar es Salaam.

Mkutano huo wa siku nne ulioanza juzi unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence ni mwendelezo wa mikutano ya viongozi wa dini kubwa za Kikristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini. Mkutano wa mwisho ulifanyika mwaka juzi, 2012 kwenye Hoteli hiyo hiyo.

Aidha, Mkutano huo ambao moja ya wadhamini wake ni taasisi ya Programme for Christian-Muslim Relations in Africa (PROCMURA) yenye makao yake makuu mjini Nairobi, Kenya, unahudhuriwa na mabalozi 15 wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini na mashirika kadhaa ya kimataifa likiwemo lile la Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP).

Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika Mkutano huo ni wa Ujerumani, Iran, Marekani, Norway, Uturuki, Sweden, Canada, Denmark, Finland, Misri, Qatar, Uswisi, Palestina, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Saudi Arabia na Umoja wa Ulaya (EU). Viongozi wa dini wanaoshiriki katika Mkutano huo wanatoka Zanzibar, Dar es Salaam, Mwanza, Morogoro, Mtwara, Lindi, Arusha, Geita na Mbeya.

Akizungumza kwenye chakula hicho cha usiku, Rais Kikwete aliungana na Mshauri Mkuu wa PROCMURA ambaye alionya kuhusu hatari za kweli zinazoendelea kuikabili dunia kwa sababu ya kuingiza dini katika siasa (Politicisation of Religion) na kuingiza siasa katika dini (Religinasation of Politics).

Rais Kikwete amewaambia viongozi hao: “Mwakilishi wa PROCMURA ametoa ujumbe mzito sana. Ametoa fumbo ambako amewaasa mabalozi wasiingize dini katika siasa na wasiingize siasa katika dini. Na mimi nataka kuungana naye na kuwaomba mabalozi waiokoe nchi yetu katika majanga makubwa yanayoweza kutokana na kutumia dini kuendeleza siasa. Ni njia ya hatari kweli kweli.”

Ameongeza Rais Kikwete: “Kuna ushahidi sasa kuwa baadhi yetu, baada ya kushindwa kutumia ukabila katika kuendeleza siasa, sasa mmegeukia dini. Mnatumia dini katika kuunga mkono baadhi ya shughuli za kisiasa na baadhi ya vyama vya siasa.”

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.

7 Oktoba, 2014.

Mama Rwakatare ni kiongozi wa dini...ni nani alimteua kuwa mbungee? sasa ni nani aliyeanzisha mbegu ya kuchanganya dini na siasa?
Hivi kweli sisi wananchi mnatuonaje?
 
Ulikuwa ujumbe sahihi, watu wenye akili ndogo wakishindwa hoja ndipo huleta vitimbi vingine badala ya kujikita katika hoja.
 
Back
Top Bottom