Rais Kikwete aonya kuingiza dini katika siasa

Rais Kikwete aonya kuingiza dini katika siasa

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,356
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa kuna ushahidi sasa unaothibitisha kuwa baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini wamekuwa wanachaganya dini na siasa wakitumia dini kuunga mkono baadhi ya vyama vya siasa na shughuli za kisiasa nchini.

Aidha, Rais Kikwete amewaomba mabalozi hao “kuiokoa” Tanzania katika majanga makubwa yanayoweza kuipata kwa kutumia dini kuendeleza siasa, hatua ambayo ameielezea kama “njia ya hatari kweli kweli.”

Rais Kikwete alikuwa anazungumza usiku wa Jumatatu, Oktoba 6, 2014, wakati wa chakula cha usiku ambacho alikula na viongozi wa dini nchini ambao wanaendelea na mkutano wao wa mwaka kwenye Hoteli ya White Sands ya Dar es Salaam.

Mkutano huo wa siku nne ulioanza juzi unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence ni mwendelezo wa mikutano ya viongozi wa dini kubwa za Kikristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini. Mkutano wa mwisho ulifanyika mwaka juzi, 2012 kwenye Hoteli hiyo hiyo.

Aidha, Mkutano huo ambao moja ya wadhamini wake ni taasisi ya Programme for Christian-Muslim Relations in Africa (PROCMURA) yenye makao yake makuu mjini Nairobi, Kenya, unahudhuriwa na mabalozi 15 wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini na mashirika kadhaa ya kimataifa likiwemo lile la Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP).

Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika Mkutano huo ni wa Ujerumani, Iran, Marekani, Norway, Uturuki, Sweden, Canada, Denmark, Finland, Misri, Qatar, Uswisi, Palestina, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Saudi Arabia na Umoja wa Ulaya (EU). Viongozi wa dini wanaoshiriki katika Mkutano huo wanatoka Zanzibar, Dar es Salaam, Mwanza, Morogoro, Mtwara, Lindi, Arusha, Geita na Mbeya.

Akizungumza kwenye chakula hicho cha usiku, Rais Kikwete aliungana na Mshauri Mkuu wa PROCMURA ambaye alionya kuhusu hatari za kweli zinazoendelea kuikabili dunia kwa sababu ya kuingiza dini katika siasa (Politicisation of Religion) na kuingiza siasa katika dini (Religinasation of Politics).

Rais Kikwete amewaambia viongozi hao: “Mwakilishi wa PROCMURA ametoa ujumbe mzito sana. Ametoa fumbo ambako amewaasa mabalozi wasiingize dini katika siasa na wasiingize siasa katika dini. Na mimi nataka kuungana naye na kuwaomba mabalozi waiokoe nchi yetu katika majanga makubwa yanayoweza kutokana na kutumia dini kuendeleza siasa. Ni njia ya hatari kweli kweli.”

Ameongeza Rais Kikwete: “Kuna ushahidi sasa kuwa baadhi yetu, baada ya kushindwa kutumia ukabila katika kuendeleza siasa, sasa mmegeukia dini. Mnatumia dini katika kuunga mkono baadhi ya shughuli za kisiasa na baadhi ya vyama vya siasa.”

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.

7 Oktoba, 2014.
 
CCM walianza na propaganda za ukabila zikashindikana. Wakaja na mbinu za ukanda zikachuja. Wakaibuka na singo ya udini haikulipa. Wakaparamia mazingaombwe ya ugaidi yakawarudi! Wakaibuka na kitisho cha kuingia msituni, kikagota. Sasa wamekuja na katiba ya kitapeli huku wakiwatisha mabalozi na viongozi wa dini eti wajiepushe na siasa!
 
Hivi huyu Kikwete hazioni propaganda chafu zinazofanywa na chama chake dhidi ya vyama vya upinzani kwamba ni vya kidini? CUF walisema ni chama cha Waislamu, wakafanikiwa kukisambaratisha. Sasa wanatunisha misuli kuwa CDM ni chama cha Wakristo. Na huyo Kikwete ndiye mwenyekiti wa hicho chama cha propaganda hizi chafu. Hivi anamhadaa nani hapa?
 
Balozi nyingi zilikuwapo katika awamu zote nne za marais hapa nchini Tanzania, mbona hakuna awamu ambayo udini na siasa vimechanganywa Tanzania kama awamu ya nne?

-Mbona JK hakumkanya Lukuvi kuongea siasa ndani ya nyumba ya ibada ya dini nyingine dhidi ya dini nyingine?
 
Huyu Kikwete mnafiki tu, yeye ndiye kinara wa udini hapa Tanzania! Amalize muda wake aende zake.
 
Huyu jamaa ni janga la Taifa, yeye ndiye kinara wa kusababisha udini nchini halafu leo anang'aka na kutaka kuwalaumu wengine. Alikuwa mmoja wa wale waliodai CHADEMA ni chama cha kidini na kikabila hakutafakari kwa kina athari ya maneno yake kwa Watanzania.
 
Unaona eeh!!!! Jamaa huyu ni mtu wa ajabu sana ana unafiki wa hali ya juu. Lukuvi alipotoka ndani ya ukumbi wa Bunge hakumuonya kabisa akaamua kukaa kimya kabisa.

https://www.jamiiforums.com/katiba-...lliam-lukuvi-ameutia-dosari-utawala-wako.html

Balozi nyingi zilikuwapo katika awamu zote nne za marais hapa nchini Tanzania, mbona hakuna awamu ambayo udini na siasa vimechanganywa Tanzania kama awamu ya nne?

-Mbona JK hakumkanya Lukuvi kuongea siasa ndani ya nyumba ya ibada ya dini nyingine dhidi ya dini nyingine?
 
namuhurumia sana sana Rais Kikwete kama alikuwa analijua hilo kwa nini aliwapeleka viongozi wa dini kwenye bunge la katiba? au ni kwa sababu alijua watawaunga mkono ccm kwenye suala la katiba? kwa maana nyingine Kikwete ndie anayetumia dini kwenye mambo ya kisiasa,sisi kina gogo la shamba ndivyo tujuavyo na kama ningekuwa dodoma bango langu ningeandika. NI KOSA KUBWA SANA VIONGOZI WA DINI KUWA MAHALI HAPA
 
kwa ccm kuchanganya dini na siasa ni pale tu,viongozi wa dini wanapoikosoa serikali lakini wakiwapongeza serikali haoni kwamba huko ni kuchanganya dini na siasa, sasa sisi kina gogo la shamba tunamuuliza kwa nini anakubali viongozi wa dini kuwepo hapo kwenye makabidhiana ya katiba?
 
hacha kumkanya Lukuvi tu,sisi kina gogo la shamba tunajiuliza kwa nini viongozi wa dini walipelekwa kwenye bunge la katiba?na kwa nini wanaitwa hapo dodoma? huko ndiko kuchanganya dini na siasa
 
Inaelekea kwamba Sitta alipokuwa anawashutumu Viongozi wa Dini kwa waraka wao, alifanya hivyo kwa baraka za JK. Maneno ya Sitta yanarandana randana na maneno haya ya JK!
 
DOUGLAS SALLU

Rais Kikwete, mbegu uliyoipanda italitafuna taifa letu...
Siyo siri kuwa muasisi wa siasa za maji taka hapa Tanzania ni JK na genge lake la wanamtandao. Mbinu hii aliizanza mapema kabla ya uchaguzi wa mwaka 2005, na wahanga wakubwa wa siasa hizi za kishenzi ni Fredrick Sumaye, Salim A. Salim, Prof.Mark Mwadosya na wengineo, na wahanga hawa walilengwa kwani walionekana kuwa tishio kwa malengo ya JK kuukwaa urais hivyo ilikuwa lazima wachafuliwe kiasi cha kutosha ili wanuke na wakati huo magazeti yakimpamba JK kwa sifa asizostahili, na kweli mbinu hii ya kishenzi ilifanikiwa na JK akawa rais.

Mwaka huu kwa vile kanuni za CCM zilikuwa zinamlinda JK asipate mpinzani toka ndani ya chama hicho hakuwa na haja ya kutumia mbinu hiyo na akawa anajiandaa kushinda kwa kishindo, lakini ghafla upepo ukabadilika baada ya mzalendo wa kweli Dr Slaa kuteuliwa na Chadema kugombea nafasi ya urais, JK baada ya kuona kuwa maji ni marefu kwake na chama chake akarudia tena mbinu yake ya maji taka na ndipo zikasikika habari za Dr Slaa kuchukuwa mke wa mtu, lakini kwa vile watanzania wa leo siyo wale wa mwaka 47, waliimpuuza JK na siasa zake hizo chafu wakaendelea kumuunga mkono Dr Slaa.

Baada ya JK na genge lake kuona kuwa mbini hii haifanyi kazi akaamua kutumia SILAHA YA MAANGAMIZI -
UDINI.

Ukazushwa uvumi kuwa Dr Slaa ametumwa na Kanisa Katoliki, mbinu hii ilikolezwa na magazeti ya fisadi Rostam Aziz na mengine kama Habari Leo, AL HUDA, AL NUR, na kama haitoshi zikatumwa sms kwa mamilion ya wapiga kura kumchafua Dr Slaa na kuhusisha na udini.

Siyo siri kuwa silaha hii imeacha majeraha mengi miongoni mwa Watanzania na mfano hai ni hata hapa jamvini hangover ya siasa hizi za udini zilizo asisiwa na Kikkwete mwenyew e ipo. Dini ni jambo nyeti sana na likitumiwa vibaya linaweza kuilipua nchi nzima na hiki ndicho alichokifanya JK.


https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...uliyoipanda-italitafuna-taifa-letu-print.html

 
Kuna watu maneno ya Kikwete yamewagusa pazuri.

Anaekasirika ndio yeye huyo.

Haoo.
 
Kuna watu maneno ya Kikwete yamewagusa pazuri.

Anaekasirika ndio yeye huyo.

Haoo.
Mahabuba .....Acha unafiki basi maana hapa alikuwa akimjibu LUkuvi.........ama hujui kwanini Falme za Kiarabu na Oman waliwakilishwa? Hujui aliko sultan wewe? Ama ni kwanini Nigeria iliwasilishwa , hujui Bokoharamu weye ? Ama hujui kwanini alienda kuzungumzia hapo siku moja kabla ya kuhutubia taifa?
 
Majanga katika nchi yakitokea utasikia wanasiasa wote wanawaangukia viongozi wa dini ili kuliombea taifa, lkn linapokuja suala la viongozi wa dini kutoa muongozo bora wa uongozi utasikia ohoo.. Msichanganye dini na siasa. Ni upumbavu endapo viongozi wa dini watakaa kimya bila kuingilia na kutoa maonyo juu ya tabia mbaya ya viongozi ambao hawalitakii mema taifa hili kisa tu wanaambiwa wasichanganye dini na siasa.na iwapo viongozi wa dini watakaa kimya basi watakuwa hawajui wajibu wao waliopewa juu ya kukemea uovu.
 
Back
Top Bottom