Rais Kikwete aonya kuingiza dini katika siasa

Rais Kikwete aonya kuingiza dini katika siasa

Huyu Kikwete mnafiki tu, yeye ndiye kinara wa udini hapa Tanzania! Amalize muda wake aende zake.

Tupe ushahidi kama uko nao ndugu tafadhari si yuwafaham uzuri mkono mtupu haurambwiii.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa kuna ushahidi sasa unaothibitisha kuwa baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini wamekuwa wanachaganya dini na siasa wakitumia dini kuunga mkono baadhi ya vyama vya siasa na shughuli za kisiasa nchini.

Aidha, Rais Kikwete amewaomba mabalozi hao “kuiokoa” Tanzania katika majanga makubwa yanayoweza kuipata kwa kutumia dini kuendeleza siasa, hatua ambayo ameielezea kama “njia ya hatari kweli kweli.”

Rais Kikwete alikuwa anazungumza usiku wa Jumatatu, Oktoba 6, 2014, wakati wa chakula cha usiku ambacho alikula na viongozi wa dini nchini ambao wanaendelea na mkutano wao wa mwaka kwenye Hoteli ya White Sands ya Dar es Salaam.

Mkutano huo wa siku nne ulioanza juzi unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence ni mwendelezo wa mikutano ya viongozi wa dini kubwa za Kikristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini. Mkutano wa mwisho ulifanyika mwaka juzi, 2012 kwenye Hoteli hiyo hiyo.

Aidha, Mkutano huo ambao moja ya wadhamini wake ni taasisi ya Programme for Christian-Muslim Relations in Africa (PROCMURA) yenye makao yake makuu mjini Nairobi, Kenya, unahudhuriwa na mabalozi 15 wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini na mashirika kadhaa ya kimataifa likiwemo lile la Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP).

Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika Mkutano huo ni wa Ujerumani, Iran, Marekani, Norway, Uturuki, Sweden, Canada, Denmark, Finland, Misri, Qatar, Uswisi, Palestina, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Saudi Arabia na Umoja wa Ulaya (EU). Viongozi wa dini wanaoshiriki katika Mkutano huo wanatoka Zanzibar, Dar es Salaam, Mwanza, Morogoro, Mtwara, Lindi, Arusha, Geita na Mbeya.

Akizungumza kwenye chakula hicho cha usiku, Rais Kikwete aliungana na Mshauri Mkuu wa PROCMURA ambaye alionya kuhusu hatari za kweli zinazoendelea kuikabili dunia kwa sababu ya kuingiza dini katika siasa (Politicisation of Religion) na kuingiza siasa katika dini (Religinasation of Politics).

Rais Kikwete amewaambia viongozi hao: “Mwakilishi wa PROCMURA ametoa ujumbe mzito sana. Ametoa fumbo ambako amewaasa mabalozi wasiingize dini katika siasa na wasiingize siasa katika dini. Na mimi nataka kuungana naye na kuwaomba mabalozi waiokoe nchi yetu katika majanga makubwa yanayoweza kutokana na kutumia dini kuendeleza siasa. Ni njia ya hatari kweli kweli.”

Ameongeza Rais Kikwete: “Kuna ushahidi sasa kuwa baadhi yetu, baada ya kushindwa kutumia ukabila katika kuendeleza siasa, sasa mmegeukia dini. Mnatumia dini katika kuunga mkono baadhi ya shughuli za kisiasa na baadhi ya vyama vya siasa.”

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.

7 Oktoba, 2014.

Kwenye siasa mheshimiwa rais kakataa, lakini kwenye kuteua wakuu wa idara wa maisha ya umma kama vyuo vikuu, wajumbe wa bunge maalum la katiba, hamasa zingine dhidi ya dini nyingine ni sawa au huko yeye haoni? Mabalozi wamezuiliwa lakini wao kama viongozi ruksa kuacha redio imaan na magazeti ya al-nuur kutukana na kukejeli viongozi wakristo bila tatizo
 
askofu-liberatus-sangu_300_173.jpg

Rais Jakaya Kikwete akimpongeza Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Mhashamu Liberatus Sangu wakati wa ibada ya kumweka wakfu iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Parokia Mama Mwenye Huruma, Ngokolo mjini Shinyanga jana. (Picha na Freddy Maro).

RAIS Jakaya Kikwete amesema wakati taifa likielekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani baadaye mwaka huu, kumeibuka nyufa zinazojengwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa na mashabiki wao ambao wanatumia tofauti za dini zilizopo nchini kwa uchu wa kuingia madarakani.

Kwa hali hiyo, amewaomba viongozi wa dini kuchukua hatua kwa kukemea tatizo hilo ili kuliponya taifa na changamoto hiyo aliyoita kuwa ni kubwa, hasa ukizingatia kuwa Tanzania haina historia ya kuuana wala kugombana kwa sababu ya tofauti za kidini na kikabila.

Rais Kikwete aliyasema hayo jana katika sherehe za kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu Mteule wa Jimbo Kuu la Shinyanga, Liberatus Sangu katika Kanisa Kuu la Mama Mwenye Huruma, Parokia ya Ngokolo mjini hapa.

"Katika kipindi hiki tunachotakiwa ni kubadilika ili kutoingia katika maangamizi… tunaomba viongozi wa dini kuliponya taifa na changamoto hii kubwa ili tudumishe namna ya kuishi pamoja, kwani hatutaki kuingia kwenye ukabila wala udini," alisema Rais Kikwete.

Aliongeza kuwa kama kisingizio ni Katiba Pendekezwa, alisisitiza kuwa masuala ya dini yamerekebishwa hivi sasa hakuna tatizo tena, hivyo kinachotakiwa ni Watanzania kuwa wamoja na kudumisha mshikamano.

Rais Kikwete pia alitumia sherehe hizo kuwataka viongozi wa dini kushirikiana na Serikali kuielimisha jamii juu ya umuhimu wa kuachana na imani potofu ya kuua vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi.

Alionya kama mafundisho yao yakiwaingia vizuri wanajamii, ni dhahiri wataachana na imani kwamba, macho mekundu ya vikongwe si kigezo cha ushirikina, hali kadhalika watafuta imani kuwa viungo vya albano ni chanzo cha utajiri, vikitumiwa na waganga wa kienyeji kung'arisha nyota za wafanyabiashara na wanasiasa.

Akizungumza kwa hisia kali, Rais Kikwete alisema: "Yamekuwepo malalamiko mengi kuwa Serikali haifanyi kazi, lakini hivi sasa kuna watuhumiwa 11 waliokamatwa kwa mauaji hayo ila tayari watuhumiwa 16 wako kwenye orodha ya kunyongwa. "Kama tungekuwa hatufanyi kazi, hata hao tusingewakamata, Magereza yamejaa wahalifu na kila mara nimekuwa nikitoa msamaha."

Alisema kusimikwa kwa Askofu Sangu kumekuja kwa wakati mwafaka, kwani anaamini atashirikiana na viongozi wengine wa dini kuiongoza jamii ili kuondokana na vitendo viovu na vya kikatili dhidi ya vikongwe na albino.

Alitumia fursa hiyo kuwasihi viongozi wa dini kushirikiana na Serikali kuhakikisha jamii inakuwa mahali pazuri pa kuishi.
Rais pia alilipongeza Kanisa Katoliki kutoa mchango mkubwa katika masuala ya elimu na afya kwenye jamii na akamtaka kiongozi huyo kuendelea kushirikiana na Serikali ili kama kuna upungufu atakaouona aeleze ili kanisa na Serikali wajue namna ya kuyatatua ili kuongeza kasi ya maendeleo.

Kwa upande wake Askofu wa Jimbo la Mwanza, Thadeus Ruwa'ichi alimueleza Askofu Sangu kuwa changamoto iliyopo katika eneo lake la kazi ni kuuawa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) pamoja na vikongwe.

"Kama alivyolisema Rais Kikwete, kinachotakiwa ni kuendelea kutoa elimu na ushirikiano wa jamii, jimbo hili ni kubwa lakini tayari unao wasaidizi walio na moyo wa kutenda kazi. Jimbo hili lina waumini zaidi ya 300,000, lina mapadre 18 na jimbo zima lina wahudumu wa kipadre 70, watawa wa kiume wawili na watawa wa kike 70, mafrateli 19," alisema.

Kwa upande wake, Balozi wa Baba Mtakatifu nchini Askofu Mkuu Francisco Padilla, alimpongeza Askofu Sangu kwa kukubali uteuzi huo, kwani umetokana na sala za waumini wa Mkoa wa Shinyanga.

Alitamtaka pia asitende kazi kwa manufaa yake, bali ashirikiane na viongozi wengine kuleta maendeleo na kuwafundisha waumini misingi ya kimaadili kwa njia ya ushirikiano ili kuweza kuondoa changamoto zilizopo.

Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa alimkaribisha katika baraza hilo Askofu Sangu, akisema kanisa linafurahishwa na uteuzi wake kwani kazi yake imeonekana, hivyo sasa ana jukumu la kuwaongoza mapadri na kuwaunganisha wanajamii.

Jimbo Katoliki la Shinyanga, Tanzania kuanzia mwaka 2012 limekuwa wazi kutokana na kifo cha Askofu Aloysius Balina.

Kabla ya uteuzi wake, Askofu Mteule Sangu alikuwa ni Ofisa Mwandamizi katika Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu mjini Vatican. Tangu kifo cha Askofu Balina, jimbo hilo lilikuwa chini ya uangalizi wa Askofu Ruwa'ichi.

CHANZO: Habari Leo
 
tatizo la viongozi wa ccm na serikali yake wanapoambiwa mapungufu yao na viongozi wa dini wanakimbilia kusema kwamba viongozi wa dini wasifanye siasa, wanachotaka wao ni kusifiwa tu,hawataki kukosolewa
 
[h=3]Rais Kikwete Aonya Chokochoko za Siasa Kupitia Dini[/h]
Mpekuzi blog

RAIS Jakaya Kikwete amesema wakati taifa likielekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani baadaye mwaka huu, kumeibuka nyufa zinazojengwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa na mashabiki wao ambao wanatumia tofauti za dini zilizopo nchini kwa uchu wa kuingia madarakani.

Kwa hali hiyo, amewaomba viongozi wa dini kuchukua hatua kwa kukemea tatizo hilo ili kuliponya taifa na changamoto hiyo aliyoita kuwa ni kubwa, hasa ukizingatia kuwa Tanzania haina historia ya kuuana wala kugombana kwa sababu ya tofauti za kidini na kikabila.

Rais Kikwete aliyasema hayo jana katika sherehe za kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu Mteule wa Jimbo Kuu la Shinyanga, Liberatus Sangu katika Kanisa Kuu la Mama Mwenye Huruma, Parokia ya Ngokolo mjini hapa.

“Katika kipindi hiki tunachotakiwa ni kubadilika ili kutoingia katika maangamizi… tunaomba viongozi wa dini kuliponya taifa na changamoto hii kubwa ili tudumishe namna ya kuishi pamoja, kwani hatutaki kuingia kwenye ukabila wala udini,” alisema Rais Kikwete.

Aliongeza kuwa kama kisingizio ni Katiba Pendekezwa, alisisitiza kuwa masuala ya dini yamerekebishwa hivi sasa hakuna tatizo tena, hivyo kinachotakiwa ni Watanzania kuwa wamoja na kudumisha mshikamano.

Rais Kikwete pia alitumia sherehe hizo kuwataka viongozi wa dini kushirikiana na Serikali kuielimisha jamii juu ya umuhimu wa kuachana na imani potofu ya kuua vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi.

Alionya kama mafundisho yao yakiwaingia vizuri wanajamii, ni dhahiri wataachana na imani kwamba, macho mekundu ya vikongwe si kigezo cha ushirikina, hali kadhalika watafuta imani kuwa viungo vya albano ni chanzo cha utajiri, vikitumiwa na waganga wa kienyeji kung’arisha nyota za wafanyabiashara na wanasiasa.

Akizungumza kwa hisia kali, Rais Kikwete alisema: “Yamekuwepo malalamiko mengi kuwa Serikali haifanyi kazi, lakini hivi sasa kuna watuhumiwa 11 waliokamatwa kwa mauaji hayo ila tayari watuhumiwa 16 wako kwenye orodha ya kunyongwa.

“Kama tungekuwa hatufanyi kazi, hata hao tusingewakamata, Magereza yamejaa wahalifu na kila mara nimekuwa nikitoa msamaha.”

Alisema kusimikwa kwa Askofu Sangu kumekuja kwa wakati mwafaka, kwani anaamini atashirikiana na viongozi wengine wa dini kuiongoza jamii ili kuondokana na vitendo viovu na vya kikatili dhidi ya vikongwe na albino.

Alitumia fursa hiyo kuwasihi viongozi wa dini kushirikiana na Serikali kuhakikisha jamii inakuwa mahali pazuri pa kuishi.

Rais pia alilipongeza Kanisa Katoliki kutoa mchango mkubwa katika masuala ya elimu na afya kwenye jamii na akamtaka kiongozi huyo kuendelea kushirikiana na Serikali ili kama kuna upungufu atakaouona aeleze ili kanisa na Serikali wajue namna ya kuyatatua ili kuongeza kasi ya maendeleo.

Kwa upande wake Askofu wa Jimbo la Mwanza, Thadeus Ruwa’ichi alimueleza Askofu Sangu kuwa changamoto iliyopo katika eneo lake la kazi ni kuuawa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) pamoja na vikongwe.

“Kama alivyolisema Rais Kikwete, kinachotakiwa ni kuendelea kutoa elimu na ushirikiano wa jamii, jimbo hili ni kubwa lakini tayari unao wasaidizi walio na moyo wa kutenda kazi. Jimbo hili lina waumini zaidi ya 300,000, lina mapadre 18 na jimbo zima lina wahudumu wa kipadre 70, watawa wa kiume wawili na watawa wa kike 70, mafrateli 19,” alisema.

Kwa upande wake, Balozi wa Baba Mtakatifu nchini Askofu Mkuu Francisco Padilla, alimpongeza Askofu Sangu kwa kukubali uteuzi huo, kwani umetokana na sala za waumini wa Mkoa wa Shinyanga.

Alitamtaka pia asitende kazi kwa manufaa yake, bali ashirikiane na viongozi wengine kuleta maendeleo na kuwafundisha waumini misingi ya kimaadili kwa njia ya ushirikiano ili kuweza kuondoa changamoto zilizopo.

Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa alimkaribisha katika baraza hilo Askofu Sangu, akisema kanisa linafurahishwa na uteuzi wake kwani kazi yake imeonekana, hivyo sasa ana jukumu la kuwaongoza mapadri na kuwaunganisha wanajamii.

Jimbo Katoliki la Shinyanga, Tanzania kuanzia mwaka 2012 limekuwa wazi kutokana na kifo cha Askofu Aloysius Balina.

Kabla ya uteuzi wake, Askofu Mteule Sangu alikuwa ni Ofisa Mwandamizi katika Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu mjini Vatican. Tangu kifo cha Askofu Balina, jimbo hilo lilikuwa chini ya uangalizi wa Askofu Ruwa’ichi.
Mpekuzi blog
 
Haina shida kama haukuwa usanii wa kutangaza kitu hewa ambacho hakikukusanywa ili kuonyesha ulimwengu kuwa kimekusanywa! Au isiwe watu walipewa kabla toka kwa Gwajima Mwenyewe wafanye kutoa alichotoa ili filamu ya kisanii ionekane!

Anyway sina tatizo.Tatizo langu kama hizo hela zilizokusanywa ziliingia akaunti binafsi ya Gwajima badala ya akaunti ya kanisa hapo pana maneno.Lakini kama zilikusanywa ni mali ya kanisa basi najua v milioni mia saba si haba zinatosha kuwapa mitaji waumini wengi wa Kwa GWAJIMA ambao ni malofa wa kutupwa kuweza kuondokana na umaskini.

Lakini kama amepewa Gwajima BINAFSI AKANUNULIE Flora Mbasha GARI la kifahari hapo sikubali.

Wewe una nini mpaka uwaone waumini wa Gwajima ni malofa? Umeishiwa wewe, malofa wanawezaje kumwaga elfu kumi kumi? Unajitutumuuuua kupigana na Gwajima, selikali yako imemshindwa wewe utaweza?mwisho wa Siku utaishia kuwa muumini wake tu
 
dini kanisani na misikitini, masinagogi na mahekaluni, ukitika huko wate ni binadamu mahitaji yetu sawa
 
....si kweli,Rais amesahau kuwa kuna padre aliuwawa kule zanzibar kwa sb tu ya dini yake?,lakini pia kuna mwingine alipigwa risasi ya kidevuni.Hapa nia ilikuwa risasi ya kichwani lakini target tu ndio ilikataa.Lakini pia tumeona pale mbagala ambako makanisa ya SDA,CATHOLIC na LUTHERANI yaliaharibiwa na waumini wa dini ya kislam eti kwa sb tu kuna taarifa kuwa katoto fulani alikojolea quaran ya katoto fulani.Sasa reaction hapa umeisoma?.Hapa kuna kitu.Lakini kama haotoshi kule kagera walokole waliokuwa kwenye mkesha waliuwawa wote kanisani kwao.....hapa kuna kitu.
 
JK angeonya kuhusu siasa na dini, pale ambapo Viongozi wa dini walipomwambia yeye ni CHAGUO LA MUNGU! Kinyume cha hapo, ni unafiki mtupu!
 
Raisi wa nchi ya Kisekula mbona kila mara yupo kwenye Sherehe za Kusimika Maaskofu kwenye Majimbo yao?- Huo Muda si Angefanya kazi za kujenga uchumi, Kupambana na Umasikini Maradhi na Ujinga?- Ndiyo maana tunasema hii nchi Inaongozwa kwa Mfumo Kristo
 
Mwanasiasa au kiongozi wa dini anayetumia dini yake kuwafarakanisha wtz huyo anafikra za kitumwa
 
....si kweli,Rais amesahau kuwa kuna padre aliuwawa kule zanzibar kwa sb tu ya dini yake?,lakini pia kuna mwingine alipigwa risasi ya kidevuni.Hapa nia ilikuwa risasi ya kichwani lakini target tu ndio ilikataa.Lakini pia tumeona pale mbagala ambako makanisa ya SDA,CATHOLIC na LUTHERANI yaliaharibiwa na waumini wa dini ya kislam eti kwa sb tu kuna taarifa kuwa katoto fulani alikojolea quaran ya katoto fulani.Sasa reaction hapa umeisoma?.Hapa kuna kitu.Lakini kama haotoshi kule kagera walokole waliokuwa kwenye mkesha waliuwawa wote kanisani kwao.....hapa kuna kitu.

Najua hauelewi na hautaelewa kamwe unaleta udini hapa kwa hoja hewa,jifunze madahra ya udini kwa mataifa yenye itikadi hizo.
 
Back
Top Bottom