Wakubwa,
Tuliangalie suala hili tofauti kidogo. Hakuna hujuma hapo. Hii ni mara ya kwanza kukamatwa kwa wavuvi Maharamia katika pwani na Tanzania. Kumuhusisha Rais katika suala hili ni kutokuelewa taratibu za ki-Mahakama zinavyofanya kazi. Katika utawala wa Kisheria kama ilivyo hapa kwetu Tanzania, suala likiwa Mahakamani haliingiliwi na yeyote isipokuwa Mahakama yenyewe.
Kwa Maana hiyo Rais hakuwa na mamlaka ya kulizungumza au kulichelewesha aua hata kulifuta mpaka pale Mahakama itakapokuwa imemaliza kazi yake. Jambo la msingi hapa kuepusha tatizo kama hili na mengine kama hayo siku za usoni ni kuangalia na kuzipa uwezo Mahakama zetu na ofisi ya DPP (Mkurugenzi wa Mashitaka) kuweza kusimamia kesi zake kwa haraka na kuweza kuzimaliza kwa wakati ha hapo tutakuwa tumeepuka kumtupia lawama yeyote na pia kuepuka kuwaweka Rais na Mawaziri wake kwenye mapambano ambayo ni ya kufikirika na kusadikika tu.
Hoja hapa ni uwezo wa Mahakama zetu kuendesha kesi kwa haraka na ufanisi ili kuweza kusimamia na kutoa haki katika jamii husika. Lakini si Mahakama pekee na jeshi la Polisi na Mwanasheria Mkuu na DPP wote wanahitaji kuwa na Raslimali watu na vifaa vya kuwawezesha kufanya kazi zao kwa wakati na kuweza kusimamia haki pale inapokuwa inastahili.
Nakubali mkuu hapo umenena lkn kwa ticket ipi sasa?au ajiunge na CCJ maana vyama vingine ndo kuna longolongo sanaNakubaliana na wewe lakini si kwa tiketi ya CCM.
As longer as atashika nchi kwa tiketi ya chama hiki mambo ya Longolongo yataendelea kama kawa.
ninachoshangaa ni kwa nini Budget iliyotumika ilikuwa ni ile ya idara ndani ya wizara hiyo, kweli hapo aliachwa pekee. Lakini pia haiingii akilini kwa nini Mheshimiwa rais ampige vita waziri aliyemteua mwenyewe. Kama hamtaki asingemchagua toka day one, hana sababu ya kufanya hivyo leo. chunguzeni zaidi leteni hoja, hiyo hapo is not water tight.
acheni porojo, kwani nani kati yenu aliepiga kura ya kumchagua magufuli kwenye uwaziri, mnge juaje utendaji wake kwenye hiyo wizara kama sio busara ya Rais kuunda wizara hiyo? kama suala la kutumia bajeti yake kuhudumia hao samaki kwani tatizo liko wapi, hakuna pesa iliyokuwa inazagagaa. Mema ya Waziri mnayatenganisha na Rais, bt Mabaya ya waziri lazima muunganishe na Rais?? jifunzeni kufikiri kabla ya kusema.Kikwete ni Tishio ukibisha rejea 2005 au subiri Octoba2010 then unikumbushe kama utakuwa na ujasiri wa kukumbuka kunikumbusha!!!!!!!!!!
Luteni,
Kama huwezi kuiona inakuwaje unasema Rais anamhujumu Waziri Magufuli au ni kupiga porojo na mbwembwe?
Sun Tzu sijakuelewa nilichosema inawezekana kabisa Magufuli akawa anahujumiwa ila kwa macho ya kawaida unaweza usijue sasa kutokuona kwa macho si kwamba hakuna hujuma au unasemaje
Luteni,
Hoja ya msingi ni kwamba huyu Mheshimiwa anahujumiwa na Rais Kikwete, mimi nasema lahasha, tuboreshe na kukuza ufanisi na uwezo wa Mahakama, ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka na uwezo wa kipolisi wa kuchunguza na kuhitimisha uchunguzi kwa haraka na kuzipeleka kwa Mkurugenzi wa Mashitaka na AG zikiwa zimekamilika na hapo ndiyo haki itakuwa imetendeka bila ya mtu kudhulumiwa au kuwekwa ndani pasipo ushahidi wa kutosha. Lakini tukikimbilia kusema kuwa Rais anamhujumu Magufuli wakati hatuna ushahidi na ukiulizwa unasema ushahidi unaweza kuwepo lakini hauonekani hapo unakuwa hujitendei haki katika fikra zako na hata sisi wengine tunaosoma unachokiandika kwani zinakuwa hazitofautiani sana na porojo.
nakubaliana na wewe lakini si kwa tiketi ya ccm.
As longer as atashika nchi kwa tiketi ya chama hiki mambo ya longolongo yataendelea kama kawa.
mfano mzuri ni mh pinda, alivyochukuwa nafasi ya lowasa ilidhaniwa na watanzania kwamba nuru mpya imeangaza na kiama cha mafisadi kimewadia. Tatizo hatukuwazia kwamba bado yupo ndani ya ccm. System imembana vilivyo na sasa hivi amageuka kuwa mpambe wa kina rostam tena kwa gharama ya kulitukana benge kwa kuwaaminisha wananchi kwamba mijadala ya bungeni ni porojo.
umepotea mkuu!
Unachosema ni kweli, magufuli anajihujumu mwenyewe! Akiwa ccm hadithi zitakuwa zina recycle zile zile. One simple test, if he cares for people aondoke ccm.
wewe nawe ni mwizi wa mali y a umma nini?Mnamponza Magufuli.
mwenda wazimu hutambulika kwa matendo yake, unachojaribu kupenyeza, hakiwezi kufanikiwa labda kwa maamuma..kuna madai kwamba, Magufuli alilazimisha ujenzi wa barabara jimboni kwake kwa kutumia madaraka yake ya Uwaziri wa Ujenzi na Miundo mbinu.
..Magufuli tena akatumia ubabe na kukiuka ushauri wa wataalamu wake na kuvunja kituo cha mafuta kule Mwanza. Mahakama Kuu imetoa hukumu kwamba serikali ilipe fidia ya shilingi bilioni 15.
..Magufuli tena amehusika na kashfa ya viongozi kujiuzia nyumba za serikali kwa bei ya kutupa. katika kashfa hiyohiyo Magufuli anatuhumiwa kuwauzia ndugu na rafiki zake nyumba za serikali.
..KAMA KWELI MAGUFULI NI MSAFI NA ANA NIA NJEMA NA TAIFA HILI BASI ARUDISHE NYUMBA YA SERIKALI ALIYOJITWALIA.
..WATANZANIA TUNALILIA MAPESA NA MALI ZILIZOFICHWA NJE[SWISS,DUBAI] YA NCHI ZIWE-RECOVERED WAKATI TUNA MALI/NYUMBA ZETU HAPAHAPA NCHINI KWANINI ZISIREJESHWE?