Rais Kikwete anamhujumu waziri Magufuli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete anamhujumu waziri Magufuli?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzizi wa Mbuyu, Mar 3, 2010.

 1. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,755
  Likes Received: 1,532
  Trophy Points: 280
  Jamani hii nimeipata kwenye chanzo kimoja cha uhakika mno; kwamba wale samaki wa magufuli walikuwa wanakwama kuuzika kutokana na hujuma za Raisi wa Tanzania JM Kikwete dhidi ya Dk Magufuli.
  Chanzo hicho kimesema kwanza alijaribu kufunika na kudakia kazi ile ya kukamata jodari ili ionekane ni yeye aliyefanya lakini ikashindikana kwani watu waliendelea kumpongeza Magufuli tu.
  Ndipo alipokuja na mbinu mpya lengo likiwa ni kumpunguzia umaarufu Magufuli ili aonekane alifanya zoezi la kamatakamata samaki Jodari kwa kukurupuka na zoezi zima limeiletea hasara nchi..kama kwaida yake Kikwete alitumia vyombo vya habari na "UWT". Lakini kwa bahati mbaya kwake Raisi, Magufuli alifanikiwa kujua mapema hila hizo na akazisambaratisha kwa hoja zenye busara mno, kama vile Serikali inapofanya kazi yake kwa kufuata sheria hakuna hasara, akatoa mfano wa "mwizi wa vitumbua anavyohudumiwa na serikali kwa gharama kubwa kuliko alichoiba"
  Inasemekana hujuma za Kikwete na wanamtandao kwa ujumla dhidi ya Magufuli hazikuanza hivi karibuni, hofu yao kubwa ni kukubalika kwa Magufuli miomngoni mwa watanzania kuona ni hatari kwa mbinu zao(wanamtandao) za kurithishana Uraisi wa TZ.
   
 2. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #2
  Mar 3, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  hiki kitu kinahitaji ujasiri kukifikiria, na ukifanikiwa kukifikiria kwa mtazamo huu kweli unapata jibu.
  binafsi nimewahi kufuatilia hili swala kwa kina , nakuziangalia sheria zetu hasa za UVUVI sehemu ya EEZ[EXCLUSIVE ECONOMIC ZONE]
  hakika Magufuli alifanya kile ambacho sheria za Kimataifa za uvuvi katika ukanda huo wa kiuchumi ulimruhusu.,
  kilichoshangaza ni kule mamlaka za kimahakama , ofisi ya Mwanasheria Mkuu, DPP zilivyokua zinaboronga kwenye swala zima, hadi ilifikia mahala Magufuli alitupiwa Zigo lote binafsi na yeye akaonekana kama msemmaji pekee wa sakata zima, huku mamlaka za kipolisi, jeshi na hata UWT zikiwa Kimya.
  niliwahi kumsikia waziri huyu wa Uvuvi akilalamika kuhusu sakata lile lote kuelekezwa kwenye wizara yake.
  mara zote Rais amekuwa mkimya , na ninasikia Wizara ya samaki na Mifugo ndo wamelipa gharama zote za utunzaji wa samaki hao kupitia bajeti yao ya kawaida.
  nahisi upo ukweli kuna kukwamishana kwa faida za kisiasa.
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,831
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  hiyo ndiyo nchi yetu!!!
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,231
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Mbona hii iko live miaka yote ya JK?
  Makufuli anabaniwa wazi kabisa...Lakini bahatimbaya kila wanakomficha ana wika na kuwaonyesha kuwa ni star wa utendaji...Shame on these betrayers!
   
 5. K

  Kabengwe JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2010
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Magufuli poses threat kwa muungwana
  Lazma muungwana amnyamazishe, that's politics
  Ila ni aibu sana kwa Rais kushindana na Waziri wake, huko ni kutokujiamini kwa hali ya juu sana!
   
 6. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mnamponza Magufuli.
   
 7. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2010
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 6,942
  Likes Received: 23,652
  Trophy Points: 280
  Magufuri anatisha na anaogopesha na kama itatokea akashika nchi mambo ya longolongo yatapotea
   
 8. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,755
  Likes Received: 1,532
  Trophy Points: 280
  How?
   
 9. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #9
  Mar 3, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Magufuli anabebwa na uhodari wake, staha yake, na haitaji sifa za kijinga kumfanya awe maarufu ama mtu anaechapa kazi.
  kama ilivyo kwa kila binadamu anamapungufu yake, ila mambo mema mengi anayoyafanya hapa TZ yanafunika hayo madhaifu.
  Kumbukeni issue ya hao Jodari ilivyokuwa, walipokamatwa tu, ikulu ikatoa taarifa yakuwapongeza wote waliohusika, kisha wakaitwa Ikulu, wakapongezwa na Rais.
  kisha tangu hapo Ikulu imekauka, kwanini isitumike pesa ya dharula katika kulipa gharama za ile meli ?
  nasikia Bajeti ya Idara inayohusika na samaki imekwama , mambo hayaendi, wanataka aonekane hajui kufanya kazi vyema.
   
 10. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,937
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na wewe lakini si kwa tiketi ya CCM.
  As longer as atashika nchi kwa tiketi ya chama hiki mambo ya Longolongo yataendelea kama kawa.
   
 11. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #11
  Mar 3, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,903
  Likes Received: 1,133
  Trophy Points: 280
  Magufuli ni mchapakazi, kichwani anapeta ile mbaya!! Sasa kwa hili kwa nini hao wanaopiga bla bla wasimchukie na kutaka kumwangusha!!!! Hon. Magufuli usikate tamaa, tulikuheshimu tangu ulipokuwa hasa Wizara ya ardhi, na ulipotoka tu, kumerudi kama zamani, rushwa kuanzia reception!!! Hupati file pale bila kutoa kitu kidogo.Viwanja ndiyo hivyo, tena. Maneo ya wazi yameisha kuuziwa wakubwa, hata wengine kule Mbezi Beach wanataka kufunga street road kwa kuwa eti kuna michoro mipya imetolewa!! Hivi michoro hiyo inafuta street roads?? Magufuli Hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee. Jitose urais 2015 utapata!!! Nitapiga kura kwa mara ya kwanza tena tokea mwisho wa uchaguzi wa Baba yangu wa Taifa aliyehakikisha nimesoma na kutibiwa bure mpaka nikawa health mentally and physically capable. R.I.P!
   
 12. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,935
  Likes Received: 384
  Trophy Points: 180
  Huyu Jamaa anatufaa sana, Alisimamia sana MABARABARA, na akawaadabisha makandarasi feki, na wale waliotaka kuuza pale NYAMAGANA, tunamhitaji awe RAIS, nadhani ndo maana CCM wanaogopa mgombea binafsi
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,484
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Lakini swali ni..

  Kuna jipya hapa??
   
 14. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kama ndio kutegeana basi wote wanategena maana mzee wa kaya naye ni mtu wa sifa sana na anapenda sana kuongoza kwa sifa za watu na hulka za watu wanasemaje
   
 15. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #15
  Mar 3, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 925
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  Magufuli alipokuwa Wizara ya Miundo Mbinu alifanya mambo makubwa hadi kufikia kuonekana kuwa tishio. Haikushangaza kusikia "kalishwa" sumu hadi kwenda kupata matibabu nje. Kwa umaarufu aliojijengea katika awamu ya tatu, akaonekana anaweza "kum-overshado" jk kama agapewa wizara nyeti. Kwa maana hiyo, kwa "kutupwa"kwenye wizara ya kitoweo, wenye serikali yao walifikiri ndo mwisho wa nyota yake kung'ara. Lah haulah! samaki wa johari wakakamatwa, mara wanabadilishwa jina kuitwa "samaki wa magufuli". Ungetegemea nini zaidi ya kuhujuma juhudi hizi? Msishangae baada ya uchaguzi akapewa kazi ya Ubalozi Chile au Haiti!
   
 16. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #16
  Mar 3, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kweli Magufuri amefanya mengi mazuri na rekodi yake ya utendaji inawapita kwa mbali sana wanasiasa wetu wa kizazi hiki. Tatizo ni mfumo, unaweza kumbadilisha mtu, labda awe na ngozi ngumu kama Bingu wa Mutharika aliyekwenda kinyume na wanasiasa wezi ili kuinusuru nchi yake. Magufuri aliwahi kusimamia na kutetea kwa kauli zake mara kwa mara uuzwaji wa nyumba za serikali. Utetezi wake haukuingia kwenye vicha vya watanzania. Nakumbuka Jenerali ulimwengu aliwahi kuandika kuwa suala la kuuza nyumba za serikali amelifikiria kwa muda mrefu na mara kwa mara lakini hakupata mantiki yake.

  Je Magufuli anaweza kuwa kama Bingu wa Mutharika aliyeenda kinyume na wanasiasa wenzake kwa manufaa ya umma? Kikwete yeye hoi, yupo taabani ndani ya mifuko ya mafisadi.
   
 17. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #17
  Mar 3, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Magufuli ni Waziri katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo kiongozi mkuu/Rais ni JK. Waziri yeyote akifanya jambo jema ama baya katika utekelezaji wa shughuli za kiserikali anafanya kwa niaba ya Rais. Magufuli ni Waziri hodari na mchapakazi asiyeogopa kutekeleza wajibu wake ipasavyo na anafanya hivyo kwa niaba ya Rais vilevile. Rais anawezaje kumhujumu subordinate wake? Akitaka anaweza tu kuteua mwingine kushika nafasi ile badala ya kumhujumu. Tusimpalie makaa Magufuli bila kujijua!
   
 18. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #18
  Mar 3, 2010
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hivi unajua kuwa baada ya samaki kukamatwa, waliohusika katika lile zoezi walipongezwa akiwemo Magufuli, na walipongezwa na Kikwete.

  Kuhusu kuzuia samaki wasiuzwe mapema sikubaliabi nawe, wakati Serikali ilipoomba kibali Mahakamani kugawa hao Samaki bure, Jaji aliyekuwa akisikiliza hiyo kesi aliona kibali cha Serikali kina makosa makubwa, kumbuka hao Samaki japo walikamatwa katika eneo letu, lakini kesi ilikuwa Mahakamani. Na hii kesi inahusu mataifa mengine (meli sio yetu, na hata wavuvi walikuwa toka mataifa mengine), ni lazima Mahakama ijitahidi kufuata taratibu ama sivyo nchi inaweza ingia katika mgogoro na mataifa mengine. Hivyo Jaji baada ya kukataa hati ya kiapo, ndio ilichelewesha uuzaji wa hao samaki. Isifikie kila jambo tuaingiza Siasa, mahakama zetu hazitafanya kazi kwa haki.
   
 19. annamaria

  annamaria Senior Member

  #19
  Mar 3, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Lisemwalo lipo manake huyu mkulu Magufuli ni tishio sana kwa watendaji wababaishaji.Nyota yake inang'ara kwa merits na siyo ujanja ujanja wa kuwanunua wanahabari na kuwahadaa wananchi.
  Siyo siri huyu mkuu siku anaukwaa Urais,basi within 5years tu tungeona mabadiliko makubwa sana Tanzania.Bahati mbaya watu kama Magufuli katika siasa zetu hawana nafasi.Ndiyo maana sometimes nakereka sana manake watendaji wazuri tunao lakini wanapigwa vita kwa maslahi binafsi.
  Mkapa leo kesho haachi kumsifia na kumshukuru Magufuli kama waziri aliyeiletea sifa kubwa serikali yake.
  Go Magufuli go,as long as umma upo upande wako basi ile siku ya vikwazo wako kuumbuka iko njiani inakuja.
   
 20. nzalendo

  nzalendo JF-Expert Member

  #20
  Mar 3, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,870
  Likes Received: 2,717
  Trophy Points: 280
  Si mnakumbuka walishajaribu kumkill?
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...