Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 301
Wakubwa,
Tuliangalie suala hili tofauti kidogo. Hakuna hujuma hapo. Hii ni mara ya kwanza kukamatwa kwa wavuvi Maharamia katika pwani na Tanzania. Kumuhusisha Rais katika suala hili ni kutokuelewa taratibu za ki-Mahakama zinavyofanya kazi. Katika utawala wa Kisheria kama ilivyo hapa kwetu Tanzania, suala likiwa Mahakamani haliingiliwi na yeyote isipokuwa Mahakama yenyewe.
Kwa Maana hiyo Rais hakuwa na mamlaka ya kulizungumza au kulichelewesha aua hata kulifuta mpaka pale Mahakama itakapokuwa imemaliza kazi yake. Jambo la msingi hapa kuepusha tatizo kama hili na mengine kama hayo siku za usoni ni kuangalia na kuzipa uwezo Mahakama zetu na ofisi ya DPP (Mkurugenzi wa Mashitaka) kuweza kusimamia kesi zake kwa haraka na kuweza kuzimaliza kwa wakati ha hapo tutakuwa tumeepuka kumtupia lawama yeyote na pia kuepuka kuwaweka Rais na Mawaziri wake kwenye mapambano ambayo ni ya kufikirika na kusadikika tu.
Hoja hapa ni uwezo wa Mahakama zetu kuendesha kesi kwa haraka na ufanisi ili kuweza kusimamia na kutoa haki katika jamii husika. Lakini si Mahakama pekee na jeshi la Polisi na Mwanasheria Mkuu na DPP wote wanahitaji kuwa na Raslimali watu na vifaa vya kuwawezesha kufanya kazi zao kwa wakati na kuweza kusimamia haki pale inapokuwa inastahili.
Unaweza usiione hujuma kwa macho ya kawaida lakini ikawepo vile vile unaweza kusingizia Mahakama na DPP kuchelewesha kesi kumbe ndipo hujuma inapoanzia mara ngapi DPP anakalia kesi zilizowazi kabisa kesi za EPA,BOT nk ni wangapi wamefikishwa mahakamani kwa hiyo hujuma si lazima rais mwenyewe aende kuzuia kitu inaweza kutekelezwa kwa mbinu mbalimbali halafu umeongelea zaidi hawa samaki wa juzi umeshindwa kuoanisha mtiririko mzima wa matukio toka Magufuli yuko wizara ya miundombinu