Mimi naomba kuhitilifiana na nyinyi nyote,, kwani Magufuli yupo pale kwa kuteuliwa na raisi, Raisi akiamua vinginevyo Magufuli tutahangaika nae mitaani, chonde chonde jamani,
Kuna mtoa hoja mmoja alisema usipoliangalia hili kwa makini unaweza kujiuliza JK ambaye ni bosi wa Magufuli anawezaje kumhujumu waziri wake anayemsaidia! na wengi humu naona wanaiangalia hoja hii kwa mtazamo huo lakini inawezekanaMagufuli ni Waziri katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo kiongozi mkuu/Rais ni JK. Waziri yeyote akifanya jambo jema ama baya katika utekelezaji wa shughuli za kiserikali anafanya kwa niaba ya Rais. Magufuli ni Waziri hodari na mchapakazi asiyeogopa kutekeleza wajibu wake ipasavyo na anafanya hivyo kwa niaba ya Rais vilevile. Rais anawezaje kumhujumu subordinate wake? Akitaka anaweza tu kuteua mwingine kushika nafasi ile badala ya kumhujumu. Tusimpalie makaa Magufuli bila kujijua!
JK nimegundua ni mfuasi mkubwa wa 48 laws of power alizoandika Robert Greene.Na hasa law namba7,ya let people work for you,take credit always
Pia Magufuli ni mchapakazi sana.Nadhani pia ukaribu wake na Urafiki8 wake mkubwa na Raila Amolo Odinga wa kenya umechangia mfanano wao wa kiutendaji
Nakumbuka ile kashfa ya kumuuzia nyumba kimada,sijui ni kweli au ilitengenezwa na mtandao ktk harakati zao?
Huyu akiwa Rais Tanzania basi tutakua tumepiga hatua maanake ana kaudikteta flani hivi ambako watanzania wanakahitaji ili wafanye kazi
To me, huu ni upuuzi mwingine tu. Maana Magufuli anafanya kazi chini ya Kikwete kwahiyo kukamata samaki ni sehem ya majukum yake. Hivi inakuwaje mafanikio ya serikali anahusishwa mtu specific lakini ikitokea tatizo Rais ndio anaandamwa. Kikwete anaouwezo wa kumdhibiti Magufuli hahitaji kumvizia. Anaweza hata kumtoa kwenye baraza la mawaziri akabakia kuwa mbunge. Naitazama hoja hii kama ni hoja yenye mapungufu au ya uongo. Hii ni very low yaani hata haifikiriki.Jamani hii nimeipata kwenye chanzo kimoja cha uhakika mno; kwamba wale samaki wa magufuli walikuwa wanakwama kuuzika kutokana na hujuma za Raisi wa Tanzania JM Kikwete dhidi ya Dk Magufuli.
Chanzo hicho kimesema kwanza alijaribu kufunika na kudakia kazi ile ya kukamata jodari ili ionekane ni yeye aliyefanya lakini ikashindikana kwani watu waliendelea kumpongeza Magufuli tu.
Ndipo alipokuja na mbinu mpya lengo likiwa ni kumpunguzia umaarufu Magufuli ili aonekane alifanya zoezi la kamatakamata samaki Jodari kwa kukurupuka na zoezi zima limeiletea hasara nchi..kama kwaida yake Kikwete alitumia vyombo vya habari na "UWT". Lakini kwa bahati mbaya kwake Raisi, Magufuli alifanikiwa kujua mapema hila hizo na akazisambaratisha kwa hoja zenye busara mno, kama vile Serikali inapofanya kazi yake kwa kufuata sheria hakuna hasara, akatoa mfano wa "mwizi wa vitumbua anavyohudumiwa na serikali kwa gharama kubwa kuliko alichoiba"
Inasemekana hujuma za Kikwete na wanamtandao kwa ujumla dhidi ya Magufuli hazikuanza hivi karibuni, hofu yao kubwa ni kukubalika kwa Magufuli miomngoni mwa watanzania kuona ni hatari kwa mbinu zao(wanamtandao) za kurithishana Uraisi wa TZ.
You are very smart ni wachache sana watakaokuelewa unataka nini nimechukua maneno yako manne tu Laws za Robert Greene, rafiki wa Odinga, kashifa ya kimada wake na ana kaudikteta mwisho umemsifia ni mchapakazi....?????
Mimi naomba kuhitilifiana na nyinyi nyote,, kwani Magufuli yupo pale kwa kuteuliwa na raisi, Raisi akiamua vinginevyo Magufuli tutahangaika nae mitaani, chonde chonde jamani,
Duh,nini tena mkuu?
Kwaharaka unaweza kuona kuwa huu ni upuuzi kwelikweli, ila kataka harakati za ujenzi wataifa lipo jambo la kufikiria, Je kama mkuu wa nnchi anafadhaishwa kwanamna umaarufu wake na waSerikali KW UJUMLA.To me, huu ni upuuzi mwingine tu. Maana Magufuli anafanya kazi chini ya Kikwete kwahiyo kukamata samaki ni sehem ya majukum yake. Hivi inakuwaje mafanikio ya serikali anahusishwa mtu specific lakini ikitokea tatizo Rais ndio anaandamwa. Kikwete anaouwezo wa kumdhibiti Magufuli hahitaji kumvizia. Anaweza hata kumtoa kwenye baraza la mawaziri akabakia kuwa mbunge. Naitazama hoja hii kama ni hoja yenye mapungufu au ya uongo. Hii ni very low yaani hata haifikiriki.
Si mnakumbuka walishajaribu kumkill?
Mnamponza Magufuli.
kwanini matatizo ? remember Jamii Forums , the home of great thinkers where we dare to talk Openly.....ongea kilichokweli kwa hoja maridhawa, tetea unavyoona kwa hoja maridhawa, shambulia uonavyo kwa hoja za kweli, pongeza inapobidi, matusi si mahala pake,MWACHENI Dr. Magufuli. Mtamsababishia matatizo bure.